Waziri Bashe, Kilimo hakihitaji maafisa wa serikali walio committed, kinahitaji ushiriki wa wanasiasa na matajiri

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Nadhani wote tunashuhudia namna wabunge wanavyolinda na kupiga kelele zinapotajwa posho na maslahi Yao. Ni mashuhuda kwamba Mzee Pinda linapokuja suala la ufugaji wa nyuki yupo radhi afunge safari kwenda Kwa Mhe. Mkubwa wa nchini kulitolea ufafanuzi, tunafahamu nguvu watakayotumia akina Zitto pale utakapoporomosha soko la korosha nchini nk.

Mifono hii inatosha kusema popote ambapo mwanasiasa amewekeza kelele zinakuwa kubwa na sera za nchi zinazingatia kelele hizo. Leo Mhe. Bashe anaangaika na maafisa Ugani Jambo ambalo ni jema ila amewahi kuwaza kuwashawishi wanasiasa walime mahindi, walime alzeti, walime michikichi nk Ili wamsaidie kulinda soko?

Ni kawaida kusikia wakulima wamevuna na soko let say la mahindi nchini Zambia lipo vizuri; then unamsikia Waziri au Mkuu wa Mkoa akitamka hakuna mkulima wa Tabora, Rukwa na Katavi kuuza mahindi nje. Ukisikia kauli hii unabaini wazi kwamba hapa hakuna mwanasiasa mwenye mahindi ndani anayeathirika na katazo hili. Au kama wapo basi wanatafuta mbinu yakununua Kwa Bei ndogo wapeleke Dsm then wasafirishe Kwa njia nyingine.

Nimwombe Mhe. Bashe asiangaike kutumia gharama kubwa kuhusu maafisa Ugani , atengeneze wakulima wakubwa then wakulima wataajiri maafisa Ugani na siyo serikali. Leo ukipata mwekezaji mkubwa wa Kilimo kutoka nje usitegemee atatumia maafisa Ugani wa serikali , ataajiri watu wake Kwa qualification anazozitaka.

Mwisho; ufuguja wa kuku nchini unakua Kwa Kasi, Lakini madaktari wa kuku awatoki serikalini wanazalishwa kwenye jamii au kuajiriwa kufanya kaz Kwa utaalam walionao.

Mhe. Bashe; tatizo la Kilimo siyo wataalam,tatizo ni nani anajihusisha na Kilimo na analindwa VIPI kumjengea confidence ya Kilimo? We need political will inline with political gurus paticipation in this sector.
 
Very good Observation.

Yaani Ahangaike na FARMERS/MAKABAILA ambao kimsingi hao ndiyo Watakaoweza kufanyiwa Marketing

Kila Mkoa ukiwa na WAKULIMA WAKUBWA 100 TU-TANZANIA TUNAWEZA KUWA HUB YA CHAKULA AFRICA NA ULAYA.

MKULIMA anayelima Hector 1000 plus...

Hiyo Mapping ikifanyika vizuri-Tanzania inahama kwenye umasikini...

Wizara iwajibike na STORAGE FACILITIES NA MASOKO YA KIMATAIFA.

Modelled ya Financing ihusike kwenye kuweka pesa kwenye Miradi ya watu hao.

WAKULIMA wengine wadogo wajiunge kwenye vikundi vidogovidogo ili washiriki kwenye iyo chain...

Hapo ndipo tunapotakuwa kufanyiwa kazi!!
 
Bashe ameanza vizuri cha kuongezea hapo Mheshimiwa Bashe ni kuweka mfumo utakaowafanya hao mabwana shamba kuwajibika watakaporudi vijijini. Mfumo huo uwe monitored kila siku na ikiwezekana wawekewe target kabisa. Tukiwaacha hivi hivi watarudi vijijini wataendelea na kazi zao kama zamani. Bwana shamba anaamka asubuhi anaenda zake twn mpaka kuwe na ishu ya muhimu sana ndo anatokea kijijini
 
Hii kitu ya kuzuia watu wasiuze mazao yao au kuwapangia namna ya kuuza sijawahi kuielewa, nafikiri ndio maana watu wenye pesa zao hawataki kuziweka kwenye kilimo kwa ajiri ya upuuzi kama huu
Bahati mbaya hii kitu sio sera, ni matakwa ya mtu. Tukipata mshamba kama Bwana yule ndio hivyo tena. Kiukweli haina maana.
 
Hakuna Afisa kilimo anayewafundisha watu kulima kwa sababu hata yeye mwenyewe siyo mkulima Bali mwanafunzi aliyehitimu fani ya kilimo.

