Waziri 'ajitundika' ATCL...................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Waziri 'ajitundika' ATCL


Imeandikwa na Lucy Lyatuu; Tarehe: 8th December 2010 @ 06:11 Imesomwa na watu: 52;

WAZIRI wa Uchukuzi, Omar Nundu amesema, anakusudia kuiwezesha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ijiendeshe kwa umahiri mkubwa ili ichangie kikamilifu katika kutoa huduma bora na nafuu za usafiri wa anga kwa wananchi.

Tangu ilipobinafsishwa kwa Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA), ATCL imeshindwa kuwa katika hali nzuri kibiashara na katika miaka ya karibuni, hali imekuwa mbaya zaidi kwani imekuwa na ndege chache, lakini ikiwa na wafanyakazi zaidi ya 300 wanaotegemea ndege zisizozidi tatu.

Baada ya ‘ndoa’ yake na SAA iliyofungwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 kuvunjika, ATCL imekuwa ikijiendesha kwa shida, wakati mwingine ikiwa haina fedha za mafuta za kurusha ndege zake na pia fedha za kuwalipa wafanyakazi wake, hali iliyoilazimu serikali kusaka mbia wa kuiendesha.

Hata hivyo, mbia hajapatikana ingawa sasa inaelezwa kuwa imekuwa katika mazungumzo na Shirika la Ndege la Sonangol linalomilikiwa na serikali za China na Angola, ili awe mbia wao.

Lakini akizungumza Dar es Salaam jana kwenye kilele cha Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga, Nundu anayetoka katika tasnia hiyo ya masuala ya usafiri wa anga, alisema kusudio lake ni ATCL kuendeshwa kwa umahiri mkubwa ili lichangie kikamilifu katika kutoa huduma bora na nafuu kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Waziri Nundu, kusudio hilo litakwenda sambamba na juhudi za kuandaa mazingira yatakayolenga kuongeza mchango wa sekta binafsi katika kujenga na kuendesha viwanja vya ndege.

Alisema kwa kuzingatia usafiri nafuu unafanikiwa, serikali itaboresha pia mazingira na kufungua milango ya biashara yenye kuvutia mashirika na kampuni mbalimbali kuwekeza katika sekta ya usafiri wa anga kama njia ya kuchochea ukuaji wa safari za ndege na ongezeko la idadi ya abiria.

“Tutafanya juhudi za makusudi na kuchukuwa hatua za dhati kuhamasisha na kuvutia wawekezaji wa usafiri nafuu ili nauli zishuke kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuutumia usafiri huu na kufanya soko lake likue,” alisema Nundu ambaye kabla ya kuwania ubunge wa Jimbo la Tanga Mjini na kushinda, alikuwa Rais wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).

Alisema kwa sasa serikali kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali, ipo katika hatua tofauti za uboreshaji wa viwanja vipatavyo saba nchini, ambavyo ni Arusha, Mafia, Bukoba, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Mpanda.

“Kwa viwanja vya Mpanda na Mafia, uboreshaji umeshaanza na hivi sasa wataalamu wameshaanza kazi katika viwanja hivi…huko Mbeya nako shughuli zinaendelea ambako ujenzi wa jengo la kufikia abiria na uwekaji lami katika njia ya kurukia katika Kiwanja cha Ndege cha Songwe unaendelea,” alisema.

“Ujenzi wa kiwanja kipya cha kimataifa cha Msalato mkoani Dodoma, ujenzi wa Kiwanja cha Kimataifa cha Bagamoyo na kuboresha Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kwa kujenga jengo jipya la abiria na majengo mengine ni baadhi ya miradi itakayopewa kipaumbele katika kipindi cha miaka mitano ijayo.”

Aidha, aliagiza miundombinu ya viwanja vya ndege itumiwe kwa kazi iliyokusudiwa na sio kugeuzwa stoo ya kuhifadhi vitu kama ilivyo kwa karakana ya kutengenezea ndege iliyoko Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro.

Pia alitoa maagizo mbalimbali huku akitaka kupatiwa ripoti ya utekelezaji wake kila mwezi ikiwemo na kukamilishwa kwa kiwanja cha ndege cha Songwe kwa muda uliopangwa na kwa kiwango kilichoainishwa kwenye mkataba wa ujenzi na kupitia upya Sera ya Taifa ya Uchukuzi kwa kuwa sasa imepitwa na wakati.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Fadhili Manongi alisema sekta hiyo inakabiliwa na changamoto ya kukosa wataalamu wazalendo na waliopo wana umri mkubwa.

“Kwa hivi sasa nchini kuna wahandisi wa ndege 221 na kati yao, Watanzania ni 108 tu na wahandisi 113 waliobaki ni raia wa nje, hali kama hiyo ipo pia kwa marubani ambapo takwimu zinaonesha wapo marubani 364 na kati ya hao, Watanzania ni 155 na wageni ni 209,” alisema Manongi.
 
Serikali ilishajivua kufanya biashara, cha kufanya hapa waiombe Precision watumie bendera ya Taifa kwenye ndege zake na Route zote za ATCL zikabidhiwe Precision. Kuruhusu kampuni inayofanya hasara ipunguze mapato ya kampuni inayofanya faida ni kupunguza mapato ya serikali yanayotokana na kodi ya mapato
 
shirika hilo lipo ila kwa sasa lina kibajaji kimoja tu kinachoruka kwenda kigoma. mwanangu kama unaenda huko kikazi for 2 dys beba pesa ya hotel ya kutosha waweza kaa hata 5 dys kibajaji hakijaruka huko.

