Waziri: Babu lazima asajiliwe

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
216
imeandikwa na Hamis Shemdoe kutoka arusha

waziri wa afya na ustawi wa jamii mh. Dr Haji Mponda amesema serikali imesikitishwa sana na ushirikiano mdogo inaopata kutoka kwa wasadizi wa Mchungaji mstaafu wa KKKT Ambilikile Mwasapile anayetoa tiba ya magonjwa sugu huko Loliondo hasa katika kupata maelezo mbalimbali yanayotakiwa ili kukamilisha taratibu za kumsajili kama mganga wa tiba za jadi kwa mujibu wa sheria za nchi

waziri mponda aliyasema hayo muda mfupi baada ya katibu mkuu wa wizara yake Bi. Blandina Nyoni kumpa taarifa kwamba zoezi la kumsajili linakwama kutokanana wasaidizi wa babu kuonyesha ushirikiano mdogo ambapo wakati wote wamekuwa wakisema kuwa hawana muda wa kukusanya taarifa zake kwa vile wamebanwa na shughuli za kuandaa dawa na kuigawa kwa wagonjwa.

Mch. Mwasapile mwenyewe alipotafutwa kufafanua utata huo alisema kuwa yeye hawezi kusajiliwa kama mganga kwani hajui chochote katika masuala ya uganga na kwamaba anachofanya yeye sio uganga. aliongeza kuwa kama ni usajili, basi asajiliwe kama mhubiri wa injili aliye chini ya kanisa linalotambulika nchini yaani KKKT na siyo mganga kwani kazi zake ni za kichungaji na zimekwishabarikiwa na kanisa lake la KKKT ambalo limeishasajiliwa.

tangu kuibuka kwa tiba jiyo ya magonjwa sugu huko loliondo mkoani Arusha kaskazini mwa Tanzania, maelfu ya watu wamekuwa wakimiminika kutafuta tiba hiyo na kuilazimu serikali kuingilia kati kuboresha mazingira ya kutolea tiba na kuanza hatua mbalimbali za kumsajili

source: BBC Swahili - Mwanzo
 
Kazi kweli!Inawezekana babu akawa yuko sawa.Hiyo dawa anayochemsha na kuwapa wagonjwa/waumini/wateja, pengine haina tofauti sana na wanaofanya maombezi kwa kuwapa waumini olive oil wanywe ama kuwapakaza sehemu mbalimbali za miili yao?:help:
 
hii kitu ni bonge la diversion, and as fools as we are, we are falling for it!

poor tanzanians..
 
Tukiuchukulia huu kama muujiza, ni bora, manake wengi wanapona wan wengi hawaponi, mwenyewe haelewi chochote.

Kizazi chetu, bahati mbaya au nzuri hatuna uzoefu na miujiza, ni wagumu kuamini, tunataka kila kitu tueleweshwe mpaka tuelewe.

zamani walikuwa wanaita 'shingo ngumu'

Anyway, bora kanisa lifanye kazi mapema, tofauti ionekane, watake charge, kama kweli wapo. tuone mabadiliko, Kanisa la KKKT si dogo, lina uwezo mkubwa sana. Mbona halisikiki?

Mie ningedhani Waziri angeshinda pale KKKT apate majibu yote.
 
Asajiliwe leo?? Hii serikali kwa staili ya zimamoto kiboko...
 
Kazi kweli!Inawezekana babu akawa yuko sawa.Hiyo dawa anayochemsha na kuwapa wagonjwa/waumini/wateja, pengine haina tofauti sana na wanaofanya maombezi kwa kuwapa waumini olive oil wanywe ama kuwapakaza sehemu mbalimbali za miili yao?:help:

Kumbe, babu mganga wa jadi! Hii ndiyo yenyewe

Tukiuchukulia huu kama muujiza, ni bora, manake wengi wanapona wan wengi hawaponi, mwenyewe haelewi chochote.

Kizazi chetu, bahati mbaya au nzuri hatuna uzoefu na miujiza, ni wagumu kuamini, tunataka kila kitu tueleweshwe mpaka tuelewe.

zamani walikuwa wanaita 'shingo ngumu'

Anyway, bora kanisa lifanye kazi mapema, tofauti ionekane, watake charge, kama kweli wapo. tuone mabadiliko, Kanisa la KKKT si dogo, lina uwezo mkubwa sana. Mbona halisikiki?

Mie ningedhani Waziri angeshinda pale KKKT apate majibu yote.

Asajiliwe leo?? Hii serikali kwa staili ya zimamoto kiboko...

jamani hivi leo tarehe ngapi?............ teh teh tih.......................
 
Back
Top Bottom