Waziri ataja sababu 3 za vurugu za Nyamongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri ataja sababu 3 za vurugu za Nyamongo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lilombe, May 31, 2011.

 1. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF jana usiku katika kipindi cha DAKIKA 45 kinachorushwa na ITV ambacho mgeni alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi; S. Nahodha alipoulizwa juu ya kiini cha vurugu za Nyamongo alitoa sababu zifuatazo:-

  1. Kuwepo kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara ambapo wengine wanafaidika na kuwepo kwa mgodi na wengine hawaifidiki. Wasiofadika na shughuli za uchimbaji madini wanashawishi vijana kuvamia mgodi kwa nia ya kuiba dhahabu.
  2. Kuwepo kwa uwingi wa vijana wasio na ajira wanaozunguka mgodi. Wengi wa vijana wanaona shughuli za mgodi haziwapi kipato cha ina yoyote hivyo wana mtazamo hasi dhidi ya wawekezaji pamoja na shughuli zao.
  3. Wawekezaji kushindwa kutimiza masharti ya uwekezaji juu ya kuboresha maisha ya wananchi wanaozunguka migodi.
  Pia amesema amewasiliana na Waziri Ngereja kwa nia ya kuhakikisha wawekezaji wa sekta ya madini wanatimiza masharti ya uwekezaji.
  Hivyo kwa mujibu wa mahojiano ya jana usiku, Waziri hakugusia sehemu yeyote kuwa CDM ilitia MKONO katika vurugu hizo.
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Ilikuwa ni taarifa ya RPC na naibu wa waziri
   
 3. suleym

  suleym JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,714
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  sasa huyo naibu wake alitoa wapi hayo maneno ya kuhusisha vurugu na chama 'flani' cha siasa,.
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Taarifa za kiinteligensia hapo nafikiri ila sasa zinapingana na za mkuu wake au wakuu wao wa kazi
   
 5. L

  Luiz JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amejitaidi kuzungumzia mambo ya muhimu lakini kwa kiasi kikubu hizo vurugu zinasabishwa na serikari kutowajibika kwa wananchi kuhusu wawekezaji kama umesoma kitabu kilichoandikwa na ChaChage kinaitwa "MAKUADI WA SOKO HURIA" utajua uhalisia wa suala linalotokea sehemu kama Nyamongo na sehemu nyingine zenye uwekezaji.
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Na sababu zote alizotoa zinajulikana
  Wawekezaji hawana nia ya kumuinua mtu wa chini pale walipo na hawana hata nia ya kutekeleza kile walichoambiw awafanye au kilichomo kweney mkataba la sivyo wasingewakejeli wananchi kwa kuwajengea shule ambazo mbuzi akijikuna kwenye ukuta unaanguka au barabara za kokote eti hiyo ni miundombinu
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nimependa hii sababu ya tatu

  Wawekezaji kushindwa kutimiza masharti ya uwekezaji juu ya kuboresha maisha ya wananchi wanaozunguka migodi
   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Ndio sababu kuu kwa nini wananchi wamechoka
  Sio migodi tuu hadi kweney vitalu vya uwindaji na mbuga za wanyama
  Misitu ya serikali
  Mashamba makubwa ya wawekezaji
  Wanacnhi wamechoka
  Angalia wawekezaji kwenye mashamba ya miwa kule babati wanavyochoma mashamba ya wawekezaji baada ya kujikuta hawaoni tofauti yoyote ya kuwepo kw amashamba hayo bora ardhi hiyo wangepewa wao walime mazao ya chakula
   
 9. m

  mwl JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 861
  Likes Received: 587
  Trophy Points: 180
  Kama kweli hawa ni watendaji wa JK basi yeye ni kilaza, wameweza kutoa sababu wakashindwa kutoa solutions, ni viongozi au viongozwa? Hayo mawili ya kwanza hayana majibu tujuzeni.
   
 10. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160

  Watanzania tumeshajua ukweli; CDM hawachomoki na machafuko ya Nyamongo, KIASHIRIA kiko wazi Viongozi wa CDM walikuwa wanaijua move yote. Walikuwa wa kwanza kukimbilia Nyamongo baada ya tukio.
   
 11. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Weee! Kusema "watanzania tumeshaujua ukweli" ni kuwasemea watanzania, ambayo literally ni KUWADHALILISHA kuwa wana akili kama yako. Mbaya sana!
   
 12. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  afadhali amekuja kuzungumza mwenyewe!
   