For him is good plan, but for us wit little hop kwa utendaji wa kibongo bongo, karibu waziri but this is TZ not Monterol ICAO
 
WAige mfano wa Kenya Airways. MD au CEO asiingiliwe na serikali, apewe uwezo wa kuajiri na kufukuza inapobidi. Mnajua kuwa serikali ndio imeliua shirika la ndege kwa ma LPO yasiyolipwa? Wakilifufua shirika kila kitu kiende kwa CASH. Na ile hali ya kulea wafanyakazi 300 na ndege tatu ife. Weka wafanyakazi wachache wanaozalisha siyo tu ili mradi ni shirika la serikali liwe dampo la kuwaajiri ndugu, jamaa, na marafiki na kusafirisha kwa mikopo vigogo wa serikali. ATC ikitoka Dubai inajaza tani za mizigo ya shopping ya wafanyakazi, vigogo na wafanya biashara ambayo hailipiwi. Hivi bila kuilipia hiyo mizigo mnategemea nini? Hebu amkeni nyie Wadanganyika, wakati wa kuleana umepita.
 
Why kiwanja kingine huko Msonga - Bagamoyo? Kwanini wasiimalishe Uwanja wa Dar na ile airstrip ya Mwanza?
 
Amesahau ujenzi wa kiwanja cha kimataifa Misenyi kule Kagera. Mkwere alipayuka iyo ahadi mwenyewe.
 
Huyo waziri anatakiwa kuweka juhudi , maarifa na wakati wake mwingi kwente TRL badala ya kupteza muda na ATCL

I dont see ATCL ina umuhimu gani kwenye uchumi wa nchi kama ilivyo TRL.

Kumekuwa na kasumba ya kuweka prority za Anga mbele zaidi ya zile za Reli.
 
Mtazamaji said:
...anatakiwa kuweka juhudi, maarifa na wakati wake mwingi kwenye TRL badala ya kupoteza muda na ATCL... Kumekuwa na kasumba ya kuweka prority za Anga mbele zaidi ya zile za Reli.
Anasema hivyo kwa kuwa anajua Tanzanians are not critical; $erikali iliyoshindwa kuendesha shuttle-train to Ubungo inakuja kusema itajenga flyovers ni kituko ambacho hakijatokea popote Duniani.
 
shirika hilo lipo ila kwa sasa lina kibajaji kimoja tu kinachoruka kwenda kigoma. mwanangu kama unaenda huko kikazi for 2 dys beba pesa ya hotel ya kutosha waweza kaa hata 5 dys kibajaji hakijaruka huko.

For him is good plan, but for us wit little hop kwa utendaji wa kibongo bongo, karibu waziri but this is TZ not Monterol ICAO

kuanzia Alhamisi hadi jumapili ndege iliharibikia Kigoma ndo imeanza safari jumatatu. Usafiri wa Kigoma ni shughuli hata uwe na pesa vipi ukiumwa ugonjwa ambao unatakiwa ufanyiwe rufaa ya muhimbili ndo umekufa hivyo. Tumsubiri mkwele aliesema Kigoma itakua kama DUBAI yaani hapo sijui Dar itakua kama nn? Harafu treni inaenda Kigoma mara moja kwa siku na kila siku inaenda imejaza abiria hadi inacheua lakin bado tunaambiwa shirika linaendeshwa kwa hasara, hakuna hata siku moja treni limesafiri tupu. Hata hiyo ndege ili upate nafasi inatakiwa uweke booking ya wiki moja kabla kila siku inajaa na bado tena wanasema wanakopa hadi hela ya mafuta hapo nashindwa kuelewa kabisa
 
lina kibajaji kimoja tu kinachoruka kwenda kigoma.

Lina Kibajaji kimoja ila wakurugenzi utashangaa

1. Deputy Director General
2. Director of Finance & Administration
3. Director of operations
4. Director of technical services
5. Director of man power development
6. Director of sales & marketing

Pia ikp bodi inayo ongozwa na Balozi Mustapha Nyang'anyi

Can we compare with Precision management?
 
lina kibajaji kimoja tu kinachoruka kwenda kigoma.

Lina kibajaji kimoja ila wakurugenzi utashangaa

1. Deputy director general
2. Director of finance & administration
3. Director of operations
4. Director of technical services
5. Director of man power development
6. Director of sales & marketing

pia ikp bodi inayo ongozwa na balozi mustapha nyang'anyi

can we compare with precision management?

duh!!!! Wote hao halafu ndege moja
 
mwandishi kaongopa.. waziri hakusema hivyo.. alichosema ni kwamba atahakikisha anavutia wawekezaji wa LOW COST CARRIER.. huyu mwandishi kasomea wapi.. du hii balaa.. journalists are not serious
 
Hivi huyu Mustapha Nyang'anyi bado ni mwenyekiti wa bodi ya ATCL hata baada ya kashfa aliyoifanya ya kutaka kuikodisha ndege kubeba mahujaji kinyemela halafu wakaishia kulala kiwanja cha ndege siku tatu!! Kama kweli bado yupo, hayo yatakuwa ndio matatizo ya mkwere kwani hutaka kuua nyani huku akiwaangalia usoni!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom