Waziri akiri nyuzi za pamba kiwanda cha URAFIKI zinatoka china | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri akiri nyuzi za pamba kiwanda cha URAFIKI zinatoka china

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GY, Nov 18, 2009.

 1. GY

  GY JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Ufisadi umejikita zaidi kwenye matumizi mabaya ya rasilimali za umma, na kila mwananchi anajua ubaya wa jambo hili na hatari yake kwa taifa. Tumeshasema sana na tuendelee kubanana ili mapambano haya yasiwe ni nguvu za soda.

  Lakini pia tuanze kungalia muelekeo wa uchumi wetu ukoje, focus ikiwa hasa kuhusu sera na mipango mbalimbali ya kitaifa.

  Jana waziri wa viwanda na biashara Bi Mary Nagu amekiri kuwa nyuzi zinazotumika katika kiwanda cha nguo cha URAFIKI zinatoka nchini China..(TBC 1)


  Najaribu kuitazama hii issue katika mapana yake kidogo, mfano

  Misaada ya wachina inavyoambatana na makampuni toka kwao, wakiwemo mpaka vibarua wa ujenzi wanaobaka dada zetu na kuzaa nao bila serikali kuwa na uwezo wa kufanya lolote

  Misaada toka china inavyoambatana na sera za kuruhusu raia wa nchi iyo waje watakavyo hata kama wanakuja kuwa wamachinga kariakoo, au kufungua vimigahawa vya mama ntilie. Sijasema hapo kuhusu kuruhusiwa kwa bidhaa sub-standard kutoka nchi hiyo

  Misaada kutoka Japan inavyoambatana na sera ya ununuzi wa magari ya kifahari na magari chakavu toka nchini humo

  Mifano iko mingi sana, lakini kila rafiki na mwekezaje ajae hapa nchini anaonekana kuwa anayo ajenda yake

  Uwekezaji usio tija toka Afrika kusini na namna nchi iyo inavyoleta malighafi ambazo kimsingi hata hapa zinapatikana kirahisi mno. Ebu tazama shairi, madawa, na items mbalimbali zinazotumika katika kiwanda cha bia cha TBL zinatoka hapa nchini au South Africa

  Ushirikiano na India na namna tunavyoletewa vitu vya hovyo kama bajaji ambazo si tu kuwa zinadhoofisha sekta ya umma ya usafiri (public transport system), lakini pia ni janga litakalokuja kuturipukia muda si mrefu

  Kama alivyouliza Makwaia wa Kuhenga jana katika kipindi chake "Je tutafika" Iko wapi focus ya uchumi ya nchi hii??

  Sijasema athari za ushiriano wetu na mataifa makubwa ya ulaya na marekani, maana hao tumewakaribisha mpaka chumbani, wanatujua kuliko wandani wetu

  Swali langu ni kuwa ivi bado kuna nchi kweli hapa, au mkusanyiko wa viumbe fulani mahali fulani, vikiwa havina mbele wala nyuma

  AM JUST CURIOUS!
   
 2. P

  Prior Master Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uwekezaji huo faida negative (loss). Faida investment kwa taifa (tricle down)itatokana na uuzaji wa pamba (Kilimo kwanza would me more meaningful) wider population ingefaidika toka wakulima usukumani, transporters wachuuzi (Kote huko ajira 1,000,000 za Kikwete) etc. Soko la pamba limekuwa stricked na recession then viwanda vyetu tunaimport pamba haiingii akilini we are loosing much in intrenational trade worse still hawa wachina wala hawaajiri kiviile
   
Loading...