MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,757
- 48,407
Huwa nikisoma taarifa za wabongo nacheka sana, yaani ndugu zetu wa kusini mwa mpaka wetu wanaishi wakirushiana vijembe kuhusu Kenya. Mara hatutaiga Kenya, tutaishinda Kenya, Kenya ni kainchi kadogo, Kenya lazima tuwashinde n.k.
Yaani wakisikia jina la Kenya wanatokwa na povu hadi inashangaza.
Hapa waziri anaapa hawataiga Kenya wala taifa lolote majirani, wakati huo huo wanaagiza wataalam kutokea Rwanda na kufuata ushauri wa huko kununua ndege. Kituko full...
================================================
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema Tanzania siyo koloni la Kenya kwamba kila mipango yake ya maendeleo itegemee Taifa hilo.
“Kenya siyo sehemu ya Tanzania na sisi (Tanzania) si koloni la Kenya. Kenya ni nchi tofauti, Uganda ni nchi tofauti, Uingereza ni nchi tofauti,” amesema Profesa Maghembe.
Profesa Maghembe ametoa kauli hiyo kufuatia malalamiko ya mawakala wa utalii wanaodai hatua ya Serikali kutoza Vat kwenye utalii kutaathiri sekta hiyo na kwamba, watalii wengi wamesitisha safari zao na wengi wameamua kwenda Kenya kwa vile nchi hiyo imeondoa kodi hiyo.
“Hizi ni kodi ndani ya Tanzania. Kenya ina mazingira tofauti kabisa na Tanzania. Hatuwezi kupanga kodi kwa maendeleo ya nchi yetu tukiwatazama wao,” amesema.
Tanzania siyo koloni la Kenya-Maghembe