Hakuna afisa Ugani anayedhibiti ubora wa mbolea nchini, hakuna afisa Ugani anayedhibiti ubora wa mbegu Kwa sababu hata vifaa vya kuangalia ubora wa mbegu hakuna.

Tunahitaji mapinduzi makubwa ya kilimo nchini, kama tunaoamini maafisa Ugani ndio wataalam wetu basi jukumu la kwanza Liwe udhibiti katika ngazi ya kiwanda na bandari zetu; akitoa certificate ya ubora wa mbolea na mbegu then mbegu hiyo ikagoma kuota Kwa ubora mdogo awajibishwe.

Lakini kwanini mbolea na pembejeo feki zinawafikia wakulima? Jibu ni Moja TU; ni kwasababu anayeathirika ni mkulima mdogo na siyo tajiri wala mwanasiasa.

Na hapa ndipo hoja yangu iliyo; tukiwa na wakulima wakubwa watawekeza wao wenyewe kwenye ubora wa mbegu Lakini wao pia watatuajiri sisi wadodo na hivyo tutakuwa na uhakika wa salary iwe kiangazi au masika.

Ndo maana nikasema Mhe. Bashe anaweza kuwa anawaza sawasawa na anatamani mengi ila Kwa mfumo wetu wa siasa ambao Hana uhakika wa kudumu kwenye uwaziri yeye afikiri Kuhusu sera na sheria zakumlinda mkulima huku zikiwavutia matajiri. That one will last for years, transfer na kupanga vituo vya kazi iwe kazi ya maafisa utumishi na wakurugenzi.

I'm not bulling him but I'm trying to tell him how better he can preach and convert more believers in his presence or absence.

Aanza kuunganisha wizara yake na wizara nyingine aondoke kwenye thinking za Kila idara na majukumu yake; atekeleze Kwa vitendo wish ya Katibu Mkuu Kiongozi na Mhe. Rais ya kuyavilunja vunja majukumu ya serikali Yawe yanasomana. Integration ya activities za wizara yake na wizara nyingine it's key aspect kwenye mapinduzi ya kiwanda
 
Very good Observation.

Yaani Ahangaike na FARMERS/MAKABAILA ambao kimsingi hao ndiyo Watakaoweza kufanyiwa Marketing

Kila Mkoa ukiwa na WAKULIMA WAKUBWA 100 TU-TANZANIA TUNAWEZA KUWA HUB YA CHAKULA AFRICA NA ULAYA.

MKULIMA anayelima Hector 1000 plus...

Hiyo Mapping ikifanyika vizuri-Tanzania inahama kwenye umasikini...

Wizara iwajibike na STORAGE FACILITIES NA MASOKO YA KIMATAIFA.

Modelled ya Financing ihusike kwenye kuweka pesa kwenye Miradi ya watu hao.

WAKULIMA wengine wadogo wajiunge kwenye vikundi vidogovidogo ili washiriki kwenye iyo chain...

Hapo ndipo tunapotakuwa kufanyiwa kazi!!

Wakulima wakubwa tunao tena watanzania wenyewe, tunahitaji wengi zaidi waingie kwenye kilimo kama huyu na serikalili iongeze support na kuacha kuingilia watu, na bank zetu nazo interest zipo juu sana
 
Asilimia kubwa ya watanzania wanajihusisha na kilimo.

Serikali iangalie namna ya kuwawezesha wananchi wafanye kilimo chenye tija.

Swala la kuhangaika na wawekezaji ambao tayari wanaweza kufanya lolote lisiwe kipaumbele cha serikali yetu.
 
Hakuna Afisa kilimo anayewafundisha watu kulima kwa sababu hata yeye mwenyewe siyo mkulima Bali mwanafunzi aliyehitimu fani ya kilimo.

Hakuna afisa Ugani anayedhibiti ubora wa mbolea nchini, hakuna afisa Ugani anayedhibiti ubora wa mbegu Kwa sababu hata vifaa vya kuangalia ubora wa mbegu hakuna.

Tunahitaji mapinduzi makubwa ya kilimo nchini, kama tunaoamini maafisa Ugani ndio wataalam wetu basi jukumu la kwanza Liwe udhibiti katika ngazi ya kiwanda na bandari zetu; akitoa certificate ya ubora wa mbolea na mbegu then mbegu hiyo ikagoma kuota Kwa ubora mdogo awajibishwe.

Lakini kwanini mbolea na pembejeo feki zinawafikia wakulima? Jibu ni Moja TU; ni kwasababu anayeathirika ni mkulima mdogo na siyo tajiri wala mwanasiasa.

Na hapa ndipo hoja yangu iliyo; tukiwa na wakulima wakubwa watawekeza wao wenyewe kwenye ubora wa mbegu Lakini wao pia watatuajiri sisi wadodo na hivyo tutakuwa na uhakika wa salary iwe kiangazi au masika.

