Waziri atetea matumizi ya magari ya kifahari serikalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri atetea matumizi ya magari ya kifahari serikalini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 2, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Date::2/2/2009
  Waziri atetea matumizi ya magari ya kifahari serikalini
  Na Mwandishi Wetu
  Mwananchi​

  SERIKALI imezitaja zababu za kununua magari ya kifahari na ya bei kubwa ya aina ya "mashangingi" kwa ajili ya wizara na idara zake.

  Naibu Waziri wa Miundombinu, Hezekiah Chibulunje alielezea aina hiyo ya magari kuwa ni imara na yanayoweza kuhimili safari ndefu vijijini.

  "Kigezo kinachotumika kununua magari aina ya ‘Four wheel drive' maarufu kama 'mashangingi' kwa Wizara na idara zake ni ubora, uimara na usalama wa magari hayo, kuweza kuhimili safari ndefu katika barabara za vijijini ambako viongozi na watumishi wengi wa umma hulazimika kwenda kuwahudumia wananchi," alisema Chibulunje.

  Alisema tangu magari hayo yaanze kutumika nchini mwishoni mwa miaka ya 1980, serikali imekuwa ikitathmini mwenendo wa gharama za matumizi ya magari hayo.

  Alifafanua kuwa katika tathmini hiyo, ilibaini kuwa maghari hayo yanapoanza kuchakaa, gharama za kukarabati zinapanda maradufu.

  "Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kupunguza gharama za matumizi ya magari hayo, ikiwa ni pamoja na kufuta magari yaliyochakaa kila baada ya miaka mitano," alisema Chibulunje.

  Vile vile, alisema serikali imekuwa ikihakikisha kuwa, magari hayo yanatumika inapolazimu, ili kupunguza gharama na matumizi yasiyo ya lazima.

  Pamoja na uzuri wa magari hayo, Chibulunje alisema kuwa serikali inao mkakati wa kupunguza wingi wa magari hayo nchini kwa kubana ununuzi wake.

  Katika mpango mpya ambao unaandaliwa na wizara yake, alisema utaweka utaratibu wa matumizi ya serikali kufuatana na wadhifa wa viongozi.

  "Wizara yangu, hivi sasa inaandaa waraka wa baraza la mawaziri juu ya utaratibu wa matumizi ya magari ya serikali kufuatana na wadhifa wa viongozi wa serikali," alibainisha Chibulunje.

  Alisema mpango huo wenye lengo la kupunguza matumizi ya mashangingi ukikamilika, utapelekwa kwenye baraza la mawaziri, ili kupata baraka zake kabla ya kuanza kutumika.

  Maelezo ya serikali yalitokana na swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya (Chadema) aliyeeleza kuwa matumizi ya magari ya kifahari aina ya mashangingi, yamekuwa yakiongeza matumizi yasiyo ya lazima serikalini.

  Owenya alitaka kujua kigezo kinachotumika katika kununua magari hayo, pamoja na mipango ya serikali kwa siku za baadaye.

  Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni alitangaza kuwa serikali yake ina mpango wa kupunguza matumizi ya magari ya kifahari na ya bei kubwa, ili kubana matumizi.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Kimsingi Waziri anasema kutumia haya magari kwa miaka mitano na "kuyafuta" -sijui maana yake nini- ni nafuu zaidi ya kuyakarabati.
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu hao kuna ujumbe mkubwa tu. Kufuta kunaweza kuwa kuyauza na kununua mapya (nani anauziwa) au yanahesabiwa kuwa yame-expire na hayapo tena katika hesabu ya mali za serikali.
  Kimsingi mashangigi ni moja ya incentive kubwa ya watu kuacha profession zao na kujiunga na politics, kama yakondolewa na wakaanza kutumia magari ya kawaida hakutakuwa na mvuto tena wa kugombea nyadhifa.
  Lakini mengine anayoyasema Mh Waziri si kweli ni uongo ulio wazi. Ina maana magari yote ya kifahari hwa yanaenda vijijin kwenye barabara mbaya? I wonder kama Jaji mkuu gari yake inaenda vijijini ipo Dar karibu kila siku lakini ni four wheel drive. Kuna maofisa wengi tu wa serikali ambao huwa hawatoki nje ya Dar es salaam lakini wana mashangingi, au Dar es salaam nako attoa kisingizio cha makorongo?
  Tuseme kweli tunapenda maisha ya kitajiri, na kutowajali wananchi. Solutin ni kutengeneza barabara yanakoenda magari hayo na sio kutetea ununuzi wake.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Kama sikosei tuna mikoa 27, kila mkoa ukiwa na magari 3 au hata manne kwa "ajili ya safari za viongozi" kwenda 'kuwahudumia' wananchi basi magari hayo yanaweza kabisa kufanya safari hizo za kuwasafirisha hao viongozi huko vijijini na kazi yake itakuwa ni hiyo tu badala ya kununua magari 800 mpaka 1,000 kila baada ya miaka miwili ambayo yanaongeza gharama kubwa za uendeshaji wa serikali.
   
 5. K

  Koba JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ....huyo waziri ni fisadi mwingine tuu na hana idea hayo magari yalivyo kuwa unprodutive kwa vitu anavyotetea na hasara kwa taifa,wajifunze kwa Kagame maana hakuna upuuzi kama huo na wameweza!
   
Loading...