Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema serikali itazitoza faini kampuni zote za simu za mkononi ambazo zitashindwa kupeleka mawasiliano yake vijijini kama ambavyo masharti ya mkataba walioingia na serikali wa kufikisha huduma za mawasiliano vijijini chini ya mfuko wa mawasiliano kwa wote yanavyowataka.
Alisema hatua hiyo itachukuliwa dhidi ya kampuni hizo kwakuwa hali hiyo ikiachwa, itaendelea kuchelewesha maendeleo kwa wananchi.
Kauli ya profesa Mbarawa imekuja juzi wakati akizungumza na viongozi wa idara mbalimbali za serikali pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi CCM) na serikali mkoani iringa.
Prof. Mbarawa ametaja kampuni zilizo kwenye hatari ya kukumbana na adhabu hiyo kuwa ni Hallotel, Tigo, Vodacom, Airtel pamoja na kampuni ya serikali ya TTCL.
"Narudia tena--hii kuanzia ni tarehe Mosi mwezi huu, yale ambayo yameshindwa kutekeleza, hata kama ni kampuni yetu ya serikali ya TTCL, lazima tuwatoze faini kwa sababu ni makubalino na tuliweka kwenye mkataba kuwa mkishindwa kujenga kwa wakati lazima tuwatoze faini. Nimemuita mtaalamu wa kampuni ya Halotel hapa kwa sababu serikali iliwekeana mkataba na kampuni hiyo,"alisema Mbarawa.
Source: Nipashe