Waziri anapoenda kukagua shule na gari ya millioni mia mbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri anapoenda kukagua shule na gari ya millioni mia mbili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Makene, May 27, 2011.

 1. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hebu wanajamvi mnijuze kuhusu hili. Naibu waziri anapoenda kukagua shule akiwa amepanda gari la millioni 200, pamoja na msafara unaoambatana naye.

  Je inaingia akilini kuona shule hazina madawati ili hali viongozi wenye dhamana wanafanya ufahari na mikogo na mambo hayo inaonyeshwa jamii iliyo katika lindi la umaskini?
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  halafu anakuta matundu mawili ya choo yaliyojengwa kwa milioni sabini. Anapokelewa na mwalimu anayeidai serikali hela kibao na anayelipwa mshahara wa masihara.

  Anawakuta wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika hata kidogo.

  Safari report kwa bosi wake sijui ataeleza nini?

  So help us God
   
 3. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  jamani umeugusa mtima wanguuuu!
   
 4. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Ndio maana inaibuka mijamaa inakwenda kukagua miradi ya Maendeleo... kama yule tapeli wa NGARA...
   
 5. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Gari milioni mia mbili acheni uongo hakuna gari la serikali linalozidi milioni sabini kuanzia la rais hadi das wilayani unabisha
   
 6. a

  al-karim Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata kama ni 50m..bado sio sawa!
   
 7. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Hawanunui gali zilizokwisha tumika, serikari hununua magari mapya.
  Ingia kwenye mtandao Uliza bei ya new model land cruiser V8 mkonga;)
   
 8. Tidito L

  Tidito L Member

  #8
  May 28, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Du we kweli sijui uko dunia gani,zile V8 unazozionaga na viongozi ni million 280,kama unabisha ingia kwenye web.acha kujizalilisha bro watu wanakushangaa!

  Hii nchi kuna watu wanaifaidi bana kwa hela za walipa kodi.
   
 9. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Kwa sababu wananunua mengi, wanaweza kuwa wanapewa bei ya jumla tofauti na unayoona wewe kwenye mtandano wa dealer.

  By the way, mtandao gani huo una bei ya Land Cruiser jipya VX, hebu tuonyesheni.
   
 10. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Wakati wa kutiana hasira ndo huu, angalizo: kama tumeamua kujenga chuki baina ya watawala na watawaliwa tujue na tkubali matokeo yake, tujue kuwa chuki zikiiva waathirika wakubwa ni walalahoi na hao munaodhani munawapiga vita mutabaki munachomana visu wakati wao wako Europe (Tazama Rwanda na Kenya). Mjue kuwa kiongozi mwandamizi kutumia gari enye capacity kubwa ni inevitable, rest munatafuta matatizo katika nchi.
   
 11. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Tuwe wakweli Toyota Land cruiser hard top ni Dollar za kinaObama 77,000 ije kuwa hilo V8......fanyeni utafiti wazawa
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  huyu sijui wa wapi!???
   
 13. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  "Wakati wa kutiana hasira ndo huu, angalizo: kama tumeamua kujenga chuki baina ya watawala na watawaliwa tujue na tkubali matokeo yake, tujue kuwa chuki zikiiva waathirika wakubwa ni walalahoi na hao munaodhani munawapiga vita mutabaki munachomana visu wakati wao wako Europe (Tazama Rwanda na Kenya). Mjue kuwa kiongozi mwandamizi kutumia gari enye capacity kubwa ni inevitable, rest munatafuta matatizo katika nchi."

  Nikisoma maoni kama haya ninajisikia nataka kutapika!! Huyu mbongo anaishi karne ya 18. Kazi ya watawala si kutumia vibaya kodi ya walipa kodi, bali ni kuhakikisha inatumika vizuri ikiwa ni pamoja na wao kuwa na nyenzo za kazi na pia huduma bora za msingi kama vile elimu. Basi kama hawawezi kuhakikisha watoto wa shule za msingi na sekondari wanapata madawati - na hapa tunazungumzia MADAWATIIIIIIIIIIIIIIIIII!!!, basi hawana sababu ya kutembelea hizo shule. Wajikalie huko ofisini watumie hayo magari yenye capacity kubwa. Ndugu kinachozungumzwa hapa sio chuki kati ya watawala na watawaliwa, bali ni kuwajibishana kati ya watawala na watawaliwa. umeniharibia siku yangu:angry:
   
 14. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Nduhu shida, endelea kuwa negative na kusapoti neg movements. Sisi kama wasomi tutambue pia kuwa kuna propa forums za ku-ea viyuz. Mbona hata wabunge wetu wanatumia simila vehicles na hatukemei?!. Nasema; kutumia gari kubwa kwa barabara zetu ni innevitable.
   
 15. Banzi

  Banzi Member

  #15
  May 28, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aise we jamaa ni bonge la bogus hakuna msomi yeyote anweza ku-support ujinga unaoongea hapa, otherwise ni wasomi wa type yako. Inavitability hapa inatoka wapi, unadai eti barabara..what is that... nani alipaswa kujenga hizo barabara mpaka tufike mahari tunahitaji magari powerful kwa shughuli zisizo na tija. Fuatilia mambo vizuri pumbavu, rais wa Senegal aliwahi kuwa natumia Volkswagen ya kawaida kabisa na bado aliitwa Rais, na heshima yake itabaki hivyo. Heshima kwa viongozi ni uwajibikaji na ufanisi katika kutoa na kusimamia huduma za jamii.
  Kifupi umeharibu siku yangu...zebedayo mkubwa weye....sijui wawapi wewe, au mkimbizi?
   
 16. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Hujui bei ya VX V8, Serikali yenye inasema ni 200m pale Japani. Land cruiser hardtop brand ni 130m, sasa hilo la 70m ni aina gani kijana? Penye ukweli tuseme na ikiwezekana tukosoe pale inapobidi!
   
 17. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  kutumia gari kubwa kwa barabara zetu ni inevitable! Mhh what a comment! nilifikiri kinachopaswa kuanza ni kutengeneza barabara bora ili magari hata madogo yaweze kufika mpaka vijijini lakini pia kwa kufanya hivyo kutakuwa na cascading effect kwasababu wakulima pia wataweza kusafirisha mazao kirahisi na pembejeo zitawafikia kiurahisi lakini pia bei ya za vyakula zitapungua kwa kiasi kikubwa! kununua magari makubwa tena kila baada ya miaka 2 si suluhisho la matatizo ya barabara zetu lakini ni chanzo cha kufanya viongozi wetu wasifanye maamuzi magumu ya kuendeleza barabara zetu. mkuu Gama wakati mwingine usikimbilie kutetea upuuzi na kujifanya uko analytical!
   
 18. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Baada ya matusi onesha gari lako na useme how much ume-devot kwa ndugu zako, si unajua "charity begins................................"
   
 19. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
 20. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #20
  May 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  je thamani ya pound ya uingereza ni sawa na ile ya dollar ya kimarekani
   
Loading...