Waziri aeleza alivyolambwa na FATAKI akiwa shule | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri aeleza alivyolambwa na FATAKI akiwa shule

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kashaijabutege, Dec 1, 2010.

 1. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Waziri atoa ushuhuda alivyorubuniwa na fataki
  Send to a friend Tuesday, 30 November 2010 21:23 0diggsdigg

  i Mwandishi Wetu

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Luoga Hovisa jana alitoas ushuhuda wa kusikitisha wa maisha yake katika kongamano lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), alipoeleza kuwa alipewa uja uzito na 'Fataki' wakati akisoma Chuo Kikuu.

  Waziri Luoga alilazimika kushirikisha vijana hao kuhusu maisha yake kutaka kuwaonyesha alivyomudu kuvumilia na kupambana na maisha hadi kufikia mafanikio aliyoyapata sasa, akisema badala yake sasa anaweza "kuchakachua" hadi wanaume watano lakini "haoni sababu" na kuwataka wanafunzi kuepuka watu wenye tabia za kifataki kwa kuwa wanaweza kuwaharibia mwelekeo wa maisha.

  Fataki ni jina maarufu waliopachikwa wanaume ambao wana tabia ya kufuata mabinti wadogo na kuwatelekeza baada ya kuwaharibia maisha kwa kuwapa mimba. Waziri Luoga alieleza jinsi alivyokutana na mwanamume huyo ambaye alimpa uja uzito, lakini akaongeza kuwa baadaye mtu huyo alimsomesha na hivyo kumaliza vizuri masomo. "Sio kwamba muige mfano nilioutoa," alisema Waziri Luoga akiwaambia wanafunzi hao. "Si kwamba na nyie kama wanafunzi mkayafanye haya, la asha! Badala yake ninawapa changamoto kwamba katika maisha silaha mnayopaswa kuing’angania ni elimu peke yake na si vibaka wa mitaani," alisema Dk Luoga. “Acheni kudanganywa na mafataki ambao ni matapeli na ambao huweza kuwapotezea dira ya maisha, badala yake msome kwa bidii, kwa ajili ya mafanikio ya maisha yenu.” Dk Luoga alisema kuwa vijana wengi, hasa wanafunzi wamekuwa wakirubuniwa kutokana na kushindwa kustahimili tamaa za maisha na kuamua kujiingiza kwa vijana wa mitaani ambao aliwaelezea kuwa hawana sera.

  Waziri huyo, ambaye ni sura mpya katika baraza lililoundwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete, alikumbushia taaluma yake ya ualimu kwa kutumia kalamu na kuwafundisha washiriki wa kongamano hilo masuala ya maisha na athari za ukimwi kwa vijana, huku akijitangza kuwa naye ni mtoto wa mkulima. “Ni bora kuacha kabisa na kuamua kusubiri kwani kwa kuwa mahusiano katika masomo ni hatari... badala yake mzidi kumuomba Mungu na kuwa waadilifu,” alisisitiza “Leo hii, ninamshukulu Mungu kwa Elimu aliyonipa kwa sababu alinijua mimi ni mtoto wa mkulima, hivyo niliamua kutochezea maisha yangu kiholela. "Hapa unavyoniona, kama waziri nina fedha za kutosha; gari la kifahari ninalo ehe! Unadhani nikitaka kuwa na mafataki hata watano, nitashindwa?" “Nikiamua kuchakachua wanaume hata watano, naweza kwa sababu uwezo ninao na fedha ninayo.

  Lakini sioni faida yeyote badala yake ni kujitumbikiza mahali ambapo ni hatari zaidi,” alisema. “Cha msingi hapa ni kuhakikisha mnajenga maadili mema mnapokuwa shuleni na nyumbani ili kuepuka kurubuniwa na kupoteza mwelekeo wa elimu mliopata.” Naye mtaalamu wa ushauri wa afya katika kamati ya vijana, Dk Telesphoy Kyaruzi alisema tatizo kubwa linalowapelekea vijana wengi kujiingiza katika ngono zembe na kupata maambukizi ni uchumi mbovu. Dk Kyaruzi alisema kwa kuliona hilo, wanaiomba serikali kuhakikisha inatoa mikopo kwa vijana ili kuwasaidia waweze kujiendesha na kuepuka vishawishi.
  Tuseme ukweli, aliyemlamba Dr. Terezya ni fataki kweli, au mama alipenda mwenyewe?
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Kiherehere chake tu
   
 3. M

  Makfuhi Senior Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hajatulia tu. hata hivyo kama sio huyo fataki angesoma vipi
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hata wanaowarubuni wa Vyuo vikuu wanaitwa mafataki?!!!1 Sasa wanaorubuniwa tena mwanafunzi wa chuo kikuu tumwiteje. Wachunaji
   
 5. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2010
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Huyo alitaka mwenyewe kwa raha zake, mbona alikubali kusomeshwa kwanini hakumshitaki kwa kurubuni. Alijua kuwa ni mambo ya nipa nikupe!
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Fataki wakati alikuwa chuo kikuu!

