KERO Waziri Aweso, Jiji la Dar Sasa wanakunywa na kuoga maji ya kwenye mifereji. DAWASA pakavu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,614
10,166
Hii ni hakika. Tunetoka kwenye mvua kubwa, mifereji ya Jiji la Dar na vijito bado vinatirisha maji. Wananchi wachota hayo maji kwa matumizi Yao ya kila siku.

Bila haya maji, Jiji la Dar liko kwenye hatari ya kindupindu.

Aweso changamka kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.

Waziri wa afya pia changamka kabla hujaanza kuhudumia kipindupindu.

Ni hayo tu.

Pia soma
 
Huduma ya maji ni changamoto maeneo mengi sana Dar sijui shida ni nini hawasemi Aweso hatembei Dar kuomgea na wananchi kupata ukweli.
 
Karne ya 21, miaka mingapi sijui ya Uhuru, yaani TUMESHINDWA KABISA KUONDO SHIDA YA MAJI DAR ES SALAAM.
Inasikitisha sana mkuu, tena kwa Dar kuna maji tele ya bahari hindi. Ingawa ni gharama lakini desalination ingeyafanya hayo maji kuwa safi kwa matumizi ya binadamu na kuondoa kabisa kero ya kudumu ya maji. Tunapiga porojo na kutokuwa na vipaumbele sahihi kwa zaidi ya miak 60 sasa. Yaani huko kanda ya ziwa, hata hapo manispaaa ya Musoma tu, imezungukwa na Ziwa Victoria lakini maji si ya uhakika kabisa.
 
Hii nchi inahitaji Magufuli mwingine Tena.
 
Huduma ya maji ni changamoto maeneo mengi sana Dar sijui shida ni nini hawasemi Aweso hatembei Dar kuomgea na wananchi kupata ukweli.
Aweso ameshachoka na hii kazi. Abadilishwe
 
Back
Top Bottom