Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum, nini majukumu yake?

Nchi hii ni ya ajabu kabisa. Bado kidogo tutaingia kwenye GUINESS WORLD BOOK OF RECORDS
 
Awamu ya Nne niliwahi kusikia Rais Kikwete alimteua Prof. Mark Mwandosya kuwa Waziri asiyekuwa na Wizara maalumu.

Kuna ukakasi fulani maana chini ya huyo Waziri kuna Naibu Waziri , Katibu Mkuu , Wakurugenzi na Watendaji wa Idara mbalimbali (za Wizara ).

Waziri asiyekuwa na Wizara maalumu ni Waziri wa namna gani ? Kazi zake ni zipi ? Nikimtaka Katibu Mkuu wa hiyo Wizara anakuwa wapi ?

Bunge hupitishaje Bajeti ya Wizara isiyokuwa maalum?

Ufafanuzi tafadhari
 
Back
Top Bottom