  Atumie neno jengine lakini sio fataki.
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo mengine inatakiwa busara kuyazungumza hadharani na hasa unapokuwa na nafasi kubwa kama ya uwaziri......ni mtazamo wangu tu masela msinipige mawe!!!!!
   
 8. M

  Msindima JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  What kind of ushuhuda is that? Hivi lengo lake lilikua kufundisha nini hapo?
   
 9. Muacici

  Muacici JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye red ni maana ya Fataki. Sasa tujiulize mwanachuo kikuu naye ni tunaweza kumwita binti mdogo. Yeye aseme alidanganywa na buzi na hatimaye likampa ujauzito. Hivyo tunaweza kusema alikuwa akilipa alivyopewa. Na akiwa amefikia katika umri huo alishindwa kujua cycle yake. Hii inaonyesha alivyo na upeo mdogo.... Hao ndio Mawaziri wetu!!!!!
   
 10. M

  Matarese JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Sasa ufataki wake upo wapi (mwanaume) wakati alimsomesha mpaka kafika hapo alipo?
   
 11. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hakuna wa kukupiga mawe..ni ukweli huo haikuwa busara kuongea hayo..
  Napata wasiwasi na aina ya viongozi wetu...wacha tusubiri..
   
 12. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ningekuwa mtoto wake ningeshajua nilizaliwa kwa bahati mbaya.....!
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  sawa kabisa, ...hawakukosea waliosema; "When you're up to your nose in shit, keep your mouth shut"
   
 14. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kaazi kweli kweli
   
 15. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nimeshangaa kidogo japo si sana. Kutoa ushuhuda ni kitu kizuri lakini inategemea ushuhuda wenyewe na nafasi yako katika jamii.Huyu Waziri hakupaswa kuthubutu ki hivyo kwenye kadamnasi au hadhira ile. Ingetosha kama angetumia mkasa huo na kuwaonyesha vijana wale kuwa kuna mtu alipatikana na janga kama lile lakini hatimaye alipambana na kuweka kujenga tena upya maisha yake kwa kiwango cha juu.
  Kwanza hakutokewa na Fataki maana fataki hufuata watoto wa shule na siyo wasichana wakubwa wa vyuo vikuu.Siyo siri kuwa vyuoni huk ndiko masugar daddy hujivinjari kutafuta wasichana wale wenye kupenda makuu kama pesa na mambo ya anasa.Ushuhuda wa waziri huu unakwaza zaidi badala ya kutoa funzo!

  WITO: VIONGOZI WAJIHADHARI SANA WANAPOTAKA KUONGEA KWENYE HADHARA MAANA KILA WASEMACHO KINAPEMBULIWA KWA MAPANA YAKE.
   
 16. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Amejuaje uwezo wake wa kuchakachua wanaume ni watano? Ashajaribu?

  Sasa according to u, huyu i fataki au mwanaume ulie mchakachua aka uliemchuna?

  Fundisho hapo ni nini? Mafataki ni wazuri kwasababu wanasomesha eh?

  "

  Nazidi kuchanganyikiwa, yaani wahakikishe wanapata mafataki ya kuwasomesha badala ya vibaka wa mtaani? Kweli wewe ni mchakachuzi!


  Tatizo lako unadhani tayari umefika ... au ulichakachua kwanza ndo ukapata nafasi hiyo?
   
 17. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  By the way jamaa alimsomesha tu a u na kumuwowa kabisa? maana from my point of view kamdhalilisha mfadhili wake, au keshapata Godfather mpya ndio anamuona ni fataki?
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  The next sophia simba. Mh! Tena huyu mama anaonekana ni mchakachuaji toka msingi. Ashukuru Mungu alizalishwa akapata fursa ya kufika hapo
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Dec 1, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani waziri mzima anasimama na kuzungumza bila aibu kuwa alifanya ngono teana alipigwa KAVU KAVU wakati anasoma na MIMBA JUU....kweli tanzania in mawaziri..ndo shida ya kuokota wauza bar unawapa uwaziri kisa wana sura nzuri madhara yake ndo haya
   
 20. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #20
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  [FONT="Comic Sans MS[SIZE="4"]"]Mwanamke hata angekuwa Prezidenti atabaki kuwa mwanamke ndio mama zetu hao , dada zetu, wake zetu na mabinti zetu kwa hiyo ni sahihi kwake kusema hivyo kwa sababu anafikiria hivyo. Asimlaumu sana huyo Fataki kwa sababu chupi aliivua mwenyewe hakulazimishwa na mtu. Fataki akanogewa na kumsomesha akamsomesha sasa anamsaliti. Nakwambia hata mkeo anaweza kukutenda hivi muulizeni Aminieli Mahimbo atawaambieni.[/FONT][/SIZE]
   
Loading...