macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 21,771
- 39,555
Asante. Umeelezea vizuri sana. Lakini utawala wa sasa hawana weledi kama huu. Sana sana utasikia wamezuia ndege au bidhaa za Kenya.Hatua stahiki ni kuhakikisha kuwa mazao yetu hayana sumu. Tunatakiwa kuwashukuru wakenya maana hayo mahindi hata sisi tunauziwa. Serikali inatakiwa kuanzisha utaratibu wa ku monitor mazao yetu kabla hayajaingia kwenye masoko ya ndani na nje. Hii sio mara ya kwanza kugundua kuwa watu wako tayari kuhatarisha maisha ya wenzao kwa tamaa za faida ya haraka haraka. Kuku wanalishwa dawa za ajabu ili wawe wakubwa, pombe zinachanganywa na uchafu wa kila namna ili zivutie wateja, samaki kuvuliwa kwa sumu na baruti n.k.
Hii tabia ya kila wakati kujiona sisi ni victims inatugharimu sana.
Amandla....