Waziri aomba uume wa Mwalimu usifanye kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri aomba uume wa Mwalimu usifanye kazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mponjoli, Aug 11, 2009.

 1. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Sumbawanga  NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza amewataka wananchi wa kijiji cha Muze wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa kumuombea dua mbaya aliyekuwa mwalimu wa shule ya sekondari Mazoka aliyempa mimba mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo.

  Mahiza alisema taarifa ya shule ilimsikitisha na baadhi ya matatizo yaliyoainishwa yatashughulikiwa na serikali.

  " Na hili la huyu bazazi, aliyemkatisha masomo mwanafunzi ni lazima tumuombee dua ili asisimame daima,uume wake uache kufanya kazi" alisema.

  Alisema mwalimu ndiye kioo cha jamii, lakini mwalimu anapomkatisha masomo mwanafunzi ni lazima achukuliwe hatua kali za kisheria na kinidhamu na kwamba kwa vile alitoroka dua limfuate huko aliko.

  Awali akitoa taarifa ya shule hiyo mkuu wa shule hiyo Anicent Mpemba alisema katika kipindi cha miaka mitatu hadi hivi sasa wanafunzi wanne wa kike walikatishwa masomo yao kutokana na ujauzito.

  Hata hivyo wanaume watatu walikamatwa kwa tuhuma za kutunga mimba hizo, lakini mwanaume wa nne alitoroka.
  Mpemba alisema mwalimu huyo baada ya kupatikana na hatia alifanikiwa kutoroka kabla ya kukamatwa na juhudi za kumtafuta bado zinaendelea kwa lengo la kumfikisha katika vyombo vya sheria.
   
 2. N

  Nangetwa Senior Member

  #2
  Aug 11, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nafikiri waziri hapo kavuka mipaka ya maneno. akisema hivyo kama waziri je watu wadogo si watasema tukate kabisa huo uume.
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mbona mawaziri wengi tu wa serikali wanatembea na Wanafunzi..mbona Mahiza hawaongelei hawa??
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Aug 11, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Badala ya kusugua kichwa ili kutafuta namna ya kumaliza ubazazi huu yeye anaaza adhabu za kinadharia (labda akisomewa albadili). Ndio mawaziri wetu hawa tutafanyaje!!
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahaha unajua kwa nini walimu wanafanya hivyo?
  Hakuna malupulupu na malupulupu yao ni kumega wanafunzi tatizo hapa aongeze mishahara kwa walimu wataacha kumega wanafunzi na kutoka na maduu kama wewe.
   
 6. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Huyu waziri anashangaza. Anafikiri ugonjwa uko kwenye uume! Ugonjwa uko kwenye mkichwani: kwenye fikra, mtazamo, nk. Huko ndiko kwa kufanyia kazi kwani huko ndiko chanzo cha ubazazi wote huo na si hicho kiungo kizuri kilichoumbwa na Mungu.

  Kumbe mwalimu yule na wengine wa tabia kama yake wanapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Lakini pia wanapaswa kusaidiwa ili kutambua nafasi yao katika jamii kwamba wao ni walezi wa watoto wao na watoto wa wengine waliokabidhiwa kwao. Wajiheshimu na kuwaheshimu watoto wa wenzao.
   
 7. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Huyu waziri mropokaji sana,sijui JK kamtoa wapi
   
 8. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #8
  Aug 11, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  ....... Kama ni suala la mishahara sidhani kama ni walimu peke yao wanaopata mishahara midogo na wala sidhani kama suala la mishahara linaendana na kutembea na watoto wa shule mbona kuna mapedejee wenye mapesa yao lukuki na bado wanasalandia watoto wa shule?

  Maduu kama mimi??
   
 9. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ile semina elekezi naona haikufanya kazi.........tatizo ni kuweka vihiyo kwenye nafasi muhimu katika uendeshaji wa nchi. Hivi unatagemea mtu kama huyu akipanda na kuwa waziri...atazungumza nini ndani ya baraza la mawaziri? si atabaki kunywa maji tu na kupiga makofi..!
   
 10. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ushemeji na fadhila style in action..
   
 11. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Ninakubaliana na wewe kiasi fulani lakini tatizo la hawa wanafunzi nao wanaendekeza tamaa na starehe na ndiyo maana wanamegwa.Hata mimi kuna wanafunzi wananisumbua utasikia naomba voucher(muda wa maongezi) kwaajili ya mobilephones,.....etc.Sasa kwa mpango huu unategemea nini?Anyway, bora niungane na mwanajamiione ili kuepukana na hawa wasumbufu;kama uko tayari nijulishe.
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahaha nilisahau wewe ni mama sio mrembo kwi kwi kwi nilijua bado mnyange.
  Waziri mwenye jinsia yako amekurupuka na kuropoka na kila siku mnalilia usawa katika uongozi sasa tutawapaje kama mnachemka hivi?
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nani anapaswa kulaumiwa mwanafunzi au mzazi maana wengine wanamegwa kwa kununuliwa chipsi kuku na soda wale wengine wanamegwa kwa kununuliwa mihogo wengine nauli{makonda} wengine lifti duhh.
   
 14. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mawaziri na watendaji wengi ( ambao ni presidential appointees) wamewekwa si kwa maendeleo ya nchi bali wamewekwa ili waitafune nchi vizuri kutokana na urafiki katika nyanja mbalimbali za JK. Shida tuou TZ. MUNGU ni mwema tuzidi kuiombea nchi yetu.
   
 15. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ndiyo maana amewekwa hapo eti, hawatakiwi ma-challengers karibu karibu!
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mpwa kuna nafasi za kazi majuu zimetangazwa hapa JF Yo Yo yuko busy anatafutia mashori wake....usije sema sijakutonya!
   
 17. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Sasa inabidi wana JF iundwe thread ya kutoa ushauri kwa viongozi wa serikali maana naona huenda mawazo mengi huishia humu humu jamvini wakati Waziri kama huyu angeliweza kwanza kuomba na kupata ushauri kabla ya kubwabwaja namna hiyo! Lol!
   
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Cha ajabu ni kwamba anaweza kuendelea kuwa waziri pamoja na kuonesha hata uwezo mdogo wa kuongea. Sheria iko wazi kuhusu jambo kama hilo, sijui kwa nini tuanze kumsumbua mungu wakati sheria zetu zipo, au ndio janja ya kutumia weakness ya watanzania kuwa waumini sana na kuwazuga kupitia dini.
   
 19. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mimi nashauri mwanaume yeyote akibaka au akizini na mwanafunzi hata kama ni kwa ridhaa ya mwanafunzi basi afungwe maisha ili kwanza kupunguza wahalifu wa jinsi hii na pili kuwafanya wajutie kitendo hicho kwa maisha yao yote na iwe fundisho kwa wazinzi wengine.
   
 20. F

  Froida JF-Expert Member

  #20
  Aug 11, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Waalimu wanaume wamechukulia shida za wanafunzi kama mtaji wa kuwaharibu wasichana kwa kuwakatisha masomo,adhabu ipo chini ya sheria ya SOSPA lakini inatumika kwa waangapi kwa sababu wazazi wakati mwingine wanakubaliana na mwalimu kisiri mambo huwa yanaishia kimya kimya,jamii nayo ishiriki kukemea mambo hayo.
  Sasa waziri anaweza kututhibitishia kama kweli tukiomba dua huyo mwalimu uume hautasimama au itakuwa dua la kuku halimpati mwewe,waziri kadata kweli
   
Loading...