Waziri azindua ndege ya Fastjet

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,577
6,582
Imeandikwa na Nuzulack Dausen | Gazeti la Mwananchi | Nov 28, 2012

NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba ameagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuandaa mazingira mazuri na miundombinu katika Viwanja vya Mwanza na Kilimanjaro kukabiliana na ongezeko la abiria wanaotarajia kuvitumia.

Akizindua safari za ndege za Kampuni ya Fastjet Dar es Salaam jana, Tizeba alisema kuanzishwa kwa safari za ndege za bei rahisi kwa mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza kunatoa changamoto kwa Serikali kuboresha miundombinu kukidhi mahitaji ya ongezeko la wasafiri.

“Kuanzishwa kwa safari za ndege za bei rahisi ya Sh32,000 na Kampuni ya Fastjet kunatarajiwa kuvutia abiria wengi zaidi, hali ambayo viwanja vingi nchini vikiwamo vya Mwanza na Kilimanjaro haviwezi kutimiza mahitaji,” alisema Tizeba.

Tizeba alisema hadi sasa Serikali inaendelea kurekebisha baadhi ya viwanja vya ndege nchini, vikiwamo vya Kigoma, Tabora na Mafia huku Kiwanja cha Mwanza kikiendelea kurekebishwa sehemu ya abiria na barabara za ndege.

“TAA ihakikishe hakuna abiria atakayeshindwa kusafiri kwa sababu ya wingi wa watu na ukosefu wa miundombinu kwa kiwanja chochote cha ndege nchini,” aliagiza Tizeba.
 
Kwa hiyo hawa jamaa wameanza kuruka jana? Hebu tupe habari kamili.

Tiba
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom