Waziri atoboa alivyobanwa na Nyerere; sio Kiketwe na mawaziri wake

nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
87
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 87 145
Home
Habari za Kitaifa
Personal Tech
Waziri atoboa alivyobanwa na Nyerere
TUESDAY, 11 OCTOBER 2011 11:49 NEWSROOM

MWANASIASA mkongwe, Paul Kimiti, amesema kuporomoka kwa uadilifu wa viongozi na kujilimbikizia mali, kumetokana na baadhi yao kutafsiri vibaya kufutwa kwa Azimio la Arusha. Amesema wakati wa utawala wa hayati Mwalimu Julius Nyerere, viongozi walikuwa na hofu ya kufanya hivyo kutokana na kuwepo vyombo vya ufuatiliaji.

Hata hivyo, alipongeza hatua ya Rais Jakaya Kikwete ya kuanza kuwachunguza viongozi wa aina hiyo. "Rais ameliona hili na aliwahi kusema viongozi sasa tuanze kuchunguzana," alisema.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika yanayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, jana, Kimiti alisema pamoja na serikali kuchelewa ni vizuri utekelezaji unafanywa sasa.

"Wakati wa Mwalimu kulikuwa na vyombo vinafuatilia utendaji kazi wa viongozi... nilikuwa najenga nyumba Dodoma mwaka 1983, Mwalimu aliniita na kuniuliza, Paul unajenga nyumba, umepata wapi hela?” alisema.

Alisema baada ya kufanya uchunguzi iligundulika alikopa katika iliyokuwa Benki ya Nyumba, lakini hivi sasa watu wamekuwa wakifanya mambo holela.
"Hatua hiyo ilimfanya kiongozi awe mwoga, ndiyo maana viongozi wakati ule wa

miaka ya sitini utakuta wote hali zetu ni za kubabaisha... lakini kama hakuna utaratibu kila mtu anafanya anavyotaka na wengine kutumia majina ya ajabu," alisema.

Kimiti aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu katika awamu mbili tofauti na mkuu wa mkoa kwa miaka mingi, alisema Azimio la Arusha lilifutwa ili kutoa nafasi ya watu kutumia pesa zao kwa shughuli za maendeleo.

Alisema mabadiliko ya sheria na utaratibu ndiyo yameifikisha serikali ilipo, kwa baadhi ya viongozi wake kutokuwa waadilifu.

Katika hatua nyingine, aliwataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kumsaidia kiongozi huyo katika utekelezaji wa majukumu ya serikali na kulinda heshima ya ofisi hiyo.

Alisema tangu uhuru Desemba 9, 1961 serikali imepiga hatua katika nyanja nyingi, lakini kwa bahati mbaya vijana wengi hawalitambui hilo.

Kwa mujibu wa Kimiti, kumbukumbu zinapaswa kuhifadhiwa ili watu wa mijini na vijijini wapate taarifa sahihi kuhusu mafanikio ya uhuru.

Kimiti alisema wanasiasa wa vyama vya upinzani wamekuwa wakipinga kuwepo kwa mafanikio bila ya kuwa na takwimu.

"Kazi yao siku zote ni kupinga, hakuna asiyeshangaa, ukweli ni kwamba mafanikio yapo katika sekta zote na takwimu zinaonyesha hilo," alisema.

Aliiomba serikali kusimamia ajira za watu katika fani mbalimbali ili kujenga wafanyakazi hodari.

"Siku hizi mtu anaajiriwa tu kwa vile kakosa kazi, hilo liishe badala yake watu waende shule na kufanya kazi kwa vitendo hasa vijijini," alisema.

Alitoa mfano alipoajiriwa alikaa miaka sita vijijini na kusomea kilimo, hivyo alitoa ushauri kuwa ifike mahali serikali ianze kuchagua ili kupata watumishi wenye ujuzi stahili.

Maadhimisho hayo yanaendelea leo ambapo Waziri Mkuu wa zamani, Joseph Warioba, atatembelea mabanda ya maonyesho.

P

politiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2010
Messages
2,374
Likes
190
Points
160
P

politiki

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2010
2,374 190 160

huyu mzee kimiti is so naive na pia mnafiki mkubwa lini kikwete alianza kuwachunguza viongozi wake wenye mali nyingi ambao hawana maelezo walikozipata sana sana amekuwa akiwatetea mafisadi kila kukicha kama akina jairo, chenge, rostam na lowassa sasa anachokifanya Kikwete actually ni kuzuia wezi, wala rushwa na mafisadi wakubwa nchi hii wasichunguzwe kwa mujibu wa mkurugezi wa Takukuru Bw.Hosea atakwambia ktk private conversion alizozifanya na wamarekani.
 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
87
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 87 145
Wakati wa Nyerere kama shida kila mtu alkikuwa ananayo na kama ni Elimu; ilikuwa inatolewa bora sio mombo mbovu na chafu na sasa hivi Rais anajivunia kusafirisha wanae nje ya Nchi; Mawaziri kama lau Masha South Africa n.k na hakuna hata mmoja wa kuwauliza kweli wanapata wapi hizo pesa na sio kuwa wana watoto wanne wanne wana zaiti ya sita au kumi

Tatizo ni NCHI YETU na DOLA ZETU zingesaidia kuweka Umeme...
 
Tekelinalokujia

Tekelinalokujia

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
353
Likes
1
Points
35
Tekelinalokujia

Tekelinalokujia

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
353 1 35
Hawa wazee nikiwasikiliza hua nachoka kabisa, wanatuambia habari za takwimu wakati maisha ninayoishi nayaona live magumu afadhali ya juzi na kesho sijui itakuaje, leo wanasema eti tuangalie takwimu, nakumbuka wakati wa Mkapa nchi ilikua inasifiwa eti sababu tumepunguza madeni ya nje lakini huku ndani ya nchi tulikua tunaambiwa tufunge mikanda, sasa hii habari ya takwimu inanisaidia nini kama maisha yangu hayapati unafuu? zamani kwenye vyuo vya ufundi (VETA) kulikua na system ya kuandaa mipango ya ajira kwa wahitimu wa fani mbalimbali kwenda kwenye makampuni yaliohusika na fani za wahitimu ila section hiyo ikaja ikafa na sasa wahitimu wakimaliza wanaambiwa wajiajiri ambapo ni jambo zuri zaidi ila hayo mazingira ya kujiajiri yakwapi? mtu unamaliza fani ya ufundi wa magari ukiingia mtaani unakutana na gereji kibao chini ya miti pembeni mwa barabara na mafundi waliojaa hapo ni wale wa uzoefu, alianza kumsaidia fundi na baadae yeye anakua fundi na kuanza kumfundisha mwenzake, sasa security ya kujiajiri kwa huyu mhitimu iko wapi? kilakitu kiko kiholela huwezi kupanga mkakati ukitegemea system kwenye mambo mengi tuu, tunabaki kufanya kazi kwa kuviziana na kuigana alafu hawa wazee wanasema eti wapinzani kazi yao ni kupinga tuu, sasa wanataka wote tukae upande mmoja tusema sawa kwa kilakitu wakati hali yenyewe ndio hii? Phew!!!!! Kweli nachoka sijui lini tutaweza kuangalia Tanzania kama Tanzania na sii kivyama.
 
DSN

DSN

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Messages
2,791
Likes
129
Points
160
DSN

DSN

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2011
2,791 129 160
Inasemekana enzi hizo wakati mwingine mawaziri wakiwa na tuhuma akiitwa ikulu anabanwa mpaka kiwango cha kula pingu na kuambiwa apelekwe keko.Inasemekana jasho lilikuwa linawatililika wakisikia wanaitwa ikulu.Manake walikuwa hawajui ukiitwa ikulu unaitiwa nini?Waweza kuingia getini ukifika uko ndani kustaajabu unaweza kukuta unaitwa kupewa pongezi kwa kazi nzuri a kutoa ushauri kwa Mwalimu au kupokea kibano cha kiutu uzima.

Manake walikuwa wanajua kama unaitwa ikulu si kwa nia ya uteuzi kwa kuwa uteuzi wa Mwalimu mwingi ulikuwa ni surprise walikuwa wanajua kupitia Radio Tanzania Dar es Salaam.Kwa hiyo ni hakika Mwalimu alikuwa anagawa kibano kwa wale wote waliokuwa na tuhuma za kiajabu ajabu kwenye utawala wake.Ndio maana Ikulu ilionekana kuwa ni sehemu takatifu.
 
M

Mbopo

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2008
Messages
2,532
Likes
11
Points
0
M

Mbopo

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2008
2,532 11 0
Tuache kuwa tunamlinganisha Mwalimu na viongozi wetu kwa kila jambo. Mazingira hutofautiana, lakini vile vile mifumo inatofautiana kwa kiasi kikubwa sana.
 
