Waziri anayesinzia bungeni kuliko wote kuiokoa c.c.m? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri anayesinzia bungeni kuliko wote kuiokoa c.c.m?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SILENT ACtOR, Oct 27, 2011.

 1. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Hebu wasikie CCM wanavyoendekeza utani. Baada ya vigogo kama Kikwete, Mukama, Kingunge kushindwa kuleta muafaka kati ya makundi yanayohasimiana ccm, sasa Wassira naye kachukua jukumu la kuleta suluhu. Je, huyu jamaa wa kulala ataweza kazi hii? Soma habari hii;
  -CCM wahaha kujinusuru-wASSIRA AJIFUNGIA ARUSHA KUSAKATA SULUHU, YUMO PIA SHIGELLA WA UVCCM.
  Peter Saramba,
  Arusha-Mwananchi

  MSUGUANO wa kisiasa ndani ya CCM ambao umekitikisa chama hicho siku chache zilizopita umechukua sura mpya, na sasa chama hicho kinamtumia kada wake mkongwe, Steven Wassira kuanza harakati za kutatua mgogoro huo.Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), yupo Arusha ambako jana alianza mchakato wa vikao vinavyowashirikisha viongozi na baadhi ya makada wa chama hicho wa Wilaya na Mkoa wa Arusha, eneo ambalo limekuwa kitovu cha vurugu zinazoonekana kukitikisa CCM hadi ngazi ya taifa.
  Tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka jana, CCM Arusha kimegeuka kuwa kitovu cha vurugu na mpasuko unaotikisa chama hicho na Umoja wake wa Vijana (UVCCM). Wassira ambaye ni mlezi wa CCM Mkoa wa Arusha, alifanya kikao na UVCCM mkoani humo ambacho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Martin Shigella. Vyanzo vya habari vilidokeza kwamba, katika siku yake ya kwanza ya ziara mkoani hapa, Wassira jana alikutana na UVCCM Wilaya ya Arusha ikiwa ni mwanzo wa safari hiyo ya kusaka suluhu. Wassira aliyewasili Arusha juzi, katika kikao chake hicho alikutana na wajumbe wa Baraza la Vijana la Wilaya ya Arusha katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Youth League eneo la Faya, ambako vijana hao walimtaka kutumia nafasi yake ya ulezi na uwaziri kukutana na pande zote zinazonyukana kutafuta ufumbuzi kabla mambo hayajaharibika zaidi.
  Pamoja na kujadili mgogoro ulioko kati ya makundi ya vijana ambao uongozi wake wilayani Arusha chini ya Godfrey Mwalusamba unadai unachochewa na mwenyekiti aliyepita, Ally Bananga, kikao hicho pia kilijadili ziara ya Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Benno Malisa iliyopingwa na kususiwa uongozi wa Mwalusamba.Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinadai kuwa, Wassira alielezwa na vijana hao wakiongozwa na mmoja wa wajumbe aliyetajwa kwa jina la Mussa Daudi Lungo kwamba tatizo la UVCCM na chama hicho kwa ujumla ni harakati za urais 2015 zinazohusisha baadhi ya makada, viongozi na wanachama. Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, zaidi ya nusu ya wajumbe wa kikao hicho walimuunga mkono Mwalusamba katika kila hoja aliyotoa.
  Kauli ya Wassira: Akihitimisha kikao hicho, Wassira aliahidi kuchukua maelezo yatakayotolewa na pande zote kwa ahadi kwamba atayawasilisha kwenye Kamati Kuu (CC) ya CCM inayotarajiwa kukutana siku chache zijazo. Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alithibitisha ujio wa Wassira na kwamba ziara hiyo ni ya kawaida katika kuimarisha chama na kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi. Chatanda aliyezungumza kwa simu jana jioni, alisema Wassira alitarajiwa kukutana na kamati ya siasa ya wilaya hiyo kabla ya leo asubuhi kukutana na wajumbe wa baraza la vijana mkoa na kuhitimisha kwa kukutana na wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa mchana. "Kama mjumbe wa NEC (Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM) na mlezi wa chama mkoa, atafanya (Wassira) vikao na ngazi mbalimbali ya uongozi wa chama na jumuiya zake na kwa sababu hii ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe kuwa mlezi wetu, tutampa taarifa ya hali ya mkoa kisiasa," alisema Chatanda.
  Ingawa Chatanda hakutaka kuzungumzia kwa undani maudhui ya ziara hiyo iliyokuja kukiwa na fukuto na minyukano kati ya makundi yanayodaiwa kuchochewa na harakati za urais 2015, moja kati ya ajenda muhimu ya vikao vya waziri huyo ni kutafuta chanzo, sababu na ufumbuzi wa migogoro ya mara kwa mara miongoni mwa viongozi na wana CCM Arusha. Migogoro ilikoanzia. Katika siku za karibuni, Arusha imegeuka kuwa chimbuko la vita ya maneno miongoni mwa makada wa CCM, hulka ambayo imesambaa hadi kwa viongozi wa kitaifa wa chama hicho. Tuhuma za hivi karibuni ni zile zinazomtaja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwamba amekuwa akikivuruga chama hicho kutokana na jinsi anavyopigia chapuo utekelezaji wa falsafa ya kujivua gamba.Wanaopinga falsafa hiyo wanasema inatumika vibaya kuwabana watu wenye nia ya kuwania urais wa 2015 lakini Nape mara kadhaa amekanusha kutokuwa na lengo hilo.
  Awali, mgogoro ulikuwa baina ya baadhi ya vijana wilaya na mkoa wa Arusha na katibu wa CCM Mkoa, Chatanda ambaye pamoja na viongozi na makada wengine walituhumiwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kusababisha chama hicho kipoteze kiti cha ubunge wa Arusha Mjini. Katikati ya mwaka huu baada ya kikao cha NEC, mkoa huo ulitoa onyo kali kwa baadhi ya vijana waliohusishwa na mvutano huo, akiwamo Mwenyekiti wa Vijana Mkoa, James Ole Millya aliyedaiwa kumtolea Chatanda maneno makali.
  Wakati hali ikionekana kutulia, mgogoro mwingine mpya umeibuka mwezi huu na safari hii ukitanuka hadi kuhusisha viongozi wa UVCCM Taifa akiwamo Malisa, baada polisi kuwanyima kibali kufungua matawi na kufanya mikutano ya hadhara. Hata hivyo, vijana hao walikaidi amri ya polisi na kuendelea na ratiba yao ambayo ilihitimishwa kwa mkutano wa hadhara ambao waliutumia kumtuhumu mtu waliyemwita mtoto wa kigogo wa chama na Serikali kwamba ndiye alitoa maelekezo ya wao kunyimwa kibali cha polisi. Siku chache baadaye, polisi walitangaza kumsaka Ole Millya ili wamhoji juu ya tuhuma hizo lakini tangu alipojisalimisha, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na jeshi hilo kuhusiana na mahojiano hayo. Wakati polisi wakiwa kimya, Ole Millya alitoa taarifa ndefu yenye kurasa 12 ambayo pamoja na mambo mengine, alirejea na kusisitiza kuwa wapo watoto wa vigogo wa chama na Serikali wanaotumia madaraka ya wazazi wao kuvuruga UVCCM na kuingilia baadhi ya utendaji serikalini.
   
 2. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hii story mbona haisomeki edit mkuu dah !!
   
Loading...