Waziri atetea madaktari kulipwa mishahara minono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri atetea madaktari kulipwa mishahara minono

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mlaizer, Apr 11, 2012.

 1. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [TABLE="align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"]UDAKTARI, Uanasheria na Uhandisi zimetajwa kuwa ni kada za utumishi zenye uzito mkubwa zinazostahili mshahara mkubwa kuliko nyingine.

  Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Ummashi, Hawa Ghasia alisema kada inayoongoza kwa uzito ni udaktari ikifuatiwa na Sheria na Uhandisi.

  "Tathmini ya kazi iliyofanyika serikalini mwaka 2000 inaonesha kuwa kada ya udaktari ilikuwa na uzito mkubwa ikilinganishwa na kada nyingine na ndiyo maana ikatengewa mshahara mkubwa ikilinganishwa na kada nyingine," alisema Ghasia.

  Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi) aliyetaka kufahamu vigezo ambavyo Serikali inatumia kutofautisha mishahara ya kada mbalimbali za watumishi wa umma kama vile walimu na madaktari.

  Machali alitoa mfano kwamba mwalimu mwenye Shahada analipwa Sh 400,000 lakini Daktari mwenye Shahada analipwa Sh 900,000 wanapoanza kazi.

  Alihoji kama hali hiyo siyo ubaguzi, inayowavunja moyo baadhi ya watumishi walio na viwango vya elimu sawa lakini wanalipwa kidogo.

  Waziri Ghasia alisema tofauti na viwango vya mishahara kati ya kada moja na nyingine inatokana na uzito wa majukumu uliofikiwa baada ya tathimini.

  Alisema uzito hupimwa kwa kuzingatia kiwango cha elimu na muda unaohitajika kupata elimu husika, uzoefu unaohitajika, usimamizi wa rasilimali mbalimbali, athari au umuhimu wa kazi, mazingira ya kazi na uhuru wa kufanya uamuzi wakati wa kutekeleza majukumu husika.

  Alisema utaratibu huo hutumika hata katika sekta binafsi na duniani kote na ndiyo unaotumika katika utumishi wa umma kupima tofauti ya majukumu miongoni mwa kada zilizopo katika utumishi wa umma.

  "Pamoja na kwamba viwango vya elimu miongoni mwa watumishi wa kada mbalimbali vinaweza kufanana, ni ukweli usiopingika kwamba uzito wa majukumu hauwezi ukalingana na kada nyingine," alisema.

  Akisisitiza kuwa hakuna ubaguzi katika kupanga mishahara ya watumishi, akisema; "kwa mfano, uzito wa kazi ya Daktari hauwezi kuwa sawa na uzito wa kazi ya Ofisa Utumishi pamoja na ukweli kwamba wote ni wahitimu wenye
  Shahada ya chuo kikuu."

  source:habarileo la 11/04/2012

  NB:Kwa hoja hizi sekta zingine zitaendelea kudorora siku hadi siku,tofauti ya mshahara kwa zaidi ya mara mbili hauwezi kuhalalishwa kwa hoja hizi.Mwalimu ambaye ndiye anayewaandaa hao watumishi wengine wote ndiyo mshahara wake uwe wa mwisho?

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  It is true Hawa
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Well, anaweza kuwa na hoja. Unahitaji angalau miaka saba kuwa daktari ama architect wakati course nyingine kama za ualimu kwa mfano ni miaka mitatu tu! Tukisema watu hawa wawili wawe sawa pengine inaweza isiwe fair sana. Lakini ni tofauti kiasi gani na hata kama kuna tofauti je malipo hayo yanakidhi? Yaani hiyo laki 9 ya daktari inafaa?
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Sasa kama yote haya yana julikana tokea mwaka 2000 kama Ghasia anavyo dai mbona kulikuwa na mgomo wa madaktari mwaka jana?
   
 5. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kosa moja dogo tu la Daktari, ni kifo, irreversible.
  Mwanasheria akikosea, kuna fursa ya rufaa.
  Mwl akikosea, kuna fursa ya masahihisho.
  Pia walimu wanaenda kusoma baada ya kufeli au kufaulu kidogo.
  Ila wahadhiri, kwa vile wamefaulu sana, wanalipwa vema tu, kuliko hata madaktari.
  Hujiulizi wangapi wanafanya makosa kwenye fani zao, lkn kosa la "mguu badala ya kichwa" linaimbwa hadi kesho?
  Huo ndo unyeti wa udaktari.
  Pia kuna urefu wa shule, ugumu wa shule, risks kibao za kuambukizwa maradhi, family instability(kuna hatari ya kupata watoto wasio wako ukiwa on call) na ile hali ya kuwa ni "noble proffesion"
   
 6. N

  Ningu Member

  #6
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inavutia...is this true?
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,783
  Likes Received: 419,796
  Trophy Points: 280
  huyu mbunge ni bomu sana.........naona yuko huko kula posho tu na hana mchango wowote ule kwenye jamii................alivyo mnafiki anazungumzia usawa wa malipo wakati wao wanajipitishia mishahara na posho kubwa hapo bungeni mbona hakusema ya kuwa bunge halistahili hayo mamishahara? La pili kama ni kweli daktari na mwalimu elimu ni sawa kwa nini waalimu hawapangiwi kazi ya udaktari...........kwa nini mwalimu anasomea shahada miaka 3 wakati daktari miaka 5 plus internship?
   
