Waziri azifunga leseni za Madereva wa Mabasi 10 kwa kuendesha speed 125 kwa saa. Aagiza washtakiwe

Kwenye mabasi wanajitia wanatupenda saana, ila internet wanakaza.. Hii nchi nchii
 
Speed 120 ni kawaida sana, mbona wao gari zao zinaenda mpk speed 220 au wao hawajali uhai wao wanatujali sana sisi wananchi? gari za Serikali mara kwa mara zinapata ajali au huwa husikii?
Kama mtu mmoja au wawili wanasafiri kwa mwendo huo kwa ridhaa yao wenyewe ni shauri yao ingawa bado ni kosa. Lakini huwezi kucheza na mamia ya maisha ya watu kwenye basi.
 
Mbona unachanga madesa? Kuendesha 125km/h siyo tatizo wakati hapo hapo unahoji kama barabara zetu zinahimili? Wewe unaona zinahimili?
Ndugu, hakuna madesa wala nini, barabara zetu Kwa speed hiyo ni kujitafutia kifo tu...labda tumpate magufuli mwingine aje ajenge highways na motorways . Hilo likifanyika na tukiwa tuko hai, ndo utanielewa...
La pili ni kwamba, barabara pia gari zetu hazina ubora na uimara unaotakiwa kimataifa... suala la madreva kukimbia 125 ni suala la udhibiti na elimu tu sio la kuwanyanganya leseni...sasa je wanadhibitiwa Kwa namna gani? Ni swali linalohitaji mjadala mpana...kuna huko kuwekewa speed camera- sio vitochi vya polisi; kuna speed radars; kuna average speed monitors - mfano inajulikana toka dar mpaka Moro ni km x na wakiweka hata 70km watajua tu Kwamba ulikuwa unaendesha Kwa Kasi gani- muhimu tu ni kuwa na automatic monitors za computers zinozoweza fanya kazi hiyo... ni mengi Kwa kweli yanayoweza fanyika kupunguza ajali...
 
Serikali ndiyo yenye jukumu la kusimamia hayo! Yapo mambo viongozi wanafanya vyema kama hili hongera sana kwa Waziri!
Bora kuchelewa lakini abiria wafike salama
Kwa hili hongera kwa waziri. Wanaambiwa watembee 80 km kwa saa lakini hawasikii
 
Napongeza uamuzi huu kupunguza ajali za mwendokasi .....hongera ingawa sidhani waziri atakuwa busy kila mwezi kusema hizo kesi za Wenda mbio mkuu u salama barabarani atosha
 
Afanye kazi kwa kufuatana na Sheria zilizopo asiweke Sheria zake binafsi... ndio kuinua mabega huku... sijawahi sikia Waziri kazi yake kufungia leseni madereva... na Madereva wa kwenye Misafara au wale wa macoster yanayobeba wafanyakazi wa bunge au mabalozi n.k ndio kazi yake aache uonevu na aache sheria zifanye kazi yake mahakama imeingiliwa na mhimili mwingine
 
Hivi mnataka muongozwe vp?
Mabasi yakikimbia hadi kuua mnalalamika

Madereva wasipochukuliwa hatua mnalalamika

Wakichukuliwa hatua mnalalamika

Ova
Hatua inachukuliwa na Mahakama au waziri...
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amefunga leseni za madereva 10 wa mabasi yanayokwenda mikoani wakidaiwa kuvunja sheria za usalama barabarani.

Simbachawene alifunga leseni hizo kwa miezi mitatu kwa kuwa madareva hao walidaiwa kuendesha mabasi kwa mwendokasi wa kilometa 125 kwa saa.

Aliwaeleza waandishi wa habari jana jijini Dodoma kuwa hivi karibuni baadhi ya madereva walianzisha tabia ya kukiuka sheria za barabarani na hivyo kuhatarisha maisha ya abiria wanaotumia vyombo hivyo.

Simbachawene alisema ameliagiza Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, liwashitaki mahakamani madereva hao 10 na agizo hilo litekelezwe ndani ya siku 14 tangu.

Ippmedia
Kampuni zilizofungiwa ni zipi?
 
Tanzania ina walalamikaji wengi sana
Haki isipotendeka lazima minong'ono... kazi ya mahakama anafanya Waziri.. sheria zetu zinaonesha adhabu hiyo ni fine elfu 30 + Sumatra kama 250,000 and akiwa hakomi nadhani ndio mahakamani.. sasa Waziri kuinua mabega kwa raisi anawafungia yeye leseni zilizo nje ya mamlaka yake
 
Kaanza kugusa kazi zake za kitambo akiwa kondakta gari za shemeji yake Urafiki bus,anagusa maslahi ya watu Sasa familia zife njaa
 
Back
Top Bottom