Waziri Aweso apiga marufuku EWURA kupandisha ankara za maji

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,763
Waziri wa maji mh Aweso ameipiga marufuku Ewura kupandisha ankara za maji kadhalika mamlaka zote za maji nchini zimeambiwa zisithubutu kuwapandishia wananchi bei za maji.

Waziri Aweso amesema hayo kwenye kikao cha watendaji wa wizara ya maji na taasisi zake.

Maendeleo hayana vyama!

---
Waziri wa Maji, Juma Aweso (pichani) amezuia kupandisha ankara za maji kuanzia mwishoni mwa mwezi huu mpaka itakapoelekezwa vinginevyo

Aweso aliyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kuelezea kutoridhishwa na utendaji kazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (EWURA) katika sekta ya maji kwenye kikao kazi cha Wizara ya Maji na taasisi zake.

Alisema Ewura imezitaka baadhi ya mamlaka za maji kupandisha bei ya maji kuanzia mwisho wa mwezi huu na kuwa utaratibu huo ameuzuia kwa muda mpaka timu ya wataalamu wa wizara itakapoona kama kuna haja ya kupandisha bei.

Alisema kazi ya Ewura si kupitisha ankara za maji, ila kudhibiti na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kwa bei mwafaka na bila kubambikiziwa ankara.

Aweso alikemea tabia ya watendaji wa mamlaka za maji kupambikiza bili za maji kwa wateja na kutaka usomaji wa bili ushirikishe wananchi.

“Ni haki ya watu kupata huduma ya maji, na mwananchi analipa bili za maji anayotumia lakini bili hizi zisiwe bambikizi.

Niwe mkweli Ewura kwa upande wa maji haifanyi vizuri kabisa, kazi yao pia kudhibiti hata hizi bei za maji za mifukoni,” alisema waziri huyo. Alisema pia kuna baadhi ya mamlaka ambazo zimekuwa zikitoa bei ya maji bila kuidhinishwa na Ewura.

“Mtalaamu wa kusoma bili kwenye mita ya mteja, bila kumshirikisha mtumiaji, ni wakurugenzi tuangalie kurejesha utaratibu wa awali wa mtaalamu anaposoma bili anasaini na mteja anasaini na ushirikishwaji huu utaondoa manung'uniko yasiyo ya lazima,” alisema Aweso.

Aliwaagiza Ewura kuwajengea uwezo wakurugenzi na kutoa elimu kwa wananchi wafahamu ni wapi kwa kwenda wanapokuwa na malalamiko ikiwa ni pamoja na kutokubaliana na bili zinazotolewa.

Aidha, amewataka wahandisi, wakuu wa mamlaka za maji nchi na watumishi wote katika sekta ya maji kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuwa wabunifu na kuwa hatawafumbia macho watumishi wazembe.

Aweso pia amewataka viongozi wa mamlaka za maji kuhakikisha wanarejesha maji ndani ya saa 24 kama sheria zinavyotaka kwa wale ambao wamekatiwa maji na kutaka kurejeshewa.

“Wakurugenzi mlisimamie hili, tusiwaadhibu wananchi pasipo stahili, mteja akitumia maji wana wajibu wakulipa, na pindi mnapotakiwa kurejesha maji kwa mliomkatia ni ndani ya saa 24 na isiwe zaidi ya siku 10 kama mnavyofanya sasa,” alisema waziri huyo.

Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi alisema katika ziara kwenye mikoa mbalimbali amebaini baadhi ya miradi imepitwa na wakati na kuwa chakavu na kutaka wataalamu wafanye tathmini ili kufanya maboresho.

Pia alisema kumekuwa na changamoto ya uendeshaji miradi ya maji kwa jumuiya za watumiaji maji na kusisitiza haja ya kuwa na wataalamu wa maji katika kamati hizo ili miradi hiyo ijiendeshe.
 
Hongera waziri, lipo tatizo kubwa bili za maji kuwa kubwa, na kupandishwa mara kwa mara ili hali miradi na maboresho hugaramiwa na serikali.Inafika pahala ina kuwa bidhaa ya biashara na sio huduma muhimu.
 
Iko chini ya wizara ya maji.

Lakini sheria ya kuanzishwa kwa ewura, au mamlaka nyingine yoyote ya udhibiti, inaelekeza kwamba chombo hicho kinapaswa kuwa huru ktk maamuzi yake ili kuwalinda watumia huduma na watoa huduma.
Kimeshindwa kutekeleza majukumu basi kivunjiliwe mbali.
 
..sheria haijampa waziri wa maji mamlaka ya kuweka bei elekezi.

..badala yake sheria imeipa jukumu hilo ewura na hawapaswi kuingiliwa ktk kazi zao.
Kwenye sheria kuna kipengele kinawapa mamlaka mawaziri wa wizara husika kutengemeza regulation au miongozo kwa inavyoona au itakavyoona inafaa kwaio kwenye sheria yako ya ewura hicho kipengele kipo pia
 
Iiko chini ya wizara ya maji.

Lakini sheria ya kuanzishwa kwa ewura, au mamlaka nyingine yoyote ya udhibiti, inaelekeza kwamba chombo hicho kinapaswa kuwa huru ktk maamuzi yake ili kuwalinda watumia huduma na watoa huduma.
Hicho chombo bila kuwa na mkuu zaidi yake ni tatizo so waziri yupo sawa bin sawia, kama una bomba la maji ndipo utajua hii kero kama umepanga huwezi kujua hii.
 
Hicho chombo bila kuwa na mkuu zaidi yake ni tatizo so waziri yupo sawa bin sawia, kama una bomba la maji ndipo utajua hii kero kama umepanga huwezi kujua hii.

..lengo la mamlaka za udhibiti ni kuwalinda watumia huduma na watoa huduma.

..inawezekana kuna watendaji wabovu, lakini madhumuni ya kuanzishwa kwa mamlaka ni hiyo niliyoieleza hapo juu.

..again, waziri hatakiwi aingilie mamlaka husika na kuamrisha bei elekezi.
 
Kwenye sheria kuna kipengele kinawapa mamlaka mawaziri wa wizara husika kutengemeza regulation au miongozo kwa inavyoona au itakavyoona inafaa kwaio kwenye sheria yako ya ewura hicho kipengele kipo pia
Ategeneze si kupayuka payuka
 
..lengo la mamlaka za udhibiti ni kuwalinda watumia huduma na watoa huduma.

..inawezekana kuna watendaji wabovu, lakini madhumuni ya kuanzishwa kwa mamlaka ni hiyo niliyoieleza hapo juu.

..again, waziri hatakiwi aingilie mamlaka husika na kuamrisha bei elekezi.
Kwani wewe ni raia wa nchi gani mpaka hujui kila mamlaka inakuwa chini ya mamlaka nyingine?
 
Back
Top Bottom