Waziri anawezaje kuchelewesha mafao ya wastaafu?

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
10,526
13,013
Wandugu.

Inawezekana mm ndiyo sijaelewa.

Raisi wa JMT leo alikuwa chuo cha mapolisi kurasini. Hapo alizindua majengo mengi. Kama kawaida.

Awali kabla ya kuanza kuhutubia alitangulia means CCM mwenziwe naye ni bwana Simon Siro. Siro aliongea changamoto nyingi zinazowakabili mapolisi wakiwemo wale waliostaafu. Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kucheleweshwa kwa mafao ya wastaafu. Siyo Polisi tu wanaocheleweshewa mafao yao ni karibu wastaafu wote na kote. Sababu zinajulikana, na zishajadiliwa hapa mara nyingi.

Jambo hilo liletwa kwa raisi kama changamoto ya wizara kwa serikali.

Alipopewa nafasi ya kuzungumza RAIS hakuwa na la maana la kuzungumza juu ya hili. Alimtupia lawama wazir na kumwambia aende wizarani akapige kelele! Yawezekana mkuu ana amini kwenye kufika kuliko sheria na taratibu.

Sasa nimejikuta sielewi, hivi wazir ndiyo mwenye mamlaka ya kulipa mafao ya watumishi mafao yao au ni mifuko waliokuwa wanachangia? Yaani mtu afanye kazi kwa miaka 55-60 kisha kulipwa haki yake iwe hadi waziri apige mayowe?

Kwanini rais hajaagiza wwlipwe moja kwa moja na wizara kama afanyavyo kwa wanyonge wengine? Tena hawa ni wanyonge waliosaidia ushindi kwenye uchaguzi.

Alihitimisha kwa kuwashukuru polisi kwa kuleta amani nchini? Nilidhani angewashukuru kwa ushindi wa kishindo hapo mwaka jana.
Alienda mbali kwa kuagiza ikijengwe kituo cha afya. Lakini pale kuna zahanati ya barracks tayari.

Raisi lipa watumishi wote wastaafu mafao yao wakapumzike acha ngonjera. Lipa stahiki za walio kazini acha ngonjera.

MADARAJA HAYANA MAANA KWA WASTAAFU.

ASANTE
 
Back
Top Bottom