Waziri anayehusika, anipe majibu ya maswali haya

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
1. Kwanini Mbunge alipwe mshahara wa zaidi ya 11,000,000/= kwa mwezi na Mtumishi mwingine wa Serikali alipwe chini ya sh.500,000/?

2. Kwanini Wabunge walipwe posho ya kila kikao zaidi ya sh.300,000/= kwa siku na watumishi wengine wa Serikali walipwe chini ya sh.50,000/= au hata chini ya 30,000/=?

3. Kwanini baadhi ya Viongozi wa umma(Wakuu wa mikoa, Wilaya nk) wapewe fedha za kujikimu kila mwezi, yaani Chakula nk. wakati watumishi wengine hawapewi?

4. Je, Wananchi wengine wanafaidi nini kutokana na utajiri wa Nchi yao?

Tanzania siyo maskini. Isipokuwa, utajiri wa Nchi hii unachukuliwa na kikundi kidogo kabisa cha watu wenye nafasi zao huko juu.

Watanzania tunataka umeme, maji, afya, Elimu, miundombinu bora.

Hatuhitaji tena longolongo. Tunahitaji huduma bora za jamii na mgawanyo sawa wa KEKI ya Taifa.

Tukiamua, inawezekana kabisa.
 
Kwanini Kuna mfuko wa Jimbo ambapo pesa anapewa Mbunge? Mbunge anasimamia mradi gani Jimboni mpaka apewe pesa ya Jimbo na wakati huohuo kuna Bajeti ya TAMISEMI ambayo imetengwa kuendesha shughuli za serikali Mikoani na Wilayani!!!
 
Pia kwa nini kuna wabunge wasiokuwa na majimbo? Wanamuwakilisha nani ikiwa kazi ya ubunge ni ya uwakilishi?

Kwa ufupi bunge ni miongoni mwa biashara kichaa. Tunawekeza pesa nyingi sana lakini matokeo hafifu.

Kuna wakati sioni kabisa haja ya kuwa na bunge. Mawaziri wapatiwe ajira, waombe kazi kulingana na sifa, iwe kama wakurugenzi wenye mishahara ya kawaida.

Kuhusu sheria, tunaweza kuwa na tume au Chombo kilichobobea wataalam wanasheria na sekta zingine watakua na hilo jukumu la kusimamia mchakato wa kupitisha miswaada na mabadiliko yote ya sheria, zikiwepi za madini na uwekezaji.

Wananchi Wana madiwani, wenyeviti, wakuu wa wilaya, mikoa, wakurugenzi n.k wanatosha sana kutekeleza mipango ya maendeleo na kusikiliza hoja na maoni ya wananchi, tena wao wako na hao wananchi huko huko tofauti na wabunge ambao wengine hawaonekani hata majimboni kwao.
 
Kumlipa mbunge mshahara hiyo tayari ni hongo, maana mbunge siyo mwajiriwa........yeye anatakiwa achangiwe pesa na wapiga kura wake za kumwezesha kuwawakilisha huko bungeni, lakini sababu sirikali inajua nini inafanya ili ipitishe mambo yake kwa ndiooooooooooooo basi hili linabaki kama lilivyo.
 
Kwa ufupi bungee ni miongoni mwa biashara kichaa. Tunawekeza pesa nyingi sana lakini matokeo hafifu sana.

Kuna wakati sioni kabisa haja ya kuwa na bungee. Mawaziri wapatiwe ajira, waombe kazi kulingana na sifa, iwe kama wakurugenzi wenye mishahara ya kawaida.

Kuhusu sheria, tunaweza kuwa na time au Chombo kilichobibea wataalam wanasheria na sekta zingine watakua Hilo jukumu la kusimamia mchakato wa kupitisha miswaada na mabadiliko yote ya sheria.

Wananchi Wana madiwani, wenyeviti, wakuu wa wilaya, mikoa, wakurugenzi n.k wanatosha sana kutekeleza mipango ya maendeleo na kusikiliza hoja na maoni ya wananchi, Tena wao wako na hao wananchi huko huko tofauti na wabunge ambao wengine hawaonekani hata majimboni kwao.
Kabisaa. Hapo umenena vyema.
 
Milioni 11 inamaana kwa siku anatakiwa atumie zaidi ya laki tatu.
Kwa huyu wa 500,000 kwa siku anatakiwa atumie elfu 15. Yeye pamoja na mkewe na watoto wake watatu. Ina maana yeye binafsi anatakiwa atumie 3,000 kwa siku.
Halafu mnasema Dar Kuna joto. Joto analoona huyu Charlie wa 500,000 sio la kawaida.
Kumbuka kwa Sasa ndoo ya maji Dar Ni 200 mpaka 500.
 
1. Kwanini Mbunge alipwe mshahara wa zaidi ya 11,000,000/= kwa mwezi na Mtumishi mwingine wa Serikali alipwe chini ya sh.500,000/?

2. Kwanini Wabunge walipwe posho ya kila kikao zaidi ya sh.300,000/= kwa siku na watumishi wengine wa Serikali walipwe chini ya sh.50,000/= au hata chini ya 30,000/=?

3. Kwanini baadhi ya Viongozi wa umma(Wakuu wa mikoa, Wilaya nk) wapewe fedha za kujikimu kila mwezi, yaani Chakula nk. wakati watumishi wengine hawapewi?

4. Je, Wananchi wengine wanafaidi nini kutokana na utajiri wa Nchi yao?

Tanzania siyo maskini. Isipokuwa, utajiri wa Nchi hii unachukuliwa na kikundi kidogo kabisa cha watu wenye nafasi zao huko juu.

Watanzania tunataka umeme, maji, afya, Elimu, miundombinu bora.

Hatuhitaji tena longolongo. Tunahitaji huduma bora za jamii na mgawanyo sawa wa KEKI ya Taifa.

Tukiamua, inawezekana kabisa.
Wakatwe posho wabunge wanapunja watumishi wengine.Hawalipi kodi,
 
Back
Top Bottom