BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,820
- 287,886
Waziri aagiza maafisa habari kujibu mapigo serikali ikipigwa madongo
Na Joseph Ishengoma, Morogoro
Mwananchi
SERIKALI imewaagiza maafisa habari elimu na mawasiliano wa wizara na idara za serikali kujibu tuhuma zinazotolewa na wananchi dhidi ya serikali na viongozi wake bila sababu wala ushahidi.
Agizo hilo lilitolewa jana mjini Morogoro na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Seif Khatibu wakati akifungua mkutano wa maofisa habari na mawasiliano wa wizara na idara za serikali.
"Baadhi yenu nyinyi badala ya kujibu haraka mapigo mnafunga midomo na mikono na kuiacha serikali inapigwa makombora kushoto na kulia. Tabia hii lazima ikome, afisa ambaye anaona wizara ama kiongozi wake anatupiwa madongo bila kutafuta majibu haraka hajui wajibu wake. Lazima serikali ijibu mapigo kwa kasi, usahihi na ufanisi," alisema Waziri huyo.
Khatibu alisisitiza kuwa, ni jukumu la maafisa hao kuhakikisha majibu yanapatikana na kuwa, kama kuna kiongozi asiyependa kutoa majibu afikishwe ngazi za juu zaidi.
Alisema ofisi yake itapenda kupata taarifa za viongozi wasiotaka kutoa majibu, na kama majibu yatakuwa yamekwama kwa waziri nipewe taarifa kwa kuwa ni mwanasiasa mwenzao ili niwasiliane nao," aliongeza kusema.
Vilevile amewaagiza makatibu wakuu wa wizara kuhakikisha wanatenga bajeti ya kutosha ili kuimarisha vitengo vya habari, elimu na mawasiliano ili kusaidia kutangaza sera na shughuli zinazofanywa na wizara zao.
Kwa mujhibu wa Waziri huyo, kushindwa kutenga bajeti ya kutosha kunadumaza haki ya wananchi ya kupata habari ambayo ni haki yao ya msingi ya raia.
"Kila mtu anayo haki ya kutoa na kupata habari. Kutokana na umuhimu huu, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na Jamhuri iya Muungano wa Tanzania zimeweka katika katiba zao vifungu vyenye kuhakikisha wananchi wanapata haki ya kupata na kutoa habari, "alisema.
Katika hatua nyngine; Khatibu amevipongeza vyombo vya habari kwa kufuata maadili ya uadishi wa habari na kuimarisha umoja na uzalendo kwa taifa na kusaidia serikali kutatua kero za wananchi.
Agenda kubwa ya mkutano huo ni kuangalia jinsi sauti ya serikali na taasisi zake zinavyosikika katika vyombo vya habari kwa lengo la kuwasaidia wananchi kujua kazi inayofanywa na serikali yao.
Mkutano huo wa siku tano unajumnuisha maafisa habari, elimu na mawasiliano wa wizara na idara zote za serikali.