 8. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  kwa hiyo vyuo vikuu vinapokea wanafunzi waliofeli kusomea ualimu?je tofauti kubwa kiasi hicho inaweza ku-justify hii hoja kweli?
  Hapo sidhani kama hoja yako ni sahihi kwani tuna wanafunzi walikwenda kusomea udaktari kwa cut-off point ambazo ni sawa na wale wa ualimu.
   
 9. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Kwenye ajali watu wengine mkiona kidonda tu kibichi mnafumba macho tena mmeona kupitia TV (runinga) na mnalalamika hii picha mbaya hawajui kuna watoto kumbe wewe ndiye uliyesisimka. Hao madaktari wao ndiyo kazi akitika kwenye kidonda anakwenda kwenye mkojo, damu na mavi ya watu tena wasio ndugu zake. Mkisikia madaktari wanalalamika tuwe wa kwanza kuwaunga mkono. Yesu moja ya kazi zilizomfanya afuatwe na watu kotekote alikokuwa akihubiri ilikuwa ni udaktari (kuponya wagonjwa wa mwili na mapepo) ukiacha kundi lingine la wenye njaa waliotaka kushibishwa. Tuwaheshimu sana madaktari, wala tusiwalinganishe ktk fani zetu wako hatua ya mbali mno kulinganishwa na mwalimu, mwanasheria au mhandisi. Ukimtukana baba yako unalaaniwa na siku zako za kuishi zinapungua, lakini ukimtukana daktari wewe kesho kufiki kila mahali mwilini panauma sijui nani atakutibu!!! hata wa kalumanzila na matunguli yao wanaiga kuponya (muhimu sana)
   
 10. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mwalimu hawezi kufanya kazi ya daktari kwa sababu hakusomea daktari hivyo hivyo kwa daktari.walimu walikuwa wanasomea shahada kwa miaka 4 ila wakajakubadilisha juzi baada ya kikwete kuingia madarakani ili kuweza kutatua tatizo la upungufu wa walimu na hii ilikuwa ikome kwa muda kama sikosei mwaka huu(ingawa sio rahisi warudishe miaka 4 kwa sababu ya siasa zilizoingilia kwenye elimu).
  Lakini hata hivyo,tofauti ya miaka 2 ndiyo ifanye tofauti ya mishahara iwe kubwa kiasi hicho?
   
 11. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  U cant be serious .. mwalimu wa shahada ya kwanza kamwe huwezi kumfananisha na dactari!... ugumu wa elimu na pia ikatokea upungufu wa madactari mwalimu hawezi kuziba pengo.. lakini ikatokea upungufu wa walimu! Dr. anauwezo wa kwenda kupiga shule ya biology kwa vijana + maths! ...
   
 12. Medical Dictionary

  Medical Dictionary JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,053
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  big up hawa ghasia..hyo ni kwel kabisa...nabado tunasubiria budget mishahara ya madaktar inaongezwa(moja ya madai yao ya mgomo)..by the way nashangilia coz mimi ni daktar mtarajiwa..
   
 13. CHIHAYA

  CHIHAYA Senior Member

  #13
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 103
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Acha kuichezea Maths weweee! Nimefundisha Sekondari na sasa Chuo kikuu, usifikirie zile hesabu za wadudu wa3 wa maralia ukawachukulia poa walimu wote. Ni ukweli usiopingika shule ya mtu kuwa daktari ni nzito but gap limezidishwa mnoo though wote pesa haiwatoshi ukizingatia hali halisi ya maisha kitaa. Tuuze mgodi wa buhemba completely tununue vifaa vya kuchimbia madini kwenye migodi mingine yote maana wataalamu tunao kwa sasa then tuchimbe wenyewe na kusafisha baadala ya kusubiria 3 percent. Ila na ccm isiwe madarakani mbna ndo ina watu wanaokumbatia hii sera kwa kuwa wanapata cha juu kutoka kwa Wanaoitwa wawekeza jini.
   
 14. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kufundisha mathematics?hata kufundisha inahitaji utaalam ambayo daktari hajaisomea?jaribu kutofautisha ufahamu wa mada na uwezo wa kufundisha.unaweza kufahamu mada lakini kwa sababu kutokuwa na taaluma ya ualimu ukashindwa kufundisha,ndio maana leo mhandisi akiamua kuacha kazi ya uhandisi na kujiunga na ualimu analazimika kufanya postgraduate diploma in education.
   
 15. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Mpaka leo huwa sioni ni kwa nini mwanasheria anakuwa na uzito mkubwa kuliko mchumi??

  Hawa, na ma-Vet Doctors nao wako kwenye group ipi?? maana wanasoma miaka sawa na medical doctors!!!
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Apr 11, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Hata mimi.

  Ila wenyewe watakuambia kwa vile wao ni "wasomi" hivyo wanastahili zaidi.
   
Loading...