Waziri Angela Kairuki atofautiana kauli na Katibu Mkuu Utumishi Dr. Ndumbaro

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,645
Serikali yawakana walioajiriwa mei mosi nukuu kutoka gazeti la Mwananchi, Dr. Ndumbaro akihojiwa na gazeti la Mwananchi amesema mikataba waliopewa ni batili.

Gazeti hilo hilo na,muandishi yule yule akamhoji Angela Kairuki
nanukuu "waziri wa ofisi ya rais ,menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora ANGELA KAIRUKI Aalifanua ''hakuna mtumishi mpya wa umma ambaye ameingizwa kwenye payrol,KAMA WALIPANGIWA VITUO NA HAWAJAINGIZWA KWENYE PAYRoll wasubiri maelekezo "alisema Kairuki

Sasa Dr. Ndumbaro anasema walipewa mikataba batili,Angela Kairuki anasema kama walipangiwa vituo na hawajaingizwa kwenye payroll wasubiri maelekezo.

Ukweli ni huu
Hawa vijana wote walipangiwa vituo vya kazi,walipewa pesa za nauli na kujikimu,waliripoti kwenye vituo vya kazi,walipewa vitambulisho lakini hawakuingizwa kwenye payroll. Je, ubatili wao upo wapi?

Ombi: Kairuki tolea tamko jambo ili linawachanganya vijana.
 
usishangae mkuu ndio Tanzania ya Magufuli hii
ni maajabu gazeti la mwananchi dr ndumbaro anasema batiri mhandishi uyo uyo mmoja ana mhoji kairuki anasema kama wamepangiwa vituo vya kazi na hawajaingizwa kwenye payroll wasubiri maelekezo wapi hawa batiri au kuna wengine
 
Mwanza wakuu wa wilaya, mkoa, waziri walitofautiana na rais kuhusu kuwaondoa wamachinga na hakuna aliyewajibika. Hata hapa ni hayo hayo, wakuu wawili wizara moja nyeti wanatofautiana mambo ya msingi huku tukitarajia viwanda!
 
Wamewatesa hawa vijana kitenɗo walicho wafanyia ni ukiukwaji wa taratibu za utumishi wa umma
 
Wamewatesa hawa vijana kitenɗo walicho wafanyia ni ukiukwaji wa taratibu za utumishi wa umma
sasa kauri ya dr ndumbaro kusema walipewa mikataba batiri ivi inaingia akilini wizara zaidi ya sita,utumishi wa mahakama,kilimo,duce,udsm na idara zingine za serikali kuwapa mikataba batiri
 
sasa kauri ya dr ndumbaro kusema walipewa mikataba batiri ivi inaingia akilini wizara zaidi ya sita,utumishi wa mahakama,kilimo,duce,udsm na idara zingine za serikali kuwapa mikataba batiri
Haingi akilini kabisa,huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu na utumishi wa umma...raia wananyanyasika ktk nchi yao na serikali yao
 
ni maajabu gazeti la mwananchi dr ndumbaro anasema batiri mhandishi uyo uyo mmoja ana mhoji kairuki anasema kama wamepangiwa vituo vya kazi na hawajaingizwa kwenye payroll wasubiri maelekezo wapi hawa batiri au kuna wengine

Mkuu jitahidi kuandika kiswahili kilichonyoka:
uyo = huyo
mhandishi = mwandishi
batiri = batili
 
Vijana Hao Ni Hovyo Kabisa. Wameshindwa Kujiajiri? Mbona Bibi Zao Vijijini Hawajawahi Kuomba Ajira Na Hawajawahi Kuwaza Kuhusu Ajira? Ningekuwa Rais Ningewatia Ndani Wote
 
Ajira! Ajira! Ajira! Hizi Kelele Zimetuchosha. Vijana Mkimaliza Masomo Mkajiajiri. Siyo Kila Siku Angela, Angela Au Ndumbaro, Ndumbaro. Hee! Mkalime.
 
Back
Top Bottom