nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Home
Habari za Kitaifa
Personal Tech
Waziri atoboa alivyobanwa na Nyerere
TUESDAY, 11 OCTOBER 2011 11:49 NEWSROOM
MWANASIASA mkongwe, Paul Kimiti, amesema kuporomoka kwa uadilifu wa viongozi na kujilimbikizia mali, kumetokana na baadhi yao kutafsiri vibaya kufutwa kwa Azimio la Arusha. Amesema wakati wa utawala wa hayati Mwalimu Julius Nyerere, viongozi walikuwa na hofu ya kufanya hivyo kutokana na kuwepo vyombo vya ufuatiliaji.
Hata hivyo, alipongeza hatua ya Rais Jakaya Kikwete ya kuanza kuwachunguza viongozi wa aina hiyo. "Rais ameliona hili na aliwahi kusema viongozi sasa tuanze kuchunguzana," alisema.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika yanayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, jana, Kimiti alisema pamoja na serikali kuchelewa ni vizuri utekelezaji unafanywa sasa.
"Wakati wa Mwalimu kulikuwa na vyombo vinafuatilia utendaji kazi wa viongozi... nilikuwa najenga nyumba Dodoma mwaka 1983, Mwalimu aliniita na kuniuliza, Paul unajenga nyumba, umepata wapi hela?†alisema.
Alisema baada ya kufanya uchunguzi iligundulika alikopa katika iliyokuwa Benki ya Nyumba, lakini hivi sasa watu wamekuwa wakifanya mambo holela.
"Hatua hiyo ilimfanya kiongozi awe mwoga, ndiyo maana viongozi wakati ule wa
miaka ya sitini utakuta wote hali zetu ni za kubabaisha... lakini kama hakuna utaratibu kila mtu anafanya anavyotaka na wengine kutumia majina ya ajabu," alisema.
Kimiti aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu katika awamu mbili tofauti na mkuu wa mkoa kwa miaka mingi, alisema Azimio la Arusha lilifutwa ili kutoa nafasi ya watu kutumia pesa zao kwa shughuli za maendeleo.
Alisema mabadiliko ya sheria na utaratibu ndiyo yameifikisha serikali ilipo, kwa baadhi ya viongozi wake kutokuwa waadilifu.
Katika hatua nyingine, aliwataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kumsaidia kiongozi huyo katika utekelezaji wa majukumu ya serikali na kulinda heshima ya ofisi hiyo.
Alisema tangu uhuru Desemba 9, 1961 serikali imepiga hatua katika nyanja nyingi, lakini kwa bahati mbaya vijana wengi hawalitambui hilo.
Kwa mujibu wa Kimiti, kumbukumbu zinapaswa kuhifadhiwa ili watu wa mijini na vijijini wapate taarifa sahihi kuhusu mafanikio ya uhuru.
Kimiti alisema wanasiasa wa vyama vya upinzani wamekuwa wakipinga kuwepo kwa mafanikio bila ya kuwa na takwimu.
"Kazi yao siku zote ni kupinga, hakuna asiyeshangaa, ukweli ni kwamba mafanikio yapo katika sekta zote na takwimu zinaonyesha hilo," alisema.
Aliiomba serikali kusimamia ajira za watu katika fani mbalimbali ili kujenga wafanyakazi hodari.
"Siku hizi mtu anaajiriwa tu kwa vile kakosa kazi, hilo liishe badala yake watu waende shule na kufanya kazi kwa vitendo hasa vijijini," alisema.
Alitoa mfano alipoajiriwa alikaa miaka sita vijijini na kusomea kilimo, hivyo alitoa ushauri kuwa ifike mahali serikali ianze kuchagua ili kupata watumishi wenye ujuzi stahili.
Maadhimisho hayo yanaendelea leo ambapo Waziri Mkuu wa zamani, Joseph Warioba, atatembelea mabanda ya maonyesho.