Ndo maana nikasema Mhe. Bashe anaweza kuwa anawaza sawasawa na anatamani mengi ila Kwa mfumo wetu wa siasa ambao Hana uhakika wa kudumu kwenye uwaziri yeye afikiri Kuhusu sera na sheria zakumlinda mkulima huku zikiwavutia matajiri. That one will last for years, transfer na kupanga vituo vya kazi iwe kazi ya maafisa utumishi na wakurugenzi.

I'm not bulling him but I'm trying to tell him how better he can preach and convert more believers in his presence or absence.

Aanza kuunganisha wizara yake na wizara nyingine aondoke kwenye thinking za Kila idara na majukumu yake; atekeleze Kwa vitendo wish ya Katibu Mkuu Kiongozi na Mhe. Rais ya kuyavilunja vunja majukumu ya serikali Yawe yanasomana. Integration ya activities za wizara yake na wizara nyingine it's key aspect kwenye mapinduzi ya kiwanda
uko sawa kabisa,
miaka fulani ya nyuma niliwahi kuona hao wataalam wa kilimo walipomaliza chuo kikuu pale sua, walienda ifakara kwenye mashamba ya mpunga.
ikabidi waanze kufundishwa na wakulima (ambao hawajasoma) kutofautisha mpunga na majani wakati wa kufanya palizi (maana yalikua yakifanana mno), na jinsi ya kutumia dawa nk...
yaani kwa kifupi wasomi walikua watupu kabisa mbele ya wakulima
 
Nadhani wote tunashuhudia namna wabunge wanavyolinda na kupiga kelele zinapotajwa posho na maslahi Yao. Ni mashuhuda kwamba Mzee Pinda linapokuja suala la ufugaji wa nyuki yupo radhi afunge safari kwenda Kwa Mhe. Mkubwa wa nchini kulitolea ufafanuzi, tunafahamu nguvu watakayotumia akina Zitto pale utakapoporomosha soko la korosha nchini nk.

Mifono hii inatosha kusema popote ambapo mwanasiasa amewekeza kelele zinakuwa kubwa na sera za nchi zinazingatia kelele hizo. Leo Mhe. Bashe anaangaika na maafisa Ugani Jambo ambalo ni jema ila amewahi kuwaza kuwashawishi wanasiasa walime mahindi, walime alzeti, walime michikichi nk Ili wamsaidie kulinda soko?

Ni kawaida kusikia wakulima wamevuna na soko let say la mahindi nchini Zambia lipo vizuri; then unamsikia Waziri au Mkuu wa Mkoa akitamka hakuna mkulima wa Tabora, Rukwa na Katavi kuuza mahindi nje. Ukisikia kauli hii unabaini wazi kwamba hapa hakuna mwanasiasa mwenye mahindi ndani anayeathirika na katazo hili. Au kama wapo basi wanatafuta mbinu yakununua Kwa Bei ndogo wapeleke Dsm then wasafirishe Kwa njia nyingine.

Nimwombe Mhe. Bashe asiangaike kutumia gharama kubwa kuhusu maafisa Ugani , atengeneze wakulima wakubwa then wakulima wataajiri maafisa Ugani na siyo serikali. Leo ukipata mwekezaji mkubwa wa Kilimo kutoka nje usitegemee atatumia maafisa Ugani wa serikali , ataajiri watu wake Kwa qualification anazozitaka.

Mwisho; ufuguja wa kuku nchini unakua Kwa Kasi, Lakini madaktari wa kuku awatoki serikalini wanazalishwa kwenye jamii au kuajiriwa kufanya kaz Kwa utaalam walionao.

Mhe. Bashe; tatizo la Kilimo siyo wataalam,tatizo ni nani anajihusisha na Kilimo na analindwa VIPI kumjengea confidence ya Kilimo? We need political will inline with political gurus paticipation in this sector.
Hoja nzuri na muhimu, ijapokuwa kuelekea huko kunahitagi mpango wenye hatua kadhaa. Mh Bashe yuko sahii kwa kuanza na maafisa ugani kama hatua ya kuanza nayo.

Hatua ya pili ni kuboresha soko la ndani la mazao ili kushawishi hao wakulima wakubwa na wanasiasa kuingia kwenye kilimo.Huwezi kumwambia mwanasiasa kama Zitto alime mahindi huku hana uhakika wa faida. Lazima kwanza tuanze chini hao wa juu wata join the chain katikati.

Hongera kwa mawazo mbadala, Hongera sana Mh. Bashe wewe ni Waziri wa aina yako tulingoja haya kwa kipindi sana sasa tunaondoka dalili za nuru.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom