Waziri Bashe tulipeni hela zetu wakulima tuliouza mbegu ASA, tunaumia

TENGEFU

Senior Member
Jan 25, 2017
138
206
Mimi ni mmojawapo wa wakulima tulioingia mkataba na wizara ya Kilimo kuzalisha mbegu bora za kilimo kupitia wakala wa uzalishaji wa mbegu bora za Kilimo; ASA.

Ni takribani miezi 9 sasa tangu Agosti na September mwaka 2021tulizalisha na kuuza mbegu kwa mujibu wa mkataba wa uzalishaji hadi sasa tunadai mamilioni ya malipo yetu na hakuna dalili ya kulipwa.

mkataba ulitutaka tuzalishe kwa gharama zetu kuanzia kuandaa shamba hadi uvunaji na tutakapomaliza kukabidhi mbegu a kuwa approved by TOSCI tutalipwa hela zetu.

ASA kama taasisi ndani ya wizara anayoongoza Mh. Bashe imeshindwa kutulipa asilimia kubwa ya madai yetu na hii imepelekea baadhi ya wawekezaji/wakulima wa mbegu kushindwa kuendelea na uzalishaji mwaka huu 2022. madeni makubwa wazalishaji wa mbegu waliyoingia kwa ahadi ya kulipwa hela mara watakapo kabidhi mbegu yamepelekea baadhi yetu kuuza vitu vyao kugharamia kulipa madeni.

Naomba kumbusha Mh. Bashe kuwa anapozungumzia kuinua uchumi wa vijana ni vema pia ashughulikie kero yetu maana sisi tuna mtazamo tofauti. Ni aibu kwa wizara yenye vyanzo vingi vya mapato kuwadhulumu wakulima ili kuendesha shughuli zake.

Hivi kwa namna hii mnaondoa umaskini au mna wazamisha watanzania kwenye umaskini.
 
Pole sana mkuu, umeandika kwa hisia sana, kama wamevunja makubaliano mjipange kwa umoja wenu mtafute haki mahakamani.
 
Back
Top Bottom