Waziri Ardhi na maendeleo ya makazi, Upimaji Viwanja wa MKURABITA Uangaziwe jicho sasa

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,032
3,478
Wakuu,

Hili ni bandiko la manung'uniko kuhusu Mkurabita upimaji viwanja na mchakato wa kupata hati.

Wananchi wengi waliojengwa au kuuziwa viwanja kwenye maeneo ambayo yalikuwa bado kupimwa na serikali wanalalamika, wengine wamelipia ada ya shilingi 310,000/= tangu 2016, 2017 hadi leo hakuna hato zozote zilizotolewa na mamlaka husika mfano mzuri ni baadhi ya maeneo DSM, Mwanza, Tanga, Lindi, Morogoro manispaa kata ya Kihonda, Mkundi nk hadi watu wamekata tamaa na viongozi waliosimamia zoezi hilo hata simu hawapokei na akipatikana majibu yake ni karaha sana.

Tafadhali mheshimwa waziri WILLIAM LUKUVI baada ya kuapishwa shughulikia hii kero ili kila aliyelipia kama alivyotakiwa, akapimiwa, akawekewa mawe apatiwe hati yake stahiki.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom