Waziri afurahia polisi kuwakamata maafisa wa TRA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri afurahia polisi kuwakamata maafisa wa TRA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 26, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  Date::10/25/2008
  Waziri afurahia polisi kuwakamata maafisa wa TRA
  Na Lilian Lugakingira, Bukoba.
  Mwananchi

  NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki amelipongeza Jeshi la Polisi mkoani Kagera kufanikiwa kuwakamata maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wanaodaiwa kusababisha kifo cha mfanyabiashara wa mjini Kayanga wilayani Karagwe, Amri Amir (54).

  Maafisa hao wawili, mmoja akitokea jijini Mwanza Kitengo cha Kuchunguza Wakwepa Kodi na mwingine wilaya ya Karagwe walikamatwa kufuatia kifo cha mfanyabiashara huyo ili waisaide polisi.

  Balozi Kagasheki alisema anatambua kwamba lazima serikali ikusanye kodi kutoka kwa wafanyabiashara, lakini sio kuitafuta kwa kutumia vitisho kama walivyofanya maafisa hao, na kudai kuwa wakazi wa Kagera wamechoshwa na vitendo wanavyofanyiwa na watu hao.

  Alisema hata kabla ya tukio hilo amekuwa akipokea malalamika kutoka kwa wananchi kuhusiana na tabia ya maafisa wa kitengo hicho mkoani hapa ya kuwatisha wananchi.

  Balozi Kagasheki alidai kuwa amepata taarifa kwamba maafisa hao walimfuata mfanyabiashara huyo na kumtishia hivyo kuanguka na kufariki kisha wakaingia kwenye gari lao na kutoroka kisha kukamatwa na polisi katika eneo la Buseresere wilayani Chato wakielekea Mwanza.

  Alisema, taarifa za uchunguzi zilizotolewa na wataalam marehemu alikufa baada ya kupasuka mishipa kichwani na kusababisha damu kuingia katika ubongo.

  Alimshukuru Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Henry Salewi ambaye baada ya kupokea taarifa kuwa watu hao wamekimbia na gari alipiga simu na kufunga mipaka yote ya kutoka mkoani hapa na kisha kupiga simu kwa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza ili kama wangekuwa tayari wamekwishaingia Mwanza wakamatwe na kurudishwa Kagera.

  Balozi Kagasheki alisema maafisa wa TRA hawazuiliwi kutafuta kodi kwa wananchi bali njia wanazozitumia sio nzuri.

  Kwa upande wake, Kamanda Salewi alikiri kushikiliwa kwa watu hao na kuwa wanaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo lililotokea Oktoba 23, mwaka huu eneo la Kayanga, wilayani Karagwe.
   
 2. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2008
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mbona huyu waziri anaonekana ni kama anawashutumu moja kwa moja hawa jamaa wa TRA wakati jamaa walikuwa kazini. Mbona ni kawaida tu watu wa mapato kufanya mahojiano hasa na wafanyabiashara ikiwa ni sehemu ya kazi yao? kama ni kuwakamata kwa ajili ya mahojiano na kufahamu wamechangia vipi kwa jamaa kupoteza maisha si ingekuwa kama kawaida tu na sio mtu kama waziri kulisimamia hilo suala kama vile ni kiongozi ndio kapoteza maisha. kwani kuna kimama na watoto wangapi wanapoteza maisha kila siku katika mahospital kwa kukosa huduma ndogo tu (e.g mwananyamala hospital), mbona hatuoni viongozi wakiwa makini na kufanya jitihada za ziada na haraka kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua kama tunavyoona kwa kifo cha huyu mfanyabiashara? mbona huyu waziri hajajiuliza ni kwanini mtu apatwe na pressure na hatimae kupoteza maisha kama hana matatizo yeyote kwenye mahesabu katika biashara yake? huyu kiongozi ni wale wale tu (wafanyabiashara wa Kagera) anajaribu kufanya namna ya kuwapunguza kasi hawa jamaa wa TRA ambao wameonekana kuwa kero kubwa kwa wafanyabishara wanaokwepa kodi hasa huko maeneo ya kanda ya ziwa.
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Kagasheki anakumbuka fadhila za mfanyibiashara huyu kwa ccm, katika nchi ambayo wafanyibiashara wanaofadhili ccm hawaguswi unategemea nini?
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kila mwenye akili anaweza kutegua kindawili hiki cha tabia aliyoionesha Mheshimiwa wetu mkubwa sana, Naibu Waziri. Kwani bila wafanyabiashara kuna CCM? Na kama siyo wao (Wafanyabiashara na mifweza yao) Nanihii na wapambe wake wangelikuwepo???
   
 5. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hivi ni lini watawala wataongea ukweli? Nani wakuaambia ukweli watanzania kuanzia kule kwenye grassroot?

  VIONGOZI WA DINI HII DHAMBI NI YENU, KAMA HUKUSOMA ELIMU YA DINI NENDA KASOME THEN URUDI OTHERWISE UNAONGEA DHAMBI TUU. Source of all these problem ni CCM. Hata kama ni TRA nyie CCM si ndio mmewalea?

  Asanteni
   
Loading...