Waziri ataka wanafunzi waandamane wenzao waliokopa walipe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri ataka wanafunzi waandamane wenzao waliokopa walipe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr. Zero, Nov 7, 2011.

 1. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Waziri ataka wanafunzi waandamane kuwadai wenzao waliokopa walipe [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 06 November 2011 20:11 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Peter Saramba, Arusha
  NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amewasihi wanafunzi wa elimu ya juu nchini kuandamana ili kushinikiza waliokopeshwa fedha za elimu miaka ya nyuma walipe ili wapewe wengine.

  Amesema wahitimu wengi walikopeshwa zaidi ya Sh21 bilioni ili kusoma kwenye vyuo mbalimbali, lakini baada ya kupata kazi wanakwepa kulipa mikopo hiyo.

  Mlugo alisema wanaosoma vyuoni sasa hawana budi kuandamana ili kuwashinikiza waliotangulia walipe fedha hizo ili ziweze kukopeshwa kwa wanafunzi wengine zaidi.

  “Fedha hizo zilikopeshwa kwa wanafunzi wa elimu ya juu tangu utoaji wa mikopo ulipoanza mwaka wa masomo wa 2004/05 na kama zitapatikana zitaiwezesha Serikali kukopesha wahitaji wengi zaidi kuliko idadi ya sasa”, alisisitiza.

  Naibu Waziri Mulugo alisema hayo alipozungumza kwenye sherehe za mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Mount Meru eneo la Ngaramtoni, nje kidogo ya mji wa Arusha.

  Alisema baadhi ya wanaodaiwa fedha hizi wamefanikiwa kupata ajira rasmi huku wengine wakijiajiri wenyewe baada ya Serikali kugharamia elimu yao kupitia mikopo ambayo sasa hawataki kurejesha.

  “Tusiandamane (wanafunzi) kudai mikopo kutoka bodi ya mikopo pekee, sasa tuandamane pia kushinikiza waliokopeshwa sasa wanafanya kazi au kujiajiri warejeshe fedha walizokopeshwa ili ziingizwe kwenye mzunguko utakaowezesha wengi kufaidika,” alisema Mulugo akipigiwa makofi.

  Alisema Serikali ina nia ya dhati kuhakikisha wote wanaofaulu na kupata sifa za kujiunga na elimu ya juu wanapata fursa hiyo bila kujali uwezo kiuchumi wa mhusika, wazazi au walezi wake, lakini lengo hilo linakwamishwa na kipato kidogo na changamoto nyingi zinazohitaji kushughulikiwa na Serikali akitaja uboreshaji wa huduma za afya, miundombinu na huduma zingine za kijamii.

  Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Naibu waziri huyo, idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu wanaokopeshwa imekuwa ikiongezeka kila mwaka wa masomo ambapo mwaka 2004/5 , Sh 9.9 bilioni zilitumika kuwakopesha wanafunzi 16,345 kabla ya idadi hiyo kuongezeka hadi kufikia wanafunzi 42,729 mwaka uliofuata.

  Kuhusu maendeleo katika sekta ya elimu, hasa elimu ya juu, Naibu waziri huyo alisema nchi ilipopata uhuru mwaka 1961 kulikuwa na chuo kikuu kimoja pekee lakini sasa vipo vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki 41, kati ya hivyo 12 vikiwa vy umma na 29 vya binafsi huku udahili ukiongezeka kutoka wanafunzi 14 kwa wakati huo hadi 155,757 kwa sasa.

  Katika risala yao kwa mgeni rasmi, wahitimu 414 wa Chuo Kikuu cha Mount Meru waliishauri serikali kuwa pamoja na kuanzisha dawati la mikopo vyuoni, muda umefika wa kufikiria kuanzisha Ofisi za Kanda za Bodi ya Mikopo ili kurahisisha na kuongeza ufanisi kiutendaji.

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [h=4]Comments [/h]


  0 #3 bugota 2011-11-07 07:55 Mheshimiwa tunashukuru kwamba umeongelea hilo. Lakini ikumbukwe kwamba swala la kusomeshwa na serikali halijaanza 2004/2005 pekee bali ni kuanzia enzi zile zenu nyie Vigogo. Tena nyie ndio mlikula pesa nyingi za Watanzania kuliko sisi ambao hata pesa zilikuwa zinatolewa baada ya kuwa tumepigwa Mabomu pale Survey karibu na Mwenge.
  Pia Serikali imeshindwa Kudhibiti Wawekezaji amabao wanaendelea kupora ajira za Watanzania migodini na kuingiza watu wao wasio hata na elimu na kwa kuwa UHAMIAJI nao wamejaa RUSHWA, wanatoa tu vibali vya kufanya kazi kwa watu hawa.
  Mbali na hayo, Serikali imeshindwa kuwaamuru Mafisadi woote warudhishe pesa za Watanzania ziweze saidia haya.

  Sasa kama tumesoma halafu ajira zinaenda na wageni, mnategemea tulipe vipi wakati sasa hivi tumelazimika kufanya kazi ambazo hazihusishi kabisa Elimu zetu?

  Hapa mmekwama.... Haturudishi ng'o hadi mrudishe pesa za EPA, RICHMOND na DOWANS..
  Quote


  +1 #2 matiko matale 2011-11-07 07:43 walioiba ndo waanze kurudisha kisha waliokopa wadaiwe
  Quote


  0 #1 rutashubanyuma 2011-11-07 06:53 Quote:
  NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amewasihi wanafunzi wa elimu ya juu nchini kuandamana ili kushinikiza waliokopeshwa fedha za elimu miaka ya nyuma walipe ili wapewe wengine.​

  huyu atabaki kuwa naibu tu...................hajui ya kuwa ugumu wa maisha ndiyo unawafanya wasiweze kulipa.................jawabu ni kuwasamehe wote wale itakaobainika hawajapata kazi kwa miaka 5 tangia wamalize mafunzo yao....................mbona makampuni hewa husamehewa madeni na hata bunge huhusishwa?
   
 2. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  kumbe bado atuja deni letu bado hafujafika mahela walioiba ya EPA kwa sasa tusamehane ngoja na mie ninunue VITZ kwanza ndio tutangalia namna ya kurudisha hizo pesa waache ujinga warudishe kwa pesa walizofisadi ndio nasie tutawalipa hizo alaaaaaaaaaaah.
  mmetutesa sana na mikopo yenu utafikiri sio wajibu wenu kutosemesha tuje kuokoa hii nchi ambayo haijakomboka kifikra kwa kiasi kikubwa sana
  walidushe kwanza wao ..............
   
 3. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  kumbe deni letu bado hafujafika mahela walioiba ya EPA ,na makashfa yote LOL kwa sasa tusamehane ngoja na mie ninunue VITZ , nipeleke wadogo zangu sekondari kwanza ndio tutangalia namna ya kurudisha hizo pesa waache ujinga warudishe kwa pesa walizofisadi ndio nasie tutawalipa hizo alaaaaaaaaaaah.
  mmetutesa sana na mikopo yenu utafikiri sio wajibu wenu kutosemesha tuje kuokoa hii nchi ambayo haijakomboka kifikra kwa kiasi kikubwa sana
  walidushe kwanza wao ..............
   
 4. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Mimi nilitegema waziri awaombe wananchi waandamane kushinikiza pesa za EPA ziingizwe kwenye elimu, taifa linawaelimisha vijana wake kwa shingo upande utadhani watoto wa kambo! Kuna mianya mingapi inayovujisha pesa za umma katika taifa hili na sijasikia waziri yeyote akitoa tamko la kuandamana? Je waziri ameshafanya tathimin hao waliosoma kwa mkopo wa serikali wameajiriwa na wanalipwa japo kiasi cha kujikim kimaisha mathalani wawe na uwezo wa kulipia kodi ya nyumba, usafiri, chakula, mavazi, umeme, maji nk?
   
 5. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Hii inaonyesha jinsi serikal yetu ilivyo legelege,serikal makini inakuwa na mfumo madhubuti unaohakikisha wadaiwa wanalipa.
   
 6. Nico1

  Nico1 JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Mbona sijasikia waziri akihamasisha maandamano juu ya mafisadi,mikataba mibovu,rushwa,katiba mbovu,nk siwezi kupoteza muda wangu kwa mambo ya kipuuzi kama hayo aandamane mwenyewe pamoja wizara yake mimi simo.
   
 7. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu waziri kimeo kweli kweli. Yaani anataka watu waandamane kwa makosa ya serikali yake yenyewe.
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  kila mwenye mawazo ya kishetani, anamwakilisha shetani na alaaaniwe kwa nguvu zote!
   
 9. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  Kwani analijua hilo???
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  yule nae ni mpuuzi tu watu walipe watalipia nini????????kuna watu wana miaka mi3 mtaani tangu wamalize chuo hawana ajira,waajiri watu ndo wawakate kwenye mishahara
   
 11. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Mimi nawashangaa sana hawa watu, kuna waraka umekuja ofcn kwetu unasema kila mtu aorodheshe chuo alichosoma na idadi ya mkwanja alioukopa ili waanze kufanya deducation kwenye mishahara yetu, sasa mimi sielewi kodi ninayolipa inafanya kazi gani?
   
 12. L

  Lua JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  unaandamana kuelekea makwao hao waliokopa! coz wengi wao hadi sasa hawana ajira.
   
 13. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kweli Mulugo anaumwa wazimu, anangoja nini kujiuzulu uwazili kama hana analolijua na hana mkakati wa kukusanya madeni hayo?Kwani wanafunzi wakiandamana ndio atapata takwimu za wadaiwa na wapi walipo? Haya ndio madhara ya kupeana vyeo kwa mitandao.
   
 14. Pdraze

  Pdraze JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Waandamane wakafikishe ujumbe kwa nani? Au kuna chama cha wanaodaiwa na bodi dah hii nchi tamu sana kwa wajanja ila chungu kwa mapatriot
   
Loading...