Waziri Anapokurupuka

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
211
Hapo zamani katika kisiwa kimoja cha kifahari kulitokea kiongozi mmoja matata sana alipendwa na watu wake kutokana na utendaji wake wa kazi tokea ujana wake mpaka siku hiyo ambayo yeye mwenyewe ndio aliamua kusalimu amri .

Siku hiyo akaamua kufanya ziara ya ghafla katika moja ya miradi ya nchi hiyo alipofika pale akaona watu wapo kama hawapo , wengine wanafanya haya nay ale , akaanza kufoka , hata kutishia kufukuza baadhi ya maofisa wa kampuni ile pale pale .

Kesho yake ile ilikuwa ni habari kubwa katika magazeti ya nchi hiyo , lakini wale makandarasi waliokuwa wanafanya kazi pale walidhalilishwa waziri aliwafokea na kutoa maneno mengine ambayo kwa hakika wataalamu hawakuweza kuyamudu .

Waziri alifunguliwa mashitaka pamoja na wizara husika kwa pamoja na kampuni ile ilishinda ile kesi serikali yake ilitakiwa kulipa hela nyingi sana kama fidia kwa kampuni ile na wafanyakazi kwake kwa kuvunja ule mkataba na kuwadhalilisha .

Hadithi hii ni sawa ya waziri wa afya alivyofanya ziara ya ghafla katika hospitali ya taifa muhimbili siku chache zilizopita , katika moja ya maagizo yake alitaka kampuni ili isimamishe kazi zake pale watafute mkandarasi mwingine sijui kama hiyo imefanyika .

Waziri pamoja na watu wengine wasiojua mambo haya wanatakiwa wajue kwamba katika mradi wowote ule watu wanakuwa na mikataba yao na watu wanafanya kazi kutokana na mkataba unavyosema na gharama halisi ya mradi huo ni siri kati ya mkandarasi na mwenye kutoa kandarasi hiyo .

Sasa waziri anavyokuja kukurupuka tu na kusema kampuni ile isimamishe mradi ule , je wizara yake itakuwa iko tayari ya kulipa gharama za ule mradi kutokana na mkataba uliowekwa kabla ya mradi ule , au waziri alipitia mkataba huo kwanza kabla ya kuamua kuja kufunga mradi husika ?

Tunaomba viongozi wa serikali na wizara wasilete siasa katika mambo yenye masilahi ya nchi haswa miradi nyeti ya afya na mengine mengi ambayo hapa siwezi kuitaja ambayo inaingiliwa na watu kwa masilahi yao binafsi bila kuwasiliana na pande zote mbili .

Hii ni sawa na mkataba wa Richmond iwapo serikali ikiamua kuvunja basi kuna kupelekana mahakamani na serikali hiyo hiyo inaweza kushindwa kesa na kutakiwa kulipa pesa nyingine nyingi sana kwa sababu ya hizi hizi siasa ambazo kwa wataalamu hawazikubali .

Na mwisho kabisa waziri kama hata ujuzi au utaalamu wa kitu Fulani ni bora awasiliane na wanojua au kuwa na ujuzi na kitu husika kabla ya kutoa tamko ili isije kuwa shida kwao , ama kuwe na wasemaji wa wizara kama mawaziri ndio wasemaji wa wizara hizo basi wawe tayari kujibu maswali inapotokea wananchi wanakuwa na wasi wasi kuhusu matamko yao wanayotoa bila kumhusisha mtu wowote .
 
Mambo ya kasi mpya bwana si shida wao kufanya haya ili mradi kasi iwe kasi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom