Waziri apokewa na mgogoro mzito TRL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri apokewa na mgogoro mzito TRL

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 17, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,507
  Trophy Points: 280
  Waziri apokewa na mgogoro mzito TRL


  Na Rehema Mohamed.

  WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wamemtaka Waziri wa Miundombinu Bw. Omary Nundu kutoa ufafanuzi kuhusu Menejimenti ya Kampuni ya RITES ya India kuendelea kufanya kazi na kukusanya mamilioni ya fedha zinazotokana
  na mapato ya shirika hilo ikiwa tayari imeshavunja mkataba wake na Serikali.
  Wafanyakazi hao wametaka, Bw. Nundu kwenda kuwapa ufafanuzi wa suala hilo Jumatatu ijayo na kuwaeleza hatma ya mafao yao (mkono wa kheri) kutokana na shirika hilo kubadilishwa kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kuwa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).
  Hoja hizo za wafanyakazi hao zilitolewa Dar es Salaam jana wakati wa kikao chao cha dharura kilichoitishwa na wafanyakazi hao na kumtaka Katibu wao wa Chama cha Wafanyakazi, Bw. Sylvester Rwegasira kutolea ufafanuzi masula hayo.
  Wafanyakazi hao wakiwa na mabango yaliyoandikwa ‘Nini siri ya serikali na Wahindi?’ Kwanyakati tofauti walisema TRL sasa imekuwa kama Ivory Coast kutokana na kuongozwa na menejimenti mbili tofauti ikiwemo iliyoteuliwa na Serikali chini ya Mkurugenzi wake, Bw. Amani Kisamfu na ile ya wawekezaji kutoka nchini India.
  “Tunataka kujua mmiliki wa TRL ni nani, Serikali au Watanzania? Tunashangaa kuona menejimenti ya Wahindi ikiendelea kukaa ofisini bila kazi yoyote ya msingi huku wakiendelea kukusanya fedha bure kwasababu hata mishahara inalipwa na Serikali,” ni moja ya malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wafanyakazi hao.
  “Tunataka Jumatatu tusiwaone, Waziri akija aje na menejimenti ya waswahili, sisi Mhindi sio mwajiri wetu alipoteza uwajiri wake tangu aliposhindwa kutulipa mishahara yetu, “alilalamika mmoja wa wafanyakazi hao.
  Akijibu hoja hizo, Bw. Rwegasira alisema hata yeye akiwa kama Katibu Mkuu wa TRAWU, hana taarifa yoyote kuhusu mustakabali wa Serikali kuhusu madai hayo ingawa Serikali ilitoa ahadi kuwa uongozi huo wa Wahindi ungeondoka wiki chache baada ya kuvunjika kwa mkataba.
  Bw. Rwegasira alisema baada ya Serikali kuvunja mkataba na TRL Oktoba mwaka huu, nakala ya kuvunjika kwa mkataba huo ilitakiwa kufikishwa mbele ya Baraza la Mawaziri ili kuanza kufanyiwa kazi na hatimaye wahindi hao kuondoka rasmi.
  Bw. Rwegasira, alisema kinyume na matarajio hadi sasa kumekuwa kimya hawana taarifa yoyote kama nakala hiyo ilifikishwa katika Baraza hilo au la!
  “Mimi sina jibu, shirika ndio linakufa, tangu menejimenti ya Wahindi iamuriwe kuondoka hawana kazi ya kufanya, cha kushangaza fedha wanachukua na Serikali imekaa kimya, kwanini serikali ipo kimya?,”alihoji Bw. Rwegasira
  B w. R w e g a s i r a a l i s e m a ingekuwa busara baada ya Serikali kuvunja mkataba wake na TRL, menejimenti ya Wahindi hao ingekaa pembeni na kuwachiwa wazalendo kuiongoza.
  Katika hatua nyingine alisema hali ya usafirishaji wa abiria ni mbaya kutokana na shirika hilo kuwa na uwezo mdogo kiute
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,507
  Trophy Points: 280
  Hivi serikali hiki kigugumizi cha kuwaondoa hawa wahindi kinasababishwa na nini?
   
Loading...