Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum, nini majukumu yake?

basically ni kwamba anaamka asubuhi anaenda kazini, analetewa chai na magazeti anasoma, anafungua computer yake anacheki emails zake akimaliza anaingia jamii forums anaanza kuchat na sisi mpaka jioni anafunga ofisi anarudi nyumbani.

Mwisho wa mwezi; mshahara, marupurupu kama viongozi wengine wa serikali, ana pension yake, house, fuel and car allowance. mshahara na posho kama wabunge wengine. Mradi anaishi na watoto wanasomeshwa. By the way tumeambiwa serikali haina hela. IT CAN ONLY HAPPEN IN BONGO :noidea:

Pana wakati huwa nnatamani kuwa kiziwi nisisikie mambo Kama haya,tusubiri bajeti ya mwaka huu namna ambavyo Serikali itawapandishia kodi watanzania.Kila kona itakuwa ni kilio
 
Katika karne hii ya 21 na muongo 1.Hii yapatikana tu Tanzania.BARAZA KUBWA NAMNA HIYO,Tena tunaletewa waziri mtembea popote.
 
kaazi kwelikweli! ngoja nisogee jirani labda nitapewa kanafasi,huko watu wanakwenda kula tu na kusinzia nothing more!!

Halafu na wananchi wanazidi kudanganywa kila iitwapo leo na ni wasahaulifu kweli Kama walivyokwisha kusahau ya Epa/Richmond to Dowans/B.o.t/Kagoda na hili la juzi la mawaziri kutafuna matrilioni ya pesa za walipakodi(wananchi)na hata Kikwete mwenyewe anatujua kwa usahaulifu(ni upepo tu utapita)
 
Wanajua atahamia CDM kwani ndo wabunge wachache wanaoipa CCM uhai. so ni vema atumie kodi hata bila majukum ili kulinda maslah ya Chama.
Ila mimi nataman huyu mzee asigombee tena 2015 ili kulinda hadhi yake asije akadhalishwa na ushind wa CDM
 
Najaribu kufikiria gari yake itakuwa inasomekaje? WAWM au? Hehehee

Hiyo plate number yake imenifurahisha sana:). Ofisi sasa inakuwa wapi? Maana mawaziri wengine wote ofisi zao zipo katika wizara zao husika! Huyu WAWM atafanyia wapi kazi zake za WIZARA ISIYO MAALUM?
 
Kazi zipo tele

1. Kuhudhuria vikao vya baraza la mawaziri na kutoa michango yake kwenye agenda husika;
2. Kuhudhiria vikao vya kazi vya baraza la mawaziri;
3. Kumuwakilisha rais, makamu wa rais au waziri mkuu pale itakapohitajika;
4. Kumuwakilisha waziri yeyote katika utekelezaji wa shughuli za kitaifa, ikiwemo bunge.
5. Nk

sio ajabu kuwa na waziri asiye na wizara maalum

hajaanzisha kikwete tanzania, baba wa taifa pia alikuwa nao;

post hii haijaanza tanzania, hata kwa wenye demokrasia ipo

Umenena vyema mkuu. Hapa umenipa mwanga mpana zaidi.
 
Hiyo plate number yake imenifurahisha sana:). Ofisi sasa inakuwa wapi? Maana mawaziri wengine wote ofisi zao zipo katika wizara zao husika! Huyu WAWM atafanyia wapi kazi zake za WIZARA ISIYO MAALUM?

Gari lake linatusaidia nini?
 
Wakuu, kwa wale wanaojua ni yapi majukumu/kazi za waziri asiyekuwa na wizara maalum anijuze kwani mimimkatika hilo ni mtupu.
mkuu niliandika post kama hii kabla yako lakini ilipotea ktk mazingira ya kutatanisha nikajiuliza nilikiuka utaratibu au ugeni wangu?haka ka wizara kamenichaganya kwa kweli.na moja kati ya swali langu waziri akienda bungeni atakuwa na bajeti na atakuwa na jengo la wizara?
 
Mie nadhani katika mambo ya msingi JK aliyofanya ni kujiweka karibu na Prof Mwandosya. Wanaomfahamu Mwandosya watakueleza wazi kwamba ni kiongozimakini sana, na in fact, sio mwanasiasa. JK atafanya la maana sana kumtumia kama mshauri wa karibu katika kipindi chake kilichobaki, na njia mojawapo ya kufanya hivi ni kumfanya waziri asiye na wizara maalum.

Na pia tumtendee haki Prof Mwandosya. Ni kiongozi makini na mzalendo. Je, tumtupe kwa kuwa tu amekuwa mgonjwa kwa kipindi fulani? Nadhani JK kumteua kuwa waziri asiye na wizara maalumu ni kumpa Mwandosya heshima sana, na pia kipindi cha kurudisha afya yake vema kuliko angempa kusimamia wizara kamili kwa hivi sasa. Nadhani ni bora hata pale Mwandosya atakapokuwa amepona kabisa JK akamtumia kama Waziri Mkuu. Kwa jinsi baraza la sasa lilivyo na PhD na Maprofessor wengi, huenda ni vizuri PM akawa huyu professor wa kikweli kweli na sio wa kudesa!

