Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,175
Waziri 'ajitundika' ATCL
Imeandikwa na Lucy Lyatuu; Tarehe: 8th December 2010 @ 06:11 Imesomwa na watu: 52;
WAZIRI wa Uchukuzi, Omar Nundu amesema, anakusudia kuiwezesha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ijiendeshe kwa umahiri mkubwa ili ichangie kikamilifu katika kutoa huduma bora na nafuu za usafiri wa anga kwa wananchi.
Tangu ilipobinafsishwa kwa Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA), ATCL imeshindwa kuwa katika hali nzuri kibiashara na katika miaka ya karibuni, hali imekuwa mbaya zaidi kwani imekuwa na ndege chache, lakini ikiwa na wafanyakazi zaidi ya 300 wanaotegemea ndege zisizozidi tatu.
Baada ya ndoa yake na SAA iliyofungwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 kuvunjika, ATCL imekuwa ikijiendesha kwa shida, wakati mwingine ikiwa haina fedha za mafuta za kurusha ndege zake na pia fedha za kuwalipa wafanyakazi wake, hali iliyoilazimu serikali kusaka mbia wa kuiendesha.
Hata hivyo, mbia hajapatikana ingawa sasa inaelezwa kuwa imekuwa katika mazungumzo na Shirika la Ndege la Sonangol linalomilikiwa na serikali za China na Angola, ili awe mbia wao.
Lakini akizungumza Dar es Salaam jana kwenye kilele cha Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga, Nundu anayetoka katika tasnia hiyo ya masuala ya usafiri wa anga, alisema kusudio lake ni ATCL kuendeshwa kwa umahiri mkubwa ili lichangie kikamilifu katika kutoa huduma bora na nafuu kwa wananchi.
Kwa mujibu wa Waziri Nundu, kusudio hilo litakwenda sambamba na juhudi za kuandaa mazingira yatakayolenga kuongeza mchango wa sekta binafsi katika kujenga na kuendesha viwanja vya ndege.
Alisema kwa kuzingatia usafiri nafuu unafanikiwa, serikali itaboresha pia mazingira na kufungua milango ya biashara yenye kuvutia mashirika na kampuni mbalimbali kuwekeza katika sekta ya usafiri wa anga kama njia ya kuchochea ukuaji wa safari za ndege na ongezeko la idadi ya abiria.
Tutafanya juhudi za makusudi na kuchukuwa hatua za dhati kuhamasisha na kuvutia wawekezaji wa usafiri nafuu ili nauli zishuke kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuutumia usafiri huu na kufanya soko lake likue, alisema Nundu ambaye kabla ya kuwania ubunge wa Jimbo la Tanga Mjini na kushinda, alikuwa Rais wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).
Alisema kwa sasa serikali kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali, ipo katika hatua tofauti za uboreshaji wa viwanja vipatavyo saba nchini, ambavyo ni Arusha, Mafia, Bukoba, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Mpanda.
Kwa viwanja vya Mpanda na Mafia, uboreshaji umeshaanza na hivi sasa wataalamu wameshaanza kazi katika viwanja hivi huko Mbeya nako shughuli zinaendelea ambako ujenzi wa jengo la kufikia abiria na uwekaji lami katika njia ya kurukia katika Kiwanja cha Ndege cha Songwe unaendelea, alisema.
Ujenzi wa kiwanja kipya cha kimataifa cha Msalato mkoani Dodoma, ujenzi wa Kiwanja cha Kimataifa cha Bagamoyo na kuboresha Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kwa kujenga jengo jipya la abiria na majengo mengine ni baadhi ya miradi itakayopewa kipaumbele katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Aidha, aliagiza miundombinu ya viwanja vya ndege itumiwe kwa kazi iliyokusudiwa na sio kugeuzwa stoo ya kuhifadhi vitu kama ilivyo kwa karakana ya kutengenezea ndege iliyoko Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro.
Pia alitoa maagizo mbalimbali huku akitaka kupatiwa ripoti ya utekelezaji wake kila mwezi ikiwemo na kukamilishwa kwa kiwanja cha ndege cha Songwe kwa muda uliopangwa na kwa kiwango kilichoainishwa kwenye mkataba wa ujenzi na kupitia upya Sera ya Taifa ya Uchukuzi kwa kuwa sasa imepitwa na wakati.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Fadhili Manongi alisema sekta hiyo inakabiliwa na changamoto ya kukosa wataalamu wazalendo na waliopo wana umri mkubwa.
Kwa hivi sasa nchini kuna wahandisi wa ndege 221 na kati yao, Watanzania ni 108 tu na wahandisi 113 waliobaki ni raia wa nje, hali kama hiyo ipo pia kwa marubani ambapo takwimu zinaonesha wapo marubani 364 na kati ya hao, Watanzania ni 155 na wageni ni 209, alisema Manongi.