Waziri alidanganya Bunge, aingia 18 za Zitto!

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,697
8,843
ZITTO KABWE AELEZEA BARUA KALI ALIYOMUANDIKIA SPIKA MAKINDA!!

10zitto.jpg

"Nimeandika barua Kwa Spika wa Bunge kutaka Waziri wa Nishati na Madini kutoa maelezo Bungeni kuhusu uamuzi wake wa kuwapa leseni kubwa ya kuchimba #Uranium huko wilayani Namtumbo. Mnamo tarehe 10 Agosti 2012 Waziri alitamka ndani ya Bunge "sisi tunajua zaidi ya anavyojua yeye, Leseni haijatolewa na haitatolewa mpaka Kampuni ya #MantraResources ilipe kodi".

Kodi ya ongezeko la mtaji (capital gains tax) ya $189m kufuatia mauzo ya mradi wa #MkujuRiverProject kutoka kampuni ya Mantra kwenda kampuni ya AMRZ ya Urusi iligomewa kulipwa. #TRA wamepeleka shauri hilo mahakama ya kodi na mpaka sasa maamuzi hayajatolewa. Kwa mujibu wa mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2012, kabla ya Waziri mwenye dhamana ya madini kubariki mauzo ya kampuni, anapaswa kupata Kibali Cha kwamba kodi zote stahili zimelipwa. Kibali Kwa kampuni ya mantra kilitolewa bila kujali hitaji la kisheria na sasa kampuni hii imepewa leseni.

Maamuzi haya ya Waziri wa Nishati na Madini yanalikosesha Taifa mapato ya zaidi ya tshs 300bn ambazo zingeweza kumaliza tatizo la nyumba za walimu nchi nzima na kulipia madai yote ya walimu. Fedha hizi zingeweza kujenga barabara ya lami kutoka Manyoni mpaka Itigi. Fedha zingeweza kukarabati reli ya Kati na kuirejesha katika ubora wa unaotakiwa. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge nimetaka Waziri atoe maelezo bungeni na wabunge wajadili. Ni dhahiri kwamba serikali inayoongozwa na CCM imeamua kumaliza utajiri wote wa nchi na kuugawa Kwa wageni Kwa bei ya Che. Wananchi Ni lazima kusimama imara kukataa uporaji huu na maamuzi haya ya kiburi Cha kudharau Bunge yaliyoyafanywa na Serikali

Mnamo tarehe 10 Agosti 2013

Asante mkuu kwa taarifa, samahani kwa usumbufu naomba ufanye editing kidogo naona hatujafika bado hizo tarehe!
 
Kumbe tumeshaanza kuchimba hii makitu?

Mbona Tanzania resources nyingi lakini maendeleo hakuna?

Kwanini Uranium tusiwawekee next generation sisi tuendeleze kilimo kwanza?
Kwa mara ya kwanza nakuona Maundumula uki-question utendaji wa serikali yako. Ukishaona serikali ipo tayari kuacha mipesa yote hiyo kwa mwekezaji basi ujue wakubwa washachukua chao. Hapo hata watu wapige kelele vipi, Kikwete ataweka pamba masikioni.
 
Last edited by a moderator:

Tatizo watanzania tunapiga kelele tu tunatakiwa tuwaonyeshe kwa vitendo hawa wapumbavu....
 
Kumbe tumeshaanza kuchimba hii makitu?

Mbona Tanzania resources nyingi lakini maendeleo hakuna?

Kwanini Uranium tusiwawekee next generation sisi tuendeleze kilimo kwanza?

Mkuu Maundumula nakubaliana na wewe kabisa. tanzania ni nchi ambayo ina rasilimali nyingi mno lakini hatuzitumii vizuri. Tusipoangalia tutageuka kuwa kama DR Congo wakati fulani walikosa hata mtaji wa kuchimba rasilimali zilizozagaa nchini humo. Tuwe wazalendo, tufikirie watoto wetu na vizazi vijavyo.
 
Kumbe tumeshaanza kuchimba hii makitu?

Mbona Tanzania resources nyingi lakini maendeleo hakuna?

Kwanini Uranium tusiwawekee next generation sisi tuendeleze kilimo kwanza?
USA naambiwa wana mafuta mengi sana lakini hawaja waza kuaanza kuyachimba jiulize kwanini...
 
Kwa taarifa tu Tanzania ni ya tatu duniani kwa kupewa misaada baada ya Somalia na Afghanistan.na ndio maana Rais hajui kwanini sisi ni masikini!
 
Aibu nkisikiaga tanzania tunachimba madini mengi lakini ndo masikini namba moja

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nayo hii yawezekana tukabadilishana na vyandarua vya uzazi wa mpango. Ccm hoyee!
 
Siku zote nasema uelewa mdogo wa siasa kwa watz wengi ni janga la kitaifa kwani baadhi ya wanasiasa uchwara wenye ubinafsi na kutaka misifa binafsi iliyopitiliza huku wakijifanya nje wazalendo wakati ndani ni vibaraka vya mafisadi wanaendelea kutuchezesha sarakasi zao zisizo na kichwa wala miguu[shame on them].watanzania bila kujua wanashabikia upuuzi huo.lakini ukweli una tabia ya kutokubali kupuuzwa ipo siku itafahamika tu.unafiki unafiki unafiki mpaka lini naibu k.mkuu
 
Kwa mara ya kwanza nakuona Maundumula uki-question utendaji wa serikali yako. Ukishaona serikali ipo tayari kuacha mipesa yote hiyo kwa mwekezaji basi ujue wakubwa washachukua chao. Hapo hata watu wapige kelele vipi, Kikwete ataweka pamba masikioni.

Mkuu Lukolo, usidhani akina Mkuu Maunduluma hawaujui ukweli; wanaujua sana, sema tu wameajiriwa kutetea hata vitu ambavyo inabidi uwe na akili ya mwendawazimu ili uweze kuvitetea.
 
Last edited by a moderator:
USA naambiwa wana mafuta mengi sana lakini hawaja waza kuaanza kuyachimba jiulize kwanini...

Hehehe hata mimi nimeisikia hii kitu.

Jamaa wanashadadia mafuta ya mwarabu kwanza wanajua nini wanafanya.

Ingefaa sana kama hiyo Uranium tungeichunia tu!
 
Marekan kupitia MCC wamesema tanzania itaendelea kupatiwa misaada maana imesaidia kupambana na rushwa na imetokomeza VIASHIRIA VYA RUSHWA
 
" Maamuzi haya ya Waziri wa Nishati na Madini yanalikosesha Taifa mapato ya zaidi ya tshs 300bn......... "

Alitakiwa tayari awe ameshakabidhi barua ya kuacha kazi. Na ----.KURU walitakiwa wameshamkamta na kumfungilia mashitaka kwa kutumia madaraka yake vibaya (Ref. YONA & MRAMBA).

Lakini unjua kitatokea nini? NOTHING !!! Kama wanavyosema wenyewe.... haya yatapita tu, maana madamu supika hawezi ruhusu wakuu wake wavuliwe nguo hadharani.
 
Back
Top Bottom