Waziri anapoenda kukagua shule na gari ya millioni mia mbili

Hebu wanajamvi mnijuze kuhusu hili. Naibu waziri anapoenda kukagua shule akiwa amepanda gari la millioni 200, pamoja na msafara unaoambatana naye.

Je inaingia akilini kuona shule hazina madawati ili hali viongozi wenye dhamana wanafanya ufahari na mikogo na mambo hayo inaonyeshwa jamii iliyo katika lindi la umaskini?
Kwakweli hali hii inasikitisha saana, wapo viongozi wengine wa kisiasa nao huenda kwenye ziara, mikutano na maandamano ya vyama vyao na magari kama hiyo huku wananchi wale wengine hawana hata chakula. Nchi hii kwakweli, sijui tunaelekea wapi?
 
Back
Top Bottom