kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,222
- 1,670
Waliopata kikombe cha Babu wa Loliondo wazidi kupoteza maisha. Utafiti uliofanyika wa idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi ktk Wilaya na Mkoa wa Geita inasemekana imeongezeka kufuatia hatua ya baadhi ya wagonjwa kuacha kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi. Mratibu wa Ukimwi ktk Kitengo cha Matibabu ktk Wilaya ya Geita, amesema watu waliamini kuwa babu alikuwa na dawa ya kutibu ugonjwa wa Ukimwi licha ya kutambua kuwa HAKUNA DAWA ILIYOTHIBITISHWA NA WATALAAMU. Source by Mwananchi - jumatatu.