Waziri anaposhiriki kwenye kampeni, je ni sawa?

nrango

Senior Member
Jun 6, 2011
102
24
Nimefuatilia kampeni za uchaguzi mdogo Igunga, mi sidhani kama ni sahihi kwa viongozi kama mawaziri kushiriki kampeni, sababu waziri ni wa watanzania wote bila kujali vyama, nimewaona Wasira, Magufuli n.k

Wadau mnasemaje..
 
Nimefuatilia kampeni za uchaguzi mdogo igunga,mi sidhani kama ni sahihi kwa viongozi kama mawaziri kushiriki kampeni,sababu waziri ni wa watanzania wote bila kujali vyama.Nimewaona Wasira,Magufuli n.k.Wadau mnasemaje..
Jibu utakalopewa ni kuwa Wamekuja kwa nyadhifa za kichama, na si kama mawaziri!
Japo Swali linabaki palepale kuwa ofisi zao wamemwachia nani, au wako likizo?
 
Anashiriki RAIS aliyechaguliwa na WATANZANIA wote itakuwa waziri ambaye kateuliwa na mtu mmoja tu!
 
Nimefuatilia kampeni za uchaguzi mdogo igunga,mi sidhani kama ni sahihi kwa viongozi kama mawaziri kushiriki kampeni,sababu waziri ni wa watanzania wote bila kujali vyama.Nimewaona Wasira,Magufuli n.k.Wadau mnasemaje..
Ndio maana tunataka katiba mpya ambayo tutaka mawaziri wasiwe wabunge na pia tuwe na idadi kamili iliyokubaliwa kikatiba ya mawaziri na wizara zao,na jinsi ya kuwapata na kuwaidhinisha ,muda si mrefu kwa huu mtindo tutakuwa na first lady waziri,mtoto wa presidaa naye waziri,nyumba ndogo ,mjukuu n.k.
Kwa ufupi waziri kwenda kwenye kampeni ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi,tutake au tusitake,sasa huko ofisini kazi zao wamemmwachia nani ,na hao ndio unawasikia wanasema tumwetumwa na raisi (sio mwenyekiti)
 
At least watanzania wanapata fursa ya kufahamu upana wa katiba utavyotakiwa kuwa!
 
Nimefuatilia kampeni za uchaguzi mdogo igunga,mi sidhani kama ni sahihi kwa viongozi kama mawaziri kushiriki kampeni,sababu waziri ni wa watanzania wote bila kujali vyama.Nimewaona Wasira,Magufuli n.k.Wadau mnasemaje..

Katiba ya Tanzania haiwakatazi kushiriki kwenye shughuli za kichama. Ikumbukwe kuwa mawaziri wote ni makada wa CCM. Hata kwenye kampeni ndogo za Marekani Hilary Clinton huwa anakwenda kuwapa nguvu Democrats kwahiyo sioni tatizo lolote hapo
 
Katiba ya Tanzania haiwakatazi kushiriki kwenye shughuli za kichama. Ikumbukwe kuwa mawaziri wote ni makada wa CCM. Hata kwenye kampeni ndogo za Marekani Hilary Clinton huwa anakwenda kuwapa nguvu CCM kwahiyo sioni tatizo lolote hapo

Kazi bado mbichi,

Bado unalinga na gpa ya 4.0!!
 
Katiba ya Tanzania haiwakatazi kushiriki kwenye shughuli za kichama. Ikumbukwe kuwa mawaziri wote ni makada wa CCM. Hata kwenye kampeni ndogo za Marekani Hilary Clinton huwa anakwenda kuwapa nguvu Democrats kwahiyo sioni tatizo lolote hapo
Tatizo ni pale wanapojazana kule kiasi kwamba anayegombea anafunikwa kabisa hasikiki tena. Kama RA na CCM ambao wamelishikilia jimbo hili tangu lilipojitenga toka Nzega miaka ya 70 wamefanya mema mengi hofu hii ya sasa inatokana na nini?
 
Uliza wewe usiye na chama.
Tukiuliza sisi wanatuita wachaga.
Tatizo ni pale wanapojazana kule kiasi kwamba anayegombea anafunikwa kabisa hasikiki tena. Kama RA na CCM ambao wamelishikilia jimbo hili tangu lilipojitenga toka Nzega miaka ya 70 wamefanya mema mengi hofu hii ya sasa inatokana na nini?
 
Nimefuatilia kampeni za uchaguzi mdogo igunga,mi sidhani kama ni sahihi kwa viongozi kama mawaziri kushiriki kampeni,sababu waziri ni wa watanzania wote bila kujali vyama.Nimewaona Wasira,Magufuli n.k.Wadau mnasemaje..

Unawaogopa hao mawaziri? Ngoja uchaguzi ukiisha tutaliangalia hilo!
 
Swali zuri zaidi ni kutumika kwa rasilimali za taifa kama vile magari, madereva na watumishi wengine wa umma katika shughuli za kampeni na uchaguzi.
 
maji yanapofika shingoni ndo huwa hivyo,
maji yakifika puani rais wao ataenda nae
 
utasikia mandela naye ametia timu hata kama ni mgonjwa lengo kudanganya wananchi kwa hiyo inabidi wale waongo maarufu watie timu
 
Anashiriki RAIS aliyechaguliwa na WATANZANIA wote itakuwa waziri ambaye kateuliwa na mtu mmoja tu!
Mawaziri wote ni makada wa CCM, hivyo huwezi kuwazuia kushiriki kampeni za chama chao. Tatizo linakuja wanapotumia rasilimali za serikali kufanya shughuli za chama. Haiingii akilini Magufuli kwenda Igunga, (Na hapa anatumia gari la serikali na mafuta ya serikali), na kuahidi barabara iwapo mgombea wake atachaguliwa. Fedha inayojenga barabara ni ya serikali na si fedha ya CCM. Wana Igunga wana haki ya kujengewa barabara bila kujali kuwa wako CCM au CDM.

Kwa maoni yangu, sababu hizi zinatosha kutengua ubunge mahakamani kama mgombea wa CCM akishinda. (Ilitokea Kigoma miaka ya 90 wakati Kabouru akipambana na Premji)
 
Magufuli ametoa ahadi ya kujenga daraja!! Anatoa ahadi kama nani??
 
Dah jamaa una akili wewe, kama mnaweza kuiga ya clinton basi magamba zaidi ya wasionazo

Katiba ya Tanzania haiwakatazi kushiriki kwenye shughuli za kichama. Ikumbukwe kuwa mawaziri wote ni makada wa CCM. Hata kwenye kampeni ndogo za Marekani Hilary Clinton huwa anakwenda kuwapa nguvu Democrats kwahiyo sioni tatizo lolote hapo
 
Na magufuli kuahidi daraja kama wakichagua magamba wakati daraja liko kwenye bajeti sio kuvunja katiba? na kama sio huoni kuwa ni hujuma dhidi ya vyama visivyokuwa na serikali? nataka jibu na sio hadidhi wala huitaji kamusi

wanaenda kwa tiketi ya chama, haina tatizo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom