Ligaba
JF-Expert Member
- Oct 12, 2018
- 1,045
- 2,821
Bado Tundu Lissu anaendelea kutaja kuliko mtu yeyote kwa sasa katika siasa za Tanzania.
Jana niliona majibu ya Waziri Kangi Lugola kuhusiana na ushambuliwaji wa Lissu, nilichogundua kuna uzembe wa hali kutoka katika Jeshi la Polisi na hata Wizara yote yenye mamlaka ya kushughulika na sakata hilo kwa namna ifuatayo.
1. Ukiwa Mtuhumiwa siku zote ni uzembe wa hali juu kwenda hadharani kulalamika na kusema wewe sie hali ya kuwa kuna njia ifaayo kukufanya usionekane mtuhumiwa. Nafikiri Tundu Lissu anaishutumu serikali ndio wapangajj wa jaribio la kumuua, waziri ni Serikali. Serikali kupitia kwa waziri wakipanga kujinasua au kama wasemavyo wanajengewa chuki, wana jambo moja tu la kufanya. WAITE JOPO HURU LA WACHUNGUZI WA KIMATAIFA. Hii itasaidia sana maana nionavyo kwa namna yoyote iwe imehusika au aikuhusika hakuna atakae waamini kwa taarifa yoyote na na itolewe na mtu yeyote.
2. Uzembe mkubwa wa pili ni pale waziri anapomtaka Lissu aje ataje kwamba waliomshambulia ni watu wa muonekano gani, majike, madume, meupe au meusi, mafupi au malefu, hii ni aibu kubwa kwa kiongozi mwenye wadhfa wa kiwango cha waziri kutamka. Jiulize hivi ailiporudishwa Roma, aliporudishwa Mo ndio kusema hawa nao hawakutoa taarifa au nao wako nje ya nchi kiasi cha serikali kushindwa kutaja au kukamata hata muhusika mmoja? Kwa nini tusiamini wizara ya Kangi Lugola ni zembe mara kumi ya Lissu?
Nawakumbusha tu serikali pale ambako ina ufanisi nzuri ni wakati waliouwawa ni watu wao, Rejea kifo cha kamanda wa Polisi mwanza -watuhumiwa walikamatwa ndani ya wiki moja, Rejea majambazi waliouwa polisi stakishari, Mbande na kwengineko wote walipatikana.
Ningemsihi waziri Lugola na serikali yake, njia pekee ya kuisafisha serikali na Rais wake ni kuita timu huru ya wachunguzi wa kimataifa, matokeo ya timu hiyo inaweza kuisaidia hata serikali kumshtaki Lissu na shutuma zake.
Sent using Jamii Forums mobile app