Waziri Aweso aibua shangwe wananchi pembezoni vyanzo vya maji Mbinga; aagiza usanifu wa mradi kuanza

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
AWESO AIBUA SHANGWE WANANCHI PEMBEZONI VYANZO VYA MAJI MBINGA; AAGIZA USANIFU WA MRADI KUANZA

MBINGA-RUVUMA

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso amekagua na kuzindua shughuli za uhifadhi wa vyanzo cha maji vya Lupembe A, B, C, na D ambavyo ni tegemeo kwa usambazaji maji Safi kwa mji wa Mbinga mkoani Ruvuma Wilaya ya mbinga na kisha kuongea na wananchi ambao ni wahifadhi wa chanzo hicho katika kijiji cha Tukuzi.

Katika hatua nyingine Waziri Aweso ameagiza usanifu wa mradi wa maji ufanyike mara moja kwa wananchi hao ambao ni wahifadhi katika kijiji cha tukuzi na baadhi ya wananchi wa Mbinga mji waishio karibu na vyanzo vya Lupembe wilayani Mbinga akiacha shangwe na hamasa kubwa kwa wananchi waliofika kwenye Mkutano.

Mwisho amezitaka mamlaka za mabonde nchi nzima kuzingatia kuwa wananchi waishio pembezoni mwa vyanzo vya Maji wajengewe Miundombinu ya upatikanaji Maji ili kuongeza hamasa ya uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya Maji.
 

Attachments

  • VID-20221006-WA0046.mp4
    17.2 MB
Back
Top Bottom