Tukumbuke kuna wakati Edward Sokoine alipumzika kwa miaka miwili toka uwaziri mkuu kwa kuwa alikuwa mgonjwa, na alipopona tu Nyerere akamrudisha uwaziri mkuu. JK kaamua kumpunzisha Mwandosya kwa namna hii ili asiwe mbali sana na yanayojiri katika baraza la mawaziri.

Kwa hili la Mwandosya ninakubaliana sana na JK, na natumaini watashirikiana vizuri kugeuza mwelekeo wa nchi na huenda hata chama chao CCM.
 
Hapo nampongeza Rais Kikwete coz Mwandosya atakua kama Gaucho au Zidane katika timu yaani mchezaji huru, so atakua anacheza namba zote and he deserve that position. I think this would be one of the good team to happen in Africa, much respect to JK for innovation of new strategies so as to reach accountability in our government
 
Cheo hiki cha waziri asiye na wizara maalumu katika hali halisi ni cheo kisicho na manufaa yoyote yale kwa taifa letu zaidi ya kutumia vibaya pesa ya walipa kodi wasio kula milo mitatu kwa siku, wasioweza kuwapeleka watoto wao katika shule binafsi, wasioweza kwenda kutibiwa india.......n.k

Kwa akili yangu ya kawaida ninachoona ni kwamba waziri asiye na wizara maalum ni waziri mkuu kwani wao ndio wanao uwezo kusimamia na kufatilia shughuli zozote zile katika wizara yoyote ile, cheo hiki anapopewa mtu mwingine tafsiri ni aidha waziri mkuu aliyepo hawezi kazi ama aliyepewa hicho cheo amepewa ili kulipwa fadhila kwa jambo fulani alilowahi kufanya au analoendelea kufanya.

NINI KIFANYIKE???
1. Cheo hicho kiondolewe kabisa kwani ni mzigo kwa walipa kodi

AU
2. Kutokana na udhaifu wa raisi(mnyika) basi Cheo hicho apewe fumua fumua(mwakyembe) au mtendaji mwingine anayefaa ambaye hatakuwa na mipaka ya kiutendaji, awe anakagua kila wizara kubaini uozo wake, kuondoa uozo na kufanya mabadiliko. Kwa kumuweka mtu anayefaa katika cheo hicho kidogo itafanya watu watambue umuhimu wa cheo hicho kuliko kukiweka cheo hicho kwa mtu ambaye kazi yake ni kuilinda serikali huo ni uhuni usio vumilika.

Kapondo,
 
Ni mwendelezo uleule uchumi kutumikia siasa, badala ya kutumikia maendeleo na ustawi wa wananchi. Ni uchoyo, kuhakikisha keki ya taifa ni stahili ya watawala pekee. Ni ufisadi kwani unaongeza ukubwa wa serikali na gharama za uendeshaji wake bila manufaa kwa umma.
 
Katika kupitia blog moja nimekutana na picha inayomuonesha Mh. Machano Othman Said ambaye ni Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum huko Zanzibar. Nakumbuka hata huku bara miaka ya nyuma waliwahi kuwepo.

Ninataka kujua majukumu yao ya kazi ni yapi hasa au ni mfumo tu wa kupeana ulaji baada ya kuwa nafasi za uwaziri zilizotengwa zinazidi idadi ya wanaostahili kupewa kwa mujibu wa mtoaji?.

Mkuu usiishie hapo tu, ni vyema tukaenda mbali zaidi; Endapo kila jimbo lina mbunge wake na kila wilaya ina mbunge wake;

  • Je kuna umuhimu gani wa rais kuwa na nafasi kumi za kuwateua washikaji zake kama wabunge?
  • Je kuna umuhimu gani wa kuwepo na viti maalum? wana mwakilisha nani?
 
Katika kupitia blog moja nimekutana na picha inayomuonesha Mh. Machano Othman Said ambaye ni Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum huko Zanzibar. Nakumbuka hata huku bara miaka ya nyuma waliwahi kuwepo

Wewe unaongea huyo wa nchi nyingine wakati hata kwenye nchi yako ya Tanganyika wapo! Kamuulize mh. Mwandosya atakutajia ni akina nani hao na wana majukumu yepi zaidi ya fadhila.
 
Sasa mbona jibu rahisi na wewe bhana?!hana wizara maalum kwa hiyo hana kazi maalum.yupo yupo tuu,idadi ya washkaji ilizidi idadi ya wateule,sasa ikabidi achomekwe tu hivyo hivyo bila kazi maalum,yaani mission town!
 
Kwa uingereza list ya mawaziri wasio na wizara kuanzia 1960's ni kama inavyoonekana hapa - Source Wikipedia



Ondoa hoja na majibu ya kipuuzi ; Huna tofauti na yule anayekwapua na kutapanya raslimali za Watanzania kwa madai ya kuwa katika nchi hii kila mtu ni fisadi.
 
Back
Top Bottom