Waziri asema atahakikisha ongezeko la tozo kwenye miamala haliathiri mteja

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968

Waziri wa fedha Dk. Philip Mpango amesema watakuwa wanawabana makampuni ya simu ili wasije wakawaumiza wateja kwa tozo kubwa kutokana na ongezeko la kodi walilofanya kwenye bajeti hii na ushuru waliouweka sasa hivi utalipwa na kampuni ya simu na mabenki na sio mtumiaji wa huduma hilo litakaguliwa na TCRA, TRA na BOT
 
Nasikia hata gharama za miamala ya kwny simu imeshaongezwa kinyemela na makampuni ya simu tena kabla ya July
 
Wajinga wote wanaweza kuiamini taarifa hii. Kwenye sukari tulihakikishiwa na kila aliye na mamlaka kuanzia Taifani mpaka wilayani kuwa kilo moja itakuwa ahilingi 1,800. Kilichofuatia ni kupata sukari kwa bei ya juu kuliko wakati mwingine wowote. Inawezekana wananchi hatukuwaelewa viongozi wetu watukufu, huenda walimaanisha kuwa sasa bei itakuwa shilingi 1,800 zaidi ya ile ya awali.

Na kwenye hili sidhani kama anamaanisha mtumiaji wa huduma hizo za miamala hataongezewa gharama, bali gharama yake haitakuwa ya kuumiza. Kuumiza kunaanzia kiasi gani? Kuna anayejua?
 
watahakikisha lini sasa, wanakuja na mikakati ila hawajui watadhibiti vipi,
ni ni hapo sasa...... wangetuambia tumehakikisha....
 
Wajinga wote wanaweza kuiamini taarifa hii. Kwenye sukari tulihakikishiwa na kila aliye na mamlaka kuanzia Taifani mpaka wilayani kuwa kilo moja itakuwa ahilingi 1,800. Kilichofuatia ni kupata sukari kwa bei ya juu kuliko wakati mwingine wowote. Inawezekana wananchi hatukuwaelewa viongozi wetu watukufu, huenda walimaanisha kuwa sasa bei itakuwa shilingi 1,800 zaidi ya ile ya awali.

Na kwenye hili sidhani kama anamaanisha mtumiaji wa huduma hizo za miamala hataongezewa gharama, bali gharama yake haitakuwa ya kuumiza. Kuumiza kunaanzia kiasi gani? Kuna anayejua?
He Huko Nyie Mnapata Huku Kwetu Kwa Mang,,,,lazima Uende Na Barua Ya Mtendaji.Passport Size Mbili Na Wadhamin Wenye Mali Zisizohamishika Wawili Ili Uuziwe Sukari,,,,#chaikwamiwababy
 
hao mawaziri ni afadhari wasiwe wanaongea kabisa...maana wanaropoka tu vitu ambavyo havipo. leo wanasema hiki.. kesho kinatokea kile. alafu mbaya zaidi ni wasomi!!!! sasa kama wasomi wa TZ ndio wako hivi.. hao wananchi wao wakoje? we are doomed!!!!
 
Wairi wa fedha Dk. Philip Mpango amesema watakuwa wanawabana makampuni ya simu ili wasije wakawaumiza wateja kwa tozo kubwa kutokana na ongezeko la kodi walilofanya kwenye bajeti hii na ushuru waliouweka sasa hivi utalipwa na kampuni ya simu na mabenki na sio mtumiaji wa huduma hilo litakaguliwa na TCRA, TRA na BOT

Mkuu Dr Mpango utamdanganya nani ? Mmeshindwa sukari mpaka mmesababisha tunafuturu kwa mashaka ndio mtaweza simu ambazo hata thamani ya vocha tunazonunua haifahamiki bei yake ? Unanunua vocha dukani tsh 1000 , aliyekuuzia kanunua 950 , wakala kanunua kwa msambazaji tsh 900 , sasa bei ya vocha hii moja ni tsh ngapi hasa ?
 
Hivi kweli wanawaweza hawa jamaa?maana wamejipanga na wao. Unajua ni rahisi kinena kuliko kitunda. Hata sisi watumishi wa Mungu hupenda na ni mahodari wa kuhubiri but when it comes to reality we are the first ones to fail. Nod maana watu waliwahi kusema politics is a dirty game once you are in you will never be out.mwingine akasema before you join politics nenda kwanza kwenye Chou cha uongo. Ukipass you will be the best politician ever. But God is the only one who can change this. Let us keep on praying ill siku atatujibu kama alivyowajibu wana as Israeli pale alipompeleka Moses kuwakomboa K utoka utumwani
 
Wajinga wote wanaweza kuiamini taarifa hii. Kwenye sukari tulihakikishiwa na kila aliye na mamlaka kuanzia Taifani mpaka wilayani kuwa kilo moja itakuwa ahilingi 1,800. Kilichofuatia ni kupata sukari kwa bei ya juu kuliko wakati mwingine wowote. Inawezekana wananchi hatukuwaelewa viongozi wetu watukufu, huenda walimaanisha kuwa sasa bei itakuwa shilingi 1,800 zaidi ya ile ya awali.

Na kwenye hili sidhani kama anamaanisha mtumiaji wa huduma hizo za miamala hataongezewa gharama, bali gharama yake haitakuwa ya kuumiza. Kuumiza kunaanzia kiasi gani? Kuna anayejua?

mkuu wanaoamini uwongo huu ni wale mamba wa lumumba tu
 
Back
Top Bottom