Waziri alishitaki gazeti la kila siku, adai fidia ya tsh. 1 bilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri alishitaki gazeti la kila siku, adai fidia ya tsh. 1 bilioni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Jan 24, 2011.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  NAIBU Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya analidai gazeti la kila siku la Kiswahili, fidia ya shilingi bilioni moja kwa madai ya kukashifiwa.

  Naibu Waziri huyo anadai kuwa gazeti hilo, lilichapisha wiki iliyopita habari anayodai ni ya uongo kumhusu yeye, yenye kichwa cha habari kinachosema, “Gari la Waziri lahusishwa na wizi”.

  Hayo yamo katika barua iliyopelekwa kwa gazeti hilo na Kampuni ya Mawakili ya East African Law Chambers ya Dar es Salaam.

  Barua hiyo imesema habari hiyo ya gazeti hilo, imemvunjia mteja wao heshima mbele ya jamii, familia yake, na mamlaka iliyomteua.

  East African Law Chambers imetoa siku saba kwa gazeti hilo kuomba radhi na pia imemtaka mteja wao kulipwa fidia ya Sh bilioni moja, kutokana na kukashifiwa na kudhalilishwa mbele ya jamii, familia yake na mamlaka iliyomteua.

  Pia, imesema habari hiyo imemweka mahali pabaya na pagumu mteja wao, kwa sababu ilinukuliwa kwenye magazeti mbalimbali na kutangazwa na kurushwa hewani kwenye televisheni na redio.

  East African Law Chambers inasema kwamba habari hiyo ilisema kwamba, “Jeshi la Mkoa wa Morogoro limekamata gari la Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya, likihusishwa kubeba tani 30 madini ya shaba iliyoibwa mkoani Morogoro.”

  “Naibu Waziri huyo hamiliki gari hilo ambalo limetajwa aina ya Toyota Surf. Hali kadhalika Naibu Waziri huyo hamiliki hoteli ambayo imetajwa. Pia mtoto wa Naibu Waziri hakutumiwa na Polisi kuwatafuta wahusika,” imesisitiza barua hiyo kutoka East African Law Chambers.

  Source: Habari leo

  My take: Huu ni udhaifu mkubwa ulioonyeshwa na gazeti linalomilikiwa na serikali. Kama habari ni ya uhakika, kwanini jina la gazeti wameliwithheld. Gazeti la habari leo inaelekea kuwa gazeti la udaku! Halafu Nkya anatamka kirahisi fidia ya I.bilion! it's amazing! anadhani wote ni mafisadi kama chama chake! Tatizo viongozi wa serikali ya ccm wamezoea editing, yaani kabla habari haijaandikwa wanataka waulizwe tuitoeje hii habari, badala ya kuandika ukweli watataka wafanye editing!
   
 2. M

  Mtemakuni JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni mkwara tuu ili asafishwe jina lake!! usikute kweli alihusika now anajitahidi kufukia mambo caz huyo mama sio mwema kihiivyo na vi NGO vyake hapa moro vya watoto yatima anapiga ufisadi tuu....!! :suspicious:
   
Loading...