Waziri abaini upigaji milioni 520 za NHIF mkoani Kilimanjaro

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,547
1626166584733.png
UKAGUZI maalum unaoendelea kufanyika katika miamala ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) umebaini kuwepo kwa ubadhirifu wa zaidi ya milion 520 mkoani Kilimanjaro.

Ubadhirifu huo unaohusisha watumishi sita wakiwamo kutoka na hospitali za rufaa ya Kanda KCMC na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi unaitaja KCMC kuongoza kwa ubadhirifu wa zaidi ya milioni 245 kwa kugushi nyaraka na kujipatia fedha hizo kinyume na sheria.

Akizungumza baada ya kikao kazi na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro wakiwamo wakuu wa hospitali za KCMC, Mawenzi na wale wa bima ya Afya, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel kuhusu tuhuma ya kuwapo kwa udanganyifu huo alitaka hatua za kinidhamu na sheria kuchukuliwa.

Alisema ubadhirifu huo umefanywa na baadhi ya watumishi kwa kushirikiana na baadhi ya maduka ya dawa za binadamu ambayo uchunguzi unaendelea kubaini cheni zaidi.

Dk. Mollel, alisema serikali itakwenda mikoa yote nchini ili kufanya uchunguzi huo na kwamba wapo baadhi ya watumishi wamekiri kuhusika na udanganyifu huo na wameanza kurejesha fedha walizojipatia.

Aidha naibu waziri amezitaka taasisi na maduka yanatoa huduma za afya kujaza fomu za bima za afya kwa madai halali na kila mtanzania kuhakikisha kadi yake ya afya inatumika kufanya malipo halali.

Aidha amewataka wote wenye nia ya kufanya ubadhilifu wowote kuacha mara moja kwani lazima watajulikana na kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwani bado uchunguzi unaendlea na unafanyika katika mikoa yote nchini.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai ameviagiza vyombo vya usalama kuwakamata wote waliohusika nakuchukuliwa hatua za kisheria pamoja na kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa.

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hasani kupitia bajet ya mwaka huu 2021 imetenga kiasi cha zaid ya sh Bil 148 kwa 9ajili ya kupeleka katika mfuko wa bima ya afya kwenda kusadia wananchi maskini na wasiojiweza.

Hata hivyo Kagaigai amewataka watumishi wa umma kuwa waaminifu kwani fedha za serikali zimelenga kuwasaidia wa Tanzania wote.

Nipashe
 
Back
Top Bottom