Waziri Aweso: Changamoto za bili bambikizi za maji ifike Mwisho

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Waziri Aweso ametumia wasaa wa ziara yake Mkoani Mwanza kwenye Mradi wa Maji Buswelo kuwaelekeza Meneja Masoko (Commercial Manager) wote wa Mamlaka za Majisafi kusimamia kikamilifu zoezi la usomaji mita za maji ziwe halisia ili kuepuka kuwabambikia wananchi bill za maji.

Mh. Aweso amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji kuwasimamia Meneja Masoko wa Mamlaka za Maji wasiwape wasoma mita za maji malengo makubwa ya makusanyo (target) yasiyo halisia ambayo hayatekelezeki na yanawaumiza wananchi na kusababisha malalamiko akisisitiza kero hii ifike mwisho.
 
Back
Top Bottom