Waziri anaposhiriki kwenye kampeni, je ni sawa?

Ngonini

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
2,023
562
Hivi sheria ya utumishi au maadili ya uongozi yanasemaje au waziri si mtumishi wa umma? Je wamechukua likizo ya muda gani maana wasira toka kampeni zianze yeye yuko igunga? Je kwa muda ambao hawapo ofsini kinyume na taratibu wanalipwa mishara ipi? Je mtu anatakiwa afukuzwe kazi kwa kutokufika kazini kwa muda gani?

Kama mawaziri ni watumishi wa umma na wanabanwa na maadili ya uongozi basi lazima kuna kesi ya kujibu kama kuna wanasheria wakiamua kuwafatilia hawa mawaziri wanaotanua Igunga.
 
Wambandwa

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
2,250
823
subirini kichapo magwanda mbona mnatia huruma mapema hivi?

Sasa wewe mrisya naona inabidi nianze kuwa PM kaka zako hapa amabao sio warisya kama wewe. Hilo jina unalidharilisha, watani zangu si waoga, legelege, wanafiki au wapumbavu.
Hawa ni mashujaa jadi tohara wanafanyiwa bila ganzi, na haruhusiwi kupiga kopa hata kope wakati wa zoezi hilo.
Nina mashaka sana kama haya uliyapitia, kisu ulipigiwa hospitali, na kwenu huwezi kupewa mke. S.u..d..
 
Mnyalu

Member
May 9, 2007
66
1
Ndio maana tunataka katiba mpya ambayo tutaka mawaziri wasiwe wabunge na pia tuwe na idadi kamili iliyokubaliwa kikatiba ya mawaziri na wizara zao,na jinsi ya kuwapata na kuwaidhinisha ,muda si mrefu kwa huu mtindo tutakuwa na first lady waziri,mtoto wa presidaa naye waziri,nyumba ndogo ,mjukuu n.k.

Kwa ufupi waziri kwenda kwenye kampeni ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi,tutake au tusitake,sasa huko ofisini kazi zao wamemmwachia nani ,na hao ndio unawasikia wanasema tumwetumwa na raisi (sio mwenyekiti)[/ QUOTE]

Mimi leo nimeshuhudia mkutano wa magufuli kata ya choma igunga. Mbali na kuwa na watu kiduchu ,bila haya alikuwa anawadanganya wana igunga kwamba ataomba bajeti ya ziada kwa ajili ya kuwatengenezea madaraja ambayo yamekuwa kero sugu miaka nenda rudi licha ya ccm kuahidi katika kila kampeni kuyatengeneza.

Ila kubwa kuliko zote na iliyonichosha ni pale alipompigia simu waziri wa kilimo, na kumuweka loud speaker aongee na wananchi na kutoa ahadi ya kukifufua kiwanda cha kuchambua pamba ambacho licha ya kwamba ni cha mtu binafsi (bwn rajani. Aliyepewa na swahiba wake rostam)kimebakia magofu baada ya mashine zote kung'olewa. Mbaya zaidi maghembe alikuwa anazungumza kama mtu aliyeshtuliwa usingizini. Ni aibu tupu!

Hakika magamba ni matapeli.
 
Mnyalu

Member
May 9, 2007
66
1
ukitaka kujua kwamba hawa mawaziri wa ccm ni wendawazimu fuatilia mikutano yao ya hadhara igunga. Utajua nchi imekwisha. Pumbaz pumbaz pumbaz.
 
Rweza

Member
Jun 18, 2011
77
42
Nilisikitishwa sana na maneno yale ya Magufuli na sikuamini kama yanatoka kinywani mwake, nina maswali kadhaa;

1.Je Magufuli anaweza kupanga bajeti ya daraja kwasababu tu wananchi wameichagua CCM?

2. Kama bajeti ya 2011/2012 haizungumzii ujenzi wa daraja lile, Magufuli atatoa pesa kwenye fungu lipi ili ajenge lile daraja? Au ndo zile 300milioni zilizokuwa zimewekwa pembeni mpaka walipozimega kufidia bajeti ya miundo mbinu?

3.Je wananchi wasipochagua sisiem daraja halitajengwa? Je atakuwa hajawakosea wananchi wa sisiem aliowaahaidi?

Kweli katiba mpya inabidi ijibu suala la kutenganisha Uwaziri na ubunge/uanasiasa otherwise kuna mkang'anyiko mkubwa sana na unaleta utahila kwa viongozi wetu.
 
Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,942
4,400
Nimefuatilia kampeni za uchaguzi mdogo igunga,mi sidhani kama ni sahihi kwa viongozi kama mawaziri kushiriki kampeni,sababu waziri ni wa watanzania wote bila kujali vyama.Nimewaona Wasira,Magufuli n.k.Wadau mnasemaje..

hawa wanaenda huko kwa kodi zetu tunao waungisha TBL tukifanya mgomo wa wateja wa tbl watapunguza visafari visivyo kuwa na tija.
 
Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,308
10,753
Jibu utakalopewa ni kuwa Wamekuja kwa nyadhifa za kichama, na si kama mawaziri!
Japo Swali linabaki palepale kuwa ofisi zao wamemwachia nani, au wako likizo?

Mbaya zaidi hao wahishimiwa wanatumia rasilimali za dola; nikimaanisha magari na mafuta yake, madereva na posho zao!!
 
Vatoi

Member
Aug 17, 2011
61
5
kwani hamjamwona wasira nae anauliza nani chadema, matokeo yake kanyooshewa vidole? hawataamini hata wakimpeleka malecela.
 
Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,144
3,189
Katika hali ya kushangaza, karibu nusu ya mawaziri wote wa serikali ya Kikwete ama wametembelea au wameweka kambi kabisa Igunga kwa ajili ya kampeni za CCM. Najiuliza, hawa mawaziri si wanatakiwa kuwa ofisini kuwatumikia watanzania? Je hawa mawaziri wakienda igunga wanaendesha magari binafsi kwa kutumia madereva binafsi? Kama wanatumia magari ya serikali, mafuta ya serikali na dereva anayelipwa na serikali, ni kwanini wanakifanyia kampeni chama kimoja ili hali wapo kiserikali na si kichama? Natoa pendekezo mawaziri wote waliotumia magari ya serikali kwenda Igunga kupiga kampeni washitakiwe. Chadema chukueni hoja hii ifanyieni kazi mara baada ya uchaguzi kuisha. Kwa hoja hii tu tunaweza pia tukaomba uchaguzi urudiwe kwa kuwa hakukuwa na usawa katika kampeni. Chama kingine kinatumia resource za chama wakati kingine kinatumia kodi za wananchi, wapi na wapi?
 
Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,046

Yani ukichunguza utendaji wa nchi hii wallah utaishia kutapata msongo wa mawazo tu. Haya mawaziri yamajisahau kabisa utadhani yapo likizo. Hapa kinachouma ni kwamba sisi ndo tunawawezesha katika kula, kulala na kututukana kwa kodi zetu. Isingekuwa hivyo, tungesema bora tu yawe Igunga mana hata yakikaa ofisini hakuna yanachofanya.
 
Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,046
Katika hali ya kushangaza, karibu nusu ya mawaziri wote wa serikali ya Kikwete ama wametembelea au wameweka kambi kabisa Igunga kwa ajili ya kampeni za CCM. Najiuliza, hawa mawaziri si wanatakiwa kuwa ofisini kuwatumikia watanzania? Je hawa mawaziri wakienda igunga wanaendesha magari binafsi kwa kutumia madereva binafsi? Kama wanatumia magari ya serikali, mafuta ya serikali na dereva anayelipwa na serikali, ni kwanini wanakifanyia kampeni chama kimoja ili hali wapo kiserikali na si kichama? Natoa pendekezo mawaziri wote waliotumia magari ya serikali kwenda Igunga kupiga kampeni washitakiwe. Chadema chukueni hoja hii ifanyieni kazi mara baada ya uchaguzi kuisha. Kwa hoja hii tu tunaweza pia tukaomba uchaguzi urudiwe kwa kuwa hakukuwa na usawa katika kampeni. Chama kingine kinatumia resource za chama wakati kingine kinatumia kodi za wananchi, wapi na wapi?
Yani ukichunguza utendaji wa nchi hii wallah utaishia kupata hasira tu. Haya mawaziri yamejisahau kabisa utadhani yapo likizo. Hapa kinachouma ni kwamba sisi ndo tunayawezesha kwa kodi zetu kula, kulala na kututukana. Isingekuwa hivyo, tungesema bora tu yawe Igunga mana hata yakikaa ofisini hakuna yanachofanya, yanasinzia tu.
 
Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,308
10,753
Katika hali ya kushangaza, karibu nusu ya mawaziri wote wa serikali ya Kikwete ama wametembelea au wameweka kambi kabisa Igunga kwa ajili ya kampeni za CCM. Najiuliza, hawa mawaziri si wanatakiwa kuwa ofisini kuwatumikia watanzania? Je hawa mawaziri wakienda igunga wanaendesha magari binafsi kwa kutumia madereva binafsi? Kama wanatumia magari ya serikali, mafuta ya serikali na dereva anayelipwa na serikali, ni kwanini wanakifanyia kampeni chama kimoja ili hali wapo kiserikali na si kichama? Natoa pendekezo mawaziri wote waliotumia magari ya serikali kwenda Igunga kupiga kampeni washitakiwe. Chadema chukueni hoja hii ifanyieni kazi mara baada ya uchaguzi kuisha. Kwa hoja hii tu tunaweza pia tukaomba uchaguzi urudiwe kwa kuwa hakukuwa na usawa katika kampeni. Chama kingine kinatumia resource za chama wakati kingine kinatumia kodi za wananchi, wapi na wapi?

Wenyewe wanasema ni mawaziri wa CCM!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom