Waziri atoboa: Matajiri wanaweka viongozi madarakani

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,136
Waziri atoboa: Matajiri wanaweka viongozi madarakani
Thursday, 01 October 2009 16:10
Asema lengo ni kutaka kulinda maslahi yao
Adai huo ni udhaifu, dawa yake inapikwa

Prosper Mosha na Neema Kalaliche

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Bw. Philip Marmo amekiri kuwapo kwa kasoro za kiuongozi katika Serikali ya Tanzania ikiwamo ile ya matajiri kuwa na msukumo mkubwa katika kuweka viongozi madarakani ili kulinda maslahi binafsi.

Bw. Marmo aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na Majira ili kutoa maoni yake juu ya kauli ya viongozi wa dini walioitaka kuhakikisha matajiri hawawachagulii wananchi viongozi.

Alisema pamoja na kwamba sio rahisi kuwabaini kwa mara moja watu hao, ila anafurahi kusikia wadau wa madhehebu ya kidini walivyoamua kulivalia njuga kwa lengo la kulinusuru Taifa.

"Hii inaashiria kuwa tumefikia mahala pazuri katika kupambana na watu wa aina hiyo," alisema.

Kauli hiyo ya Bw. Marmo inakuja siku moja baada ya viongozi wa juu wa madhehebu ya dini nchini kukemea tabia ya matajiri wanaotumia mali zao vibaya kwa kuweka viongozi watakaolinda maslahi yao.

Viongozi waliofikia azimio hilo katika mkutano wa pamoja juzi ni wawakilishi wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Ofisi ya Mufti Zanzibar na Ofisi ya Kadhi Zanzibar.

Wawakilishi madhehebu hayo ni Rais wa TEC, Askofu Yudda Thaddaeus Ruwa'Ichi, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Harith Khelef, Mwakilishi wa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Kadhi Said Mahmud, Mwenyekiti wa CCT, Askofu Peter Kitula na Mwakilishi wa Mufti Mkuu, Sheikh Taufiq Ibrahim.

Bw. Marmo alisema kuwa miongoni mwa njia zitakazotumika kuwabaini watu wa aina hiyo ni pamoja kutungwa kwa Sheria ya Kusimamia Matumizi ya Fedha wakati wa uchaguzi kuanzia kwenye kura za maoni, ambayo mchakato wake umeanza.

"Sio rahisi kwa sasa kugundua ni kwa kiasi gani watu wanatumia fedha vibaya wakati wa uchaguzi na namna ya kuwabana na hii ni kutokana na kwamba hakuna sheria inayoainisha mambo haya," alisema.

Alisema kuwa Muswada wa Sheria hiyo unatarajiwa kuchapishwa wiki ijayo kwenye Gazeti la Serikali kupitia kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ili watu wausome na kuupitia huku ukisubiri kupelekwa kusomwa kwa mara ya kwanza bungeni katika mkutano ujao kuanzia Oktoba 27, mwaka huu.

Bw. Marmo alisema kuwa sheria hiyo itakapokamilika hawezi kujihakikishia kwa asilimia mia kuwa itatekelezwa na kufuatwa katika nyakati za uchaguzi, lakini anaamini kuwa itawabana na kuwawajibisha wahusika kama zilivyo sheria nyingine.

Alisema sheria hiyo mpya itawabana wagombea wa kila chama cha siasa kuonesha viwango halali vya fedha watakazotumia katika kipindi chote cha uchaguzi, hivyo kuepusha mianya ya matajiri kuendelea kuivuruga serikali katika kuwania madaraka.
 
Hamna alichotoboa huyo Marmo!Hili ni nani asilijua kuwa viongozi wa hii nchi wanawekwa na matajiri??
This is old xul and everybody knows.kila mtu anaongea ili mradi aonekane ameongea na kusema chochote.tatizo wote ni pumba na kelele coz hamna kinachotekelezwa.
Empty tins make loud noises.
 
Marmo wacha kulalama kama mtoto mdogo,unatakakiwa kutuambia wewe kama waziri umefanya nini kuondoa utata wa katiba.
 
Hiyo siyo siri mbona! Yeye atuambie kama anatumia raslimali zake pekee wakati akigombea uchaguzi bila fadhila za matajiri hao anaowasema. Hizi ndizo athari za utandawizi na soko huria. Wenye nazo wanaweza kununua chochote, utu, haki n.k
 
Kazi kweli kweli.Kuna kitu kinapikwa sijui ni nini maana naona waliokuwa nyuma wameanza kwenda front.
 
Back
Top Bottom