Waziri akana kuwa muoga katika kumshauri Rais Magufuli

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina amesema mawaziri walioteuliwa na Rais John Magufuli si waoga na wanatekeleza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kumshauri Rais katika masuala mbalimbali.

Mpina aliyasema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu mkoani Simiyu huku akisikitika kuwa maneno yanayotolewa dhidi ya mawaziri na manaibu na viongozi wa vyama vya upinzani kuwa wao ni waoga na hawamshauri Rais si sahihi.
Alisema baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakibeza utendaji wa Baraza la Mawaziri na kuwaita waoga wasiomshauri Rais.

“Wapo wale wenzetu wa upande wa pili ambao ni wapinzani wamekuwa wakitubeza mawaziri tulioteuliwa na Rais Magufuli kuwa tumekuwa waoga na hivyo kushindwa kumshauri na kulifanya taifa kusinyaa, hii si kweli. Nyinyi ni mashahidi, mmeona jinsi tunavyochapa kazi,” alisema.

Katika kudhihirisha kuwa wanatekeleza wajibu na kumshauri Rais, Mpina alisema Serikali iliamua kumnyang’anya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye shamba la hekta 33 kwa kushindwa kuliendeleza.

“Oktoba 28, mwaka huu, Rais John Magufuli alibatilisha hati ya kumiliki ardhi ya shamba namba 3074 lililopo Mabwepande, Dar es Salaam lililokuwa na hati namba 53086. Jina la mmiliki lililoandikwa katika hati ni Frankline Sumaye huu ni ushauri Rais alipewa na Waziri wa Ardhi na akachukua hatua,” alieleza Mpina.

Alisema wataendelea kuchukua hatua bila ubaguzi wa aina yoyote kwa wasiotaka kufanya kazi kwa kufuata utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
..SIRI YA VIKAO VYA BARAZA LA MAWAZIRI.

..hapo ndipo unapoona busara ya kuwa na semina elekezi. Ni kuepuka uropokaji kama huu.

cc MsemajiUkweli , Nguruvi3
Mkuu JokaKuu

Ipi hapo kwenye maelezo ni siri ya vikao vya Baraza la Mawaziri.

Mbaya zaidi, Naibu Waziri haingii kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri wa Tanzania.

Kumbuka pia alichokisema Mpina ndicho kilichosemwa katika Katiba ya Tanzania katika Ibara ya 54(3) inayosema;

54(3) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya Katiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.

Kwa kumalizia, hii habari imetoka wapi kwa sababu siku hizi udaku umekuwa ni mwingi sana hapa jukwaani.
 
..SIRI YA VIKAO VYA BARAZA LA MAWAZIRI.

..hapo ndipo unapoona busara ya kuwa na semina elekezi. Ni kuepuka uropokaji kama huu.

cc MsemajiUkweli , Nguruvi3
Sasa tunajua kumbe shamba limejadiliwa katika kikao cha baraza na tunajua DC katumwa tu. Hii ni mbaya na ni mbaya kweli kweli

Picha inayoonkena hapa ni kuwindana, ni 'mfumo wa visasi' au kukomoana

Mwisho wa siku suala zima liwe katika muktadha wa sheria au liwe katika hali nyingine yoyote 'Mzee'' ndiye atabeba dhamana!

Kwakweli kuropoka kumetusaidia kujua mengi
 
Hahaaa hawa mawaziri ni comedian tu..Eti anajigamba walimshauri Rais amnyang'anye shamba Sumaye. Kwa hiyo huo nao ni ushauri wa maana kwao?? Kwa hiyo kumnyanganya Sumaye shamba kumesababisha haya mambo kutatuliwa..
1. Wanafunzi vyuoni kupata mikopo?
2.Kuongeza viwanda?
3.Kukuza uchumi?
4.Kutoa ajira mpya?

Kama washauri wenyewe ndo hawa kwa nini nchi isiendeshwe kwa matukio.
 
Ha ha ha ha ......kwa hiyo kikao kizima cha baraza la mawaziri wakaazimia wamshauri Rais ampoke Sumaye Shamba.....sio wamshauri Rais khs uchumi unavyokwenda.......Duh...... Kweli hawamuogopi.
 
"MsemajiUkweli, post: 18685997, member: 91662"]
Ipi hapo kwenye maelezo ni siri ya vikao vya Baraza la Mawaziri.
Hivi maamuzi ndani ya vikao vya serikali yanatangazwa na kila mtu?

Kama tutakubaliana na hoja ya naibu waziri si mjumbe, kifungu hiki hapa chini hakimhusu

Mbaya zaidi, Naibu Waziri haingii kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri wa Tanzania.

Kumbuka pia alichokisema Mpina ndicho kilichosemwa katika Katiba ya Tanzania katika Ibara ya 54(3) inayosema;

54(3) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya Katiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.

Kwa kumalizia, hii habari imetoka wapi kwa sababu siku hizi udaku umekuwa ni mwingi sana hapa jukwaani.
Unaona utetezi wako unavyokosa mashiko?

Kwamba naibu haingii katika cabinet, halafu unatupa kifungu kinacholinda aliyoyasema akiwa 'mjumbe' wa Cabinet uliyesema haiiingi.
 
Wapi Mhe.JANUARY Makamba,amekuwa kimya sana...naona Naibu wake anavuma kana kwamba yeye ndy waziri ktk wizara hiyo,kulikoni!?
 
Duhh huu ushauri hata mtoto mchanga ataushangaa....
Yani watu tunalia mtaani hali mbaya yeye analeta habari za mashamba ya hekali35...
Huu uongozi huu tutaona mwsho wake.....
Bt mwsho ni mbaya...
Naskia huyu wa Dar yy anajiita mungu??????
 
Back
Top Bottom