DSN

DSN

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Messages
2,791
Likes
129
Points
160
DSN

DSN

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2011
2,791 129 160
Tuache kuwa tunamlinganisha Mwalimu na viongozi wetu kwa kila jambo. Mazingira hutofautiana, lakini vile vile mifumo inatofautiana kwa kiasi kikubwa sana.
Kuwa Mwasisi manake nini? Mimi nafikilia kuasisi manake kuanzisha,kisha wengine wanafuata.Please
 
G

gkalunde

Senior Member
Joined
Mar 30, 2011
Messages
108
Likes
0
Points
0
G

gkalunde

Senior Member
Joined Mar 30, 2011
108 0 0
Tuache kuwa tunamlinganisha Mwalimu na viongozi wetu kwa kila jambo. Mazingira hutofautiana, lakini vile vile mifumo inatofautiana kwa kiasi kikubwa sana.
Kwhiyo unataka kutuambia Mwalimu angekuwa mkuu wa nchi sasa hivi mambo yange kuwa hivihivi yalivyo sasa kwa kuwa mazingira yapo tofauti kwa kiasi kikubwa na mifumo ipo tofauti hebu fafanua mkuu, nina uhakika hasa hili suala la uwajibikaji lingekuwepo tu hebu fikiri leo hii ni wangapi wanajua kuwa Rais Kikwete akitoa maagizo kwa wasaidizi wake hayatekelezwi na wateule wake wakianza kutekeleza sheria tu ambazo zipo Rais anawakataza mfano suala la uvunjaji nyumba zilizo kwenye maeneo ya barabara ni aibu ndio maana tunasema serikali hii ni legelege injiendea tu.
 
T

Tata

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2009
Messages
5,413
Likes
1,178
Points
280
T

Tata

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2009
5,413 1,178 280
huyu mzee kimiti is so naive na pia mnafiki mkubwa lini kikwete alianza kuwachunguza viongozi wake wenye mali nyingi ambao hawana maelezo walikozipata sana sana amekuwa akiwatetea mafisadi kila kukicha kama akina jairo, chenge, rostam na lowassa sasa anachokifanya Kikwete actually ni kuzuia wezi, wala rushwa na mafisadi wakubwa nchi hii wasichunguzwe kwa mujibu wa mkurugezi wa Takukuru Bw.Hosea atakwambia ktk private conversion alizozifanya na wamarekani.
Sasa asiposema hivyo atakumbukwa lini kupewa uenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shirika lisilokuwa na wenyewe - aah sorry shirika la umma?
 
T

Tata

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2009
Messages
5,413
Likes
1,178
Points
280
T

Tata

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2009
5,413 1,178 280
Inasemekana enzi hizo wakati mwingine mawaziri wakiwa na tuhuma akiitwa ikulu anabanwa mpaka kiwango cha kula pingu na kuambiwa apelekwe keko.Inasemekana jasho lilikuwa linawatililika wakisikia wanaitwa ikulu.Manake walikuwa hawajui ukiitwa ikulu unaitiwa nini?Waweza kuingia getini ukifika uko ndani kustaajabu unaweza kukuta unaitwa kupewa pongezi kwa kazi nzuri a kutoa ushauri kwa Mwalimu au kupokea kibano cha kiutu uzima.

Manake walikuwa wanajua kama unaitwa ikulu si kwa nia ya uteuzi kwa kuwa uteuzi wa Mwalimu mwingi ulikuwa ni surprise walikuwa wanajua kupitia Radio Tanzania Dar es Salaam.Kwa hiyo ni hakika Mwalimu alikuwa anagawa kibano kwa wale wote waliokuwa na tuhuma za kiajabu ajabu kwenye utawala wake.Ndio maana Ikulu ilionekana kuwa ni sehemu takatifu.
Na hili ndio lilikuwa tatizo kubwa la kiuongozi ambalo limeacha ombwe lisilozibika mpaka leo. Nyerere alitakiwa kuimarisha taasisi endelevu ambazo zingekuwa zikifanya kazi za kuwabana viongozi waroho. Badala yake akawa anaendesha nchi kama duka la mhindi. Matokeo yake alipoondoka tu haya majamaa aliyokuwa akiyabana yakafunguka na kuanza kuiba bila huruma yakijua kuwa aliyekuwa akiyabana ameondoka. Kwa ufupi majizi yetu ya leo ndio majamaa yaliyokuwa yakionekana kuwa maadilifu wakati wa Nyerere. Yalikuwa ni machui ndani ya ngozi ya kondoo.
 
sinafungu

sinafungu

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Messages
1,429
Likes
584
Points
280
sinafungu

sinafungu

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2010
1,429 584 280
KIJANA TAIFA LA KESHO. wao hawataki kustaafu , kila kukicha ni kupeana vyeo mara mwenyekiti wa bodi mara mkurugenzi wa...., mara mkuu wa mkoa nk. hawana jipya , akili zao zimefika mwisho . hayo ya kutengeneza mazingira mazuri kwa kizazi kipya hawana ufumbuzi wake. kwa hiyo si ajabu ukimsikia mtu kama huyo akimsifia rais ( atalipaje hisani ) xxxxxx zao
 
Forum statistics

Threads 1,264,257
Members 486,220
Posts 30,177,559