 13. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  inakera sana pale wanaposema wawekezaje wanatoa huduma muhimu kama kujenga shule, dispensari
  kitu ambacho sio sahihi haviendani na mali wanazochuma
   
 14. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,582
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Watanzania wengi tuna akili timamu hatuna makengeza ya akili kama wewe.Na hata wewe ukweli unaujua ila tu ndiyo ile MTUMIKIE KAFIRI......... Ni njaa tu inakusumbua.
   
 15. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Ukipiga mahesabu ya hizo shule na dispensary ni kama tone kwenye bahari maana kama ni shule ni just majengo hayana vitabu hayana walimu wa kutosha wala maabara za maana na hospital wanatoa majengo na vitanda may be ila dawa hakuna wala madakrati ni issue sasa hapo sijui ndo wamefanya nini
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Huu ni uongo mkuu, mwenye makosa ni serikali yetu, Kwenye mkutano alioufanya juzi Godbless Lema alisema baada ya mauwaji ya nyamongo alienda kwenge migodi hiyo akaomba kuongea na wakubwa...walicho kisema ni kwamba wanaishangaa sana serikali kwani wao waliandaa mpango wa kuwasaidia wananchi wa nyamongo kwa kuwapa mchanga katika mpango huu walihitaji bilion tatu kama sikosei, wakaiomba bank ya dunia ikakubali kuwapa kiasi hicho cha pesa, Barick wakampelekea waziri wa madini "Gereja", cha ajabu haja wajibu chochote mpaka mauji yametokea, wakasema hata wao kibiashara inawaharibia sana kwani biashara yao imeshuka kwa asilimia 7.5 watu hawataki kununua madini yanayo nuka damu...sasa tujiulize viongozi wetu wako kwa maslahi ya nani, je wanafaindiaka na damu ya watanzania ndiyo maana hawataki kutatua matatizo......
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu hatuna haja ya kuwalamu wawekezaji tuwalau viongozi wetu...yaani ni kama kumfumania mkeo na jamaa halafu unaanza kumlau jamaa ni ujinga wewe ulie na mkataba nae ni mkeo...hivyo na ni sisi tunatakiwa tuwakomalie hawa viongozi wetu na kwa kuwa wameshindwa kutekeleza/wametusaliti tuwaondoe....
   
 18. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280

  Mkuu maoni yangu hapa yalikuw asio kuwalaume wawekezaji bali ni kuilaumu mikataba ambayo serikali imeingia na wawekezaji husika maana wawekezaji wanatekelez akile ambhacho kimeandika kwenye mkataba
  Kama kwenye mkataba wako kumeandikwa utatoa huduma za kijamii kama ujenzi wa shule na dispensary mwekezaji anatekeleza hata kama shule haina madawati hiyo sio kazi yake ila yeye ni kujenga shule
  Ubovu unakuja na wa kulaumiwa ni serikali ambayo wakati wanasaini mkataba haikujiuliza ni huduma zipi za kijamii na kwa kiwango gani maana walitakiwa waambiwe ni shule ya aina gani na iwe na nini so wakikabidhi shule huwezi tena kujikuta wanafunzi wa ile shule wanalalamika madawati hakuna au vitabu hakuna au hakuna huduma za maji
   
 19. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #19
  May 31, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  naungana na wewe mkuu
  wakuwalaumu ni viongozi wetu wasiosimamia vyema mali asili yetu,wao wanachojali ni 10% yao wakipata hiyo kila kitu kwisha
  watawala wa nchi hii wamekuwa wakiwakumbatia sana wawekezaji na kusahahu wananchi,wameweka sheria ambazo zinawanufaisha sana wawekezaji kuliko hata nchi husika,
  tunalamba sana miguu ya wawekezaji sasa wanaingia hadi chumbani na hatuna la kusema

  Angalia botswana kabla hujaanza project ni lazima utimize kile ambacho serikali imepanga juu ya wananchi wanaozunguka mgodi huo,lakini hapa kwetu imekuwa ni tofauti sana tena sana

  tumebaki kuwalaumu wananchi na kuwazingizia kuwa ni wezi na kuwapiga lisasi kama vile ni wakimbizi

  yatubidi kubadilika ktk sera na mipango yetu juu ya hii mali asili la sivyo ipo siku sehemu za machimbo zitakuwa hazishikiki
   
 20. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280

  Na hii ndio ilipaswa hiwe ya kwanza!
   
Loading...