Waziri Aweso fanya maamuzi haya ili ubaki kwa kumbukumbu nzuri

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,189
Pamoja na baadhi ya Watanzania kuona kuna madudu yanafanyika pmus kuwanyonya kutokana na baadhi ya viongozi kuingia kwenye siasa kwa mgongo wa wazee wao, bado mnaweza kuwaachia watanzania legacy ya kuwakumbuka hata msipokuwepo.

MAJI; Nchi yetu imekuwa na janga la uhaba wa maji kwa miongo kadhaa kisa ukame, ilihali tumezungukwa na maziwa na mito mingi kila mkoa.

Ukiangalia baadhi ya mito mingi nchini inatiririsha maji na kuishia baharini, sehemu ambayo hakuna ulazima wowote maji kuingia baharini.

Tuchukulie mto wami au pangani kule kwenu, badala ya hayo maji kuendelea kuishia baharini inawezekana kujengwa bwawa kubwa (mwisho kabla ya eneo la bahari) hayo maji badala ya kuingia baharini yakaingia kwenye bwawa hilo kisha yanavunwa kuelekea kwenye matenki ya maji ili yasambazwe mkoa husika.

Haiwezekani nchi kama Misri hawana chanzo chochote cha maji ila wanategemea mto nile ambao maji yake yanatoka hapa kwetu na katika kufuatilia, huko misri hawwjui kitu kinaitwa mgao wa maji, ila sisi kila siku ni siasa hata kwenye mambo ya msingi.
 
Wenye maji wakibeba maji

FEfktyhXEAQ6oCZ.jpeg
 
Mvua zinaponyesha maji hutiririka kufuata mkondo na kugeuza barabara zetu kuwa mito.

Nyumba zote za bati zikivuna maji na kuingizwa kwenye mtandao wa maji mifano DAWASA, yakavunwa na kuhifadhiwa kwenye bwawa maalumu, si yangetufaa wakati wa shida ya maji kama sasa?

Tusiwalaumu wafugaji na ng'ombe wao kwa mapungufu yetu katika kutumia akili, hivi kweli kuna mtoto anaweza kuamini eti ng'ombe wengi wamekunywa maji mto Ruvu hadi yamepungua?.:oops:
 
Pamoja na baadhi ya Watanzania kukuona unafanya madudu na upo kuwanyonya kutokana na kuingia kwenye siasa kwa mgongo wa mzee wako, bado unaweza kuwaachia watanzania legacy ya kukukumbuka hata usipokuwepo.

MAJI; Nchi yetu imekuwa na janga la uhaba wa maji kwa miongo kadhaa kisa ukame, ilihali tumezungukwa na maziwa na mito mingi kila mkoa.

Ukiangalia baadhi ya mito mingi nchini inatiririsha maji na kuishia baharini, sehemu ambayo hakuna ulazima wowote maji kuingia baharini.

Tuchukulie mto wami au pangani kule kwenu, badala ya hayo maji kuendelea kuishia baharini inawezekana kujengwa bwawa kubwa (mwisho kabla ya eneo la bahari) hayo maji badala ya kuingia baharini yakaingia kwenye bwawa hilo kisha yanavunwa kuelekea kwenye matenki ya maji ili yasambazwe mkoa husika.

Haiwezekani nchi kama Misri hawana chanzo chochote cha maji ila wanategemea mto nile ambao maji yake yanatoka hapa kwetu na katika kufuatilia, huko misri hawwjui kitu kinaitwa mgao wa maji, ila sisi kila siku ni siasa hata kwenye mambo ya msingi.
Wazo zuri Sana, lakini bado utaambiwa kwenye hiyo mito na bwawa kuna water fluctuation kutokana na ukame kwahiyo mgao daily kama kawa. Ila hii sio wizara ya Makamba.
 
Back
Top Bottom