"Utaratibu wa polisi wamshangaza Kagasheki
Na Lilian Lugakingira, Bukoba
NAIBU Waziri wa wizara ya Mambo ya Ndani, Khamis Kagasheki ameshangazwa na utaratibu unaotumiwa na jeshi la polisi wa askari kulazimika kumfuata mtuhumiwa nje ya mkoa kwa gharama zake kwa madai ya kudai baadaye.
Akizungumza na askari polisi, magereza na askari wa idara ya uhamiaji, Kagasheki alisema katika maisha yake hakujua kama kuna kitu cha namna hiyo.
Hoja hiyo ilitolewa kwake na askari kuwa wamekuwa
wakilazimika kulipa gharama zao wenyewe kwenda kufuata watuhumiwa nje ya mkoa kwa maelekezo kuwa watalipwa baadaye baada ya kuwasilisha risiti zao za madai.
Askari hao ambao walionyesha kukatishwa tamaa na kusononeshwa na utaratibu huo, walisema pamoja na wao kuamua kutekeleza hilo lakini fedha zao wanazotumia huchukua muda mrefu sana kuipata.
Walisema wanaambiwa kulete risiti au tiketi walizotumia katika safari hizo ambapo mbali na kulipa nauli yake mwenyewe, pia hutakiwa kumlipia hata mtuhumiwa anayemfuata.
Askari hao walimpasha Kagasheki kuwa wamekuwa wakifuatilia kulipwa fedha zao hizo na kubakia kuzungushwa tu.
Pia askari hao walisema bado wanakabiliwa na matatizo mbalimbali, likiwemo kutopatiwa vitambulisho vya kazi ambapo mmoja wao, Konstebo Augustino alisema tangu ameanza kazi miaka 14 iliyopita hadi sasa hajapatiwa kitambulisho.
Akijibu malalamiko yao, Kagasheki alisema kila kitengo kina mkubwa wake wa ngazi ya taifa na kuwataka askari hao kupeleka malalamiko yao kupitia kwa wakuu wao wa vitengo ili yashughulikiwe.
Alisema hivi sasa wametengeneza mapendekezo ambayo yatasaidia kuondoa matatizo mengine kama askari kutokuwa na bima ili kuondoa tofauti iliyopo baina ya majeshi.
Kutokana na malalamiko ya askari kuwafuata watuhumiwa kwa gharama zao nje ya mkoa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Abdallah Mssika aliwataka askari hao kuwasilisha risiti zao za madai katika ofisi yake na kuwa hadi leo wawe tayari wamewasilisha ili warudishiwe fedha zao.
SOURCE MWANANCHI;http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5843