Waziri aagiza kampuni, waongoza watalii wanaochafua taswira ya nchi kufutiwa leseni

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro ameiagiza Bodi ya Leseni ya Biashara za Utalii nchini (TTBL) kuzifuta leseni kampuni za utalii na waongoza watalii wanaochafua taswira ya nchi kwa kufanya matendo yasiyofaa kwa watalii ukiwamo wizi na utapeli.

Aidha, ameiagiza bodi hiyo kuhakikisha mawakala wa biashara za utalii wananunua bidhaa zilizopo nchini, badala ya kuzinunua nje ya nchi na kuziuza kwa watalii kwa bei ya juu.

Alitoa maagizo hayo katika hafla ya kuzindua bodi hiyo yenye wajumbe 12 akiwemo Mwenyekiti wa Bodi hiyo inayoundwa na wataalamu kutoka sekta binafsi na wengine kutoka taasisi za serikali.

Alisema zipo kampuni za utalii zilizopewa leseni ya kuendesha biashara za utalii na bodi hiyo, lakini zimekuwa zikiwatapeli watalii linalosababisha madhara katika sekta ya utalii nchini.

Kwa mujibu wa Dk Ndumbaro, wapo waongoza watalii ambao ni vinara wa kuiba mali za watalii na kwamba, vitendo hivyo vinaikichafua nchi katika uso wa dunia.

"Ninyi bodi mna mamlaka ya kutoa leseni na kuifuta leseni, hakikisheni mnawafutia leseni waongoza watalii pamoja na kampuni za utalii zinazokiuka maadili katika sekta utalii," alisisitiza.

Alisema katika uongozi wake hatarajii kuona watalii wanaibiwa mali zao wala kutapeliwa ilihali kuna bodi iliyopewa jukumu la kushughulikia changamoto hizo.

Alisema baadhi ya hoteli zimekuwa na kasumba ya kuagiza vyakula ikiwemo nyama pamoja na viungo mbalimbali zikiwemo nyanya kutoka nje ya nchi wakati bidhaa hizo zinazalishwa nchini jambo lilofanya vyakula hivyo kuuzwa kwa watalii kwa bei kubwa na pia, kuikosesha nchi mapato yatokanayo na watalii kununua bidhaa zinazolishwa nchini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Leseni ya Biashara za Utalii (TTBL), Saleh Pamba, alimhakikishia Waziri Ndumbaro kuwa, watatekeleza maagizo aliyoyatoa na kufuata sheria.

Pamba alisema hadi sasa kampuni za utalii zaidi ya 2,000 zimepewa leseni na kwamba, idadi hiyo ni ndogo hivyo watahakikisha idadi inaongezeka na wote waliopewa leseni wanalipa kodi stahiki kwa serikali.
 
Kampuni ziko zaidi ya 2000 lakini zenye hadhi na uwezo na mtaji wa kujiendesha kama kampuni hazifiki hata 50!

Zinazobakia 1950 Ni kampuni za mfukoni na karatas za ujanja ujanja mtupu!! Blaablaa Mingi mdomoni na kusuka suka rasta kichwani kwishwaaa!

Kwa mazingira kama hayo SCAMS IS INEVITABLY.
 
Back
Top Bottom