Waziri Ashangaa Kuhusu Polisi!!!!!!

Manyiri

Member
Oct 27, 2007
80
15
"Utaratibu wa polisi wamshangaza Kagasheki
Na Lilian Lugakingira, Bukoba

NAIBU Waziri wa wizara ya Mambo ya Ndani, Khamis Kagasheki ameshangazwa na utaratibu unaotumiwa na jeshi la polisi wa askari kulazimika kumfuata mtuhumiwa nje ya mkoa kwa gharama zake kwa madai ya kudai baadaye.

Akizungumza na askari polisi, magereza na askari wa idara ya uhamiaji, Kagasheki alisema katika maisha yake hakujua kama kuna kitu cha namna hiyo.

Hoja hiyo ilitolewa kwake na askari kuwa wamekuwa

wakilazimika kulipa gharama zao wenyewe kwenda kufuata watuhumiwa nje ya mkoa kwa maelekezo kuwa watalipwa baadaye baada ya kuwasilisha risiti zao za madai.

Askari hao ambao walionyesha kukatishwa tamaa na kusononeshwa na utaratibu huo, walisema pamoja na wao kuamua kutekeleza hilo lakini fedha zao wanazotumia huchukua muda mrefu sana kuipata.

Walisema wanaambiwa kulete risiti au tiketi walizotumia katika safari hizo ambapo mbali na kulipa nauli yake mwenyewe, pia hutakiwa kumlipia hata mtuhumiwa anayemfuata.

Askari hao walimpasha Kagasheki kuwa wamekuwa wakifuatilia kulipwa fedha zao hizo na kubakia kuzungushwa tu.

Pia askari hao walisema bado wanakabiliwa na matatizo mbalimbali, likiwemo kutopatiwa vitambulisho vya kazi ambapo mmoja wao, Konstebo Augustino alisema tangu ameanza kazi miaka 14 iliyopita hadi sasa hajapatiwa kitambulisho.

Akijibu malalamiko yao, Kagasheki alisema kila kitengo kina mkubwa wake wa ngazi ya taifa na kuwataka askari hao kupeleka malalamiko yao kupitia kwa wakuu wao wa vitengo ili yashughulikiwe.

Alisema hivi sasa wametengeneza mapendekezo ambayo yatasaidia kuondoa matatizo mengine kama askari kutokuwa na bima ili kuondoa tofauti iliyopo baina ya majeshi.

Kutokana na malalamiko ya askari kuwafuata watuhumiwa kwa gharama zao nje ya mkoa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Abdallah Mssika aliwataka askari hao kuwasilisha risiti zao za madai katika ofisi yake na kuwa hadi leo wawe tayari wamewasilisha ili warudishiwe fedha zao.
SOURCE MWANANCHI;http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5843
 
Hii inaonyesha mambo matatu manne hivi.

1.Viongozi wetu wako out of touch na watu wa chini.

2.Viongozi wetu hawana information za kutosha kuhusu matatizo ya nchi yetu

3.Viongozi wetu wanapenda kusukumia matatizo katika system ya bureaucracy, mambo ya kutupiana mpira.

4.Au/na Viongozi wetu wanapenda kujifanya wanashangazwa na mambo ambayo wanayajua au walipaswa kuyajua.Kushangazwa huku kunakuwa potrayed kama vile iwe sababu ya kuwa excuse, kwamba ujinga ulikuwa unaendelea kwa sababu tu walikuwa hawajui.Uzembe ni kwamba hata kama walikuwa hawajui specific processes au incidents, wanafahamu the overall abject poverty nahopelessness inayo prevail, kwa hiyo they should not be surprised if the system produces shytty processes and products.

Kama huelewi matatizo ya watu obviously huwezi kuwa na solution ya matatizo hayo, usikubali kuongoza!

Mimi ninachoshangaa ni kwamba hii gimmick ya kushangaa inaonekana kufanya kazi.
 
Mara nyingi polisi(wapelelezi)ambao usafiri kwenda nje ya mkoa yao ya kikazi huwa hawalipi nauli toka mifukoni mwao, bali huwepo mfadhili ambae ameathirika na hiyo kesi, na polisi hao umfuata na kumweleza hali halisi na kudai kupewa nauli pamoja na gharama zingine wakati wote wa shughuli hiyo.

Utaratibu huu unajulikana mpaka kwa makamanda wao kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa, ndio maana kunakuwepo na ucheleweshaji wa kurudisha gharama hizo unless otherwise kamanda mkuu nae awe ameshirikishwa kuanzia mwanzo wa dili hiyo.

Jeshi la polisi kwa sasa linafanya kazi nzuri iwapo utakuwa na uwezo wa kuwagharamia mahitaji yao.
 
ndio pundit,hawa viongozi uchwara,na siku zote huwa wanatafuta kisingizo tu,ni kweli wanafahamu hizi habari,mie nakubaliana na point yako ya nne.we
kibunango,hakuna sheria kuwa mwenye kesi ndio ampe huduma polisi kama vile kumlipia nauli pindi itapohitajika kumfuata mtuhumiwa toka sehemu moja hadi nyingine.ni kweli madai ya hao polisi ni ya kweli lakini nao kwa upande mwingine ni wazushi,kuna wakati fulani nilikuwa nahitaji kumchukua mtuhumiwa wangu toka sehemu moja hadi nyingine lakini nikashangaa kusikia yule polisi aliyepewa ile kazi akinifuata na kuniambia nilipe gharama za kumfuata mtuhumiwa,nilipohoji zaidi ndio akadai ngoja niulizie vizuri,baada ya muda kidogo nkaona anaondoka peke yake,so here napata picha kuwa hawa viongozi wazushi na hao polisi ndio wale wale tu
 
we kibunango
,hakuna sheria kuwa mwenye kesi ndio ampe huduma polisi kama vile kumlipia nauli pindi itapohitajika kumfuata mtuhumiwa toka sehemu moja hadi nyingine.ni kweli madai ya hao polisi ni ya kweli lakini nao kwa upande mwingine ni wazushi,kuna wakati fulani nilikuwa nahitaji kumchukua mtuhumiwa wangu toka sehemu moja hadi nyingine lakini nikashangaa kusikia yule polisi aliyepewa ile kazi akinifuata na kuniambia nilipe gharama za kumfuata mtuhumiwa,nilipohoji zaidi ndio akadai ngoja niulizie vizuri,baada ya muda kidogo nkaona anaondoka peke yake,so here napata picha kuwa hawa viongozi wazushi na hao polisi ndio wale wale tu

Taadabu unapotaja jina la mtu, manake nami nikianza kutaja jina lako kwa jinsi ninavyotaka yatakuwa mengine hapa.

Nikirudi kwenye mada sijaandika kuwa kuna sheria ya kufanya hivyo, Zaidi hata wewe mwenyewe kadhia hiyo umewahi kukutana nao. Na sijui unashangaa nini hapo..!
 
Mara nyingi polisi(wapelelezi)ambao usafiri kwenda nje ya mkoa yao ya kikazi huwa hawalipi nauli toka mifukoni mwao, bali huwepo mfadhili ambae ameathirika na hiyo kesi, na polisi hao umfuata na kumweleza hali halisi na kudai kupewa nauli pamoja na gharama zingine wakati wote wa shughuli hiyo.

Utaratibu huu unajulikana mpaka kwa makamanda wao kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa, ndio maana kunakuwepo na ucheleweshaji wa kurudisha gharama hizo unless otherwise kamanda mkuu nae awe ameshirikishwa kuanzia mwanzo wa dili hiyo.

Jeshi la polisi kwa sasa linafanya kazi nzuri iwapo utakuwa na uwezo wa kuwagharamia mahitaji yao.

Sasa hii Jeshi la polisi kwa sasa linafanya kazi nzuri iwapo utakuwa na uwezo wa kuwagharamia mahitaji yao unamaanisha kama raia ndiyo watagharimia?

Kama kweli inatokea raia wanagharamia kama nilivyoelewa hapa hii ni open invitation to corruption.

Mimi nitakuwa nataka Polisi wamfuatilie mtuhumiwa, polisi wataniomba "nigharamie" nauli and what not, mie kwa sababu sijui issues nitakata kitu kidogo ili polisi aweze kutumia kwa nauli halafu kesho keshokutwa anaenda tena kuonyesha risiti na kuwa refunded hela.

What I have learned kutoka kwenye matatizo yetu ni kwamba, sehemu yeyote tunapoona matatizo kama haya, basi ujue huu ni moshi tu wa juu ambao unafuka na mwandishi wa habari akaona kuna a catchy headline hapa Waziri hajui issues zinaendaje, lakini kama tungekuwa na investigative journalism na open systems/ apractical freedom of information act basi tungeona uozo mkubwa zaidi ya huu unaobahatika kufika katika media. I am sure kama ningekuwa na access na polisi wenye uchungu wangeweza kueleza mambo mengi zaidi.
 
Hivi kuna kitu chochote tunachoweza kukifanya kwa ufanisi, wakati muafaka na kwa njia bora zaidi?
 
Hali ndio ipo hivyo na hasa katika Vituo vya Polisi Wilaya na Vituo vya Polisi Mkoa. Umeibiwa milioni tano, na Polisi wanajua kuwa una pesa na pengine umeshawaambia kuwa aliyekuibia kakimbilia mkoa fulani, basi lazima watakuchomoa tu ili kwenda kumtafuta huyo mtuhumiwa.

Ruhusa ya kutoka nje ya kituo cha kazi lazima itolewe na Mkuu wa Kituo, nae anajua ukata wa Kituo chake, hivyo kwa namna moja atajua tu kuwa safari ya polisi huyo inagharimiwa na mtu wa nje, ingawa yeye anaweza kudai kuwa anatumia fedha zake. Madai hayo ni njia ya kuja kujitengenezea pesa mara mbili zaidi pale atakaporudi na risiti zake. Kwa kuwa inajulikana na tokea kwa mkuu hadi kwa muhasibu ndio maana kunakuwepo na ucheleweshaji wa kulipa ikiwa ni namna ya kumshawishi polisi huyo kukata pande katika malipo hayo.
 
ndo nauliza je kama hali ndiyo hiyo unategemea polisi wanatoa wapi hizo pesa za kufuata watuhumiwa ikiwa mishahara yao haikizi mahitaji ya mwezi? moja kwa moja nadhani jibu ni rushwa huko ndo mizizi ya rushwa inajengwa na hao hao wakubwa wao wengi wao wakiwa wapenda rushwa ndo maana kwa polisi hata kupanda vyeo wanaangalia nani katoa nini? ndo maana utakuta kuanzia mkuu wa polisi na management yake kwa ngazi ya mkoa hadi wilaya ni darasa la saba wakati wale wa madarasa ya juu ya hapo ni watu wanaopigwa vita sana ili ikiwezekana waache kazi elimu duni waendelee kupeta . KUNA WILAYA UTAKUTA POLISI WALIOZAMU KITUONI WANAELIMU NDOGO SANA UKILINGANISHA NA WANAOLINDA BANK KISA RUSHWA!!! MIFANO HAI NINAYO NITAIMWAGA TARATIBU KADRI ITAKAVYOHITAJIKA!!!! HIYO NDO TANZANIA KAZI BADO NI KUBWA JAPO KWA JUU INAONEKANA SIYO KUBWA????!!!
 
Hii habari ya kuwa polisi wetu wengi wana elimu duni si kioja.Kwani Mawaziri wetu wengi pia hawana shahada za vyuo vikuu na wanaongoza watu ambao wana elimu kuliko wao. Pia Wabunge wetu wengine wamemaliza tu primary school.

Kwa ukweli sana tukio hili la kuwa polisi walipe kwanza na halafu ndio warudishiwe fedha zao lajulina na Mawaziri wote. Waziri ambaye ajifanya hajui hivyo basi huyu twamwiita ni mpumbavu nahafai kuwa Waziri tena.
Polisi wetu tunawadhalilisha sana tena sana kabisa. Wanakaa katika nyumba mbaya na mazingira mabaya kuliko Wanajeshi wetu. Nenda Dar es Salaam katika sehemu yoyote ile wanayokaa polisi na halafu nenda katika vituo vya majeshi yetu utaona jinsi hali ilivyo.
Njooni katika nchi ya EU uone mapolisi wanavyo ishi. Ndio maana huku hakuna rushwa nyingi ambazo zinawakabili mapolisi wa huku.
 
Ukweli ni kwamba wananchi ndio wanagharimia safari hizo na gharama zingine lukuki zitokanazo na safari hizo,nauli,chakula,malazi,pocket money na ghasia zote.
Polisi hukusanya tickets zinazolipiwa na rai kisha huziwasilisha vituoni kwa malipo.And its aracket vituoni inayowahusisha boss wa kituo na askari wanaopendelewa.
Ni utapeli mwingine askari wanapodai kutolipwa.
Ebu semeni kweli ni askari gani angetoka Dar kwa fedha yake akamtafute mtuhumiwa mathalani Kigoma,akalale siku lukuki akifanya upelelezi wa kumsaka akisha mpata amlipie nauli na chakula hadi Dar!!1
HAYA NI MACHOZI YA MAMBA!! A GIMMICK!
 
"Utaratibu wa polisi wamshangaza Kagasheki
Na Lilian Lugakingira, Bukoba

NAIBU Waziri wa wizara ya Mambo ya Ndani, Khamis Kagasheki ameshangazwa na utaratibu unaotumiwa na jeshi la polisi wa askari kulazimika kumfuata mtuhumiwa nje ya mkoa kwa gharama zake kwa madai ya kudai baadaye.

Akizungumza na askari polisi, magereza na askari wa idara ya uhamiaji, Kagasheki alisema katika maisha yake hakujua kama kuna kitu cha namna hiyo.

Hoja hiyo ilitolewa kwake na askari kuwa wamekuwa

wakilazimika kulipa gharama zao wenyewe kwenda kufuata watuhumiwa nje ya mkoa kwa maelekezo kuwa watalipwa baadaye baada ya kuwasilisha risiti zao za madai.

Askari hao ambao walionyesha kukatishwa tamaa na kusononeshwa na utaratibu huo, walisema pamoja na wao kuamua kutekeleza hilo lakini fedha zao wanazotumia huchukua muda mrefu sana kuipata.

Walisema wanaambiwa kulete risiti au tiketi walizotumia katika safari hizo ambapo mbali na kulipa nauli yake mwenyewe, pia hutakiwa kumlipia hata mtuhumiwa anayemfuata.

Askari hao walimpasha Kagasheki kuwa wamekuwa wakifuatilia kulipwa fedha zao hizo na kubakia kuzungushwa tu.

Pia askari hao walisema bado wanakabiliwa na matatizo mbalimbali, likiwemo kutopatiwa vitambulisho vya kazi ambapo mmoja wao, Konstebo Augustino alisema tangu ameanza kazi miaka 14 iliyopita hadi sasa hajapatiwa kitambulisho.

Akijibu malalamiko yao, Kagasheki alisema kila kitengo kina mkubwa wake wa ngazi ya taifa na kuwataka askari hao kupeleka malalamiko yao kupitia kwa wakuu wao wa vitengo ili yashughulikiwe.

Alisema hivi sasa wametengeneza mapendekezo ambayo yatasaidia kuondoa matatizo mengine kama askari kutokuwa na bima ili kuondoa tofauti iliyopo baina ya majeshi.

Kutokana na malalamiko ya askari kuwafuata watuhumiwa kwa gharama zao nje ya mkoa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Abdallah Mssika aliwataka askari hao kuwasilisha risiti zao za madai katika ofisi yake na kuwa hadi leo wawe tayari wamewasilisha ili warudishiwe fedha zao.
SOURCE MWANANCHI;http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5843

Mheshimiwa Kagasheki kweli hapa ka sheki sheki(read shake). Akiwa kama naibu waziri inakuwaje asilielewe hili jambo? Hizo hela wanazo zitoa huwa hazina maelezo ya kutosha au?

Hii ni hatari kwa Taifa na Usalama wa wananchi! Kwanini wao wanauliza watu vitambulisho pale wanapowakamata? Miaka 14 alikuwa askari wa kughushi basi. Toba!!

Hayo malalamiko yanahitaji Immidiate attention and not otherwise. Siyo kuanza na mapendekezo...haya ni manungu'niko yanayohitaji kazi ya haraka!

Na mie katika maisha yangu sikujua askari wanakuwa hawana vitambulisho...sasa hivi humu mtaani wakinikamata nitawauliza vitambulisho kwanza...manake hata kama haya...

Hivi huyu jamaa pichani si akanunue buti la mvua, aonyeshe risiti, arudishiwe hela. Naona Mheshimiwa hajaona hili nalo!:eek: Cheka kwa nguvu!

Hisani ya picha:Issamichuizi.blogspot.com
 
Last edited:
Ukweli ni kwamba wananchi ndio wanagharimia safari hizo na gharama zingine lukuki zitokanazo na safari hizo,nauli,chakula,malazi,pocket money na ghasia zote.
Polisi hukusanya tickets zinazolipiwa na rai kisha huziwasilisha vituoni kwa malipo.And its aracket vituoni inayowahusisha boss wa kituo na askari wanaopendelewa.
Ni utapeli mwingine askari wanapodai kutolipwa.
Ebu semeni kweli ni askari gani angetoka Dar kwa fedha yake akamtafute mtuhumiwa mathalani Kigoma,akalale siku lukuki akifanya upelelezi wa kumsaka akisha mpata amlipie nauli na chakula hadi Dar!!1
HAYA NI MACHOZI YA MAMBA!! A GIMMICK!

Well haya mazingira ya rushwa na malalamiko related sometimes yanashangaza sana. kwa sababu suala la police kukamata mtuhumiwa ambaye yupo nnje ya kituo chake cha kazi inabidi lifanyike kwa kufuata hierarchy ya utekelezaji. Hapa nina maanisha kwamba kituo cha police ambacho kipo karibu na mtuhumiwa husika, ndicho kinachotakiwa kumkamata mtuhumiwa, kwa kutuata utaratibu wa taarifa ambazo zimetolewa kwenye stakabadhi ya mashtaka ama inquiry na kumkadhi kwenye polize husika ambapo stakabadhi hiyo imeidhinishwa. Hivyo kumtoa askari sehemu moja kwenda kumkamata mtuhumiwa sehemu nyingine na mbaya zaidi kuuvuka mkoa, ni jitihada za dhahiri katika kutengeneza mwanya wa rushwa..Mawazo binafsi..
 
Back